Ni lazima ku'unstall' Jamii Forums kwenye kompyuta zote nchi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni lazima ku'unstall' Jamii Forums kwenye kompyuta zote nchi.

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by TUJITEGEMEE, Apr 12, 2012.

 1. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  CHAMA kikubwa sana cha siasa katika nchi ya Lyabishuuri kiliamua kuitisha mkutano wa dharura kupitia kurugezi yake ya propaganda na Mipango.

  Dharura hii ilitokana na kuona Jamii Forums imefanikiwa kuwaelimisha raia wa nchi hiyo, hivyo kada wa chama hicho kushindwa kuwaibia raia kwa raha kama zamani.

  Ilikudhibiti wimbi hili la JF kuwatilia mchanga kitumbua chao cha kujipenda wenyewe, basi kikao hicho cha dharura kiliazimia kuiagiza serikali ya chama hicho kuhakikisha kuwa IT specialists woote walioko nchini humo kuanza mara moja kazi ya ku'unstall' Jamii Forums kwenye kopyuta zote zilizoko nchini humo na kuhakikisha wana install ANTIJF ya kuzuia Jamii forums is 'run' kwenye kompyuta hizo na zile zote zinazoingizwa nchini humo.

  Bajeti ya kazi hiyo ilipitishwa bila kupingwa

  Source>>>http://www,RaiaMbea,blogsports,com
   
 2. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  Imegundulika kuwa kuna baadhi ya washiriki wa kikako hicho cha dharura hawakuwa na elimu ya IT hivyo maamuzi yao yalikuwa ya kufuata mkumbo.

  Baada ya mmoja wao kupata elimu ya awali ya masuala ya IT, amegundua kuwa haiwezekani ku'UNSTALL' JF, hivyo IT specialist wa Chama waliwapotosha na amejaribu kuwaeleza uwongo huo. IT wa Chama wamemgeuzia kibao na kuanza kusema mshiriki huyo wa kikao alikuwa MZIGO.

  Ilitarajiwa jana mshiriki aliyeitwa mzigo kutoa maamuzi magumu juu ya hatima yake ushiriki katika Chama hicho.Pia inasemekana ataanzisha CHUO KIKUU kitakacho kuwa kinatoa digree za uzamili katika masuala ya kutumia COPY na PASTE command, baada ya kugundua kuwa kuna matatizo ya uelewa wa mamabo ya IT nchini humo.

  Nitawajuza zaidi
   
Loading...