Ni lazima kutumia kiingereza kuonesha msisitizo?

Mtuache

Member
Mar 12, 2021
49
125
Habari za wakati huu,
Nimekuwa nikisoma nyuzi mbali mbali humu Jamii Forums na nimefurahishwa nazo. Ila sifurahishwi na hii tabia ya mtu kupachika mstari wa kiingereza eti ndo kuonesha Msisitizo wa Mawazo yake.
Kwa mfano, utakuta mtu anaongelea kuhusu kutokuwepo kwa Mungu, anaadika hivi "kiuhalisia hakuna Mungu THERE'S NO GOD......"

Kwani ukitumia kiswahili tu hutoeleweka? Yaani sababu kuu kwa kutumia kiingereza katikati ya uzi wako ni nini? Ingekuwa labda kuna neno unataka kulisema lakini hujui kwa kiswahili sawa ila sio kutafsiri kile kile. Yaani umeandika sentensi ya kiswahili alafu mbele unaandika hiyo hiyo ila kwa lugha ya kiingereza

Sisemi kwamba msitumie kiingereza hapana, tumieni. Maneno yangu mimi sio sheria.

Karibuni kwa maoni.
 
Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
6,647
2,000
Watu wanafikiria ukimtumia lugha ya malkia kuwa una akili na umesoma sana. Kumbe sivyo, mtoto akiongea hiyo lugha kwa ufasaha haimaanisha kasoma sana au ana akili sana. Mtu hata formula moja ya hesabu hajui ila lugha ya malkia inapanda. Ukiamua kiswahili usichanganye. Nafikiri wanaochanganya wakiambiwa waongee kwa mfululizo utashika mbavu.
 
Natty Bongoman

JF-Expert Member
Oct 10, 2008
253
195
Habari za wakati huu,
Nimekuwa nikisoma nyuzi mbali mbali humu Jamii Forums na nimefurahishwa nazo. Ila sifurahishwi na hii tabia ya mtu kupachika mstari wa kiingereza eti ndo kuonesha Msisitizo wa Mawazo yake.
Kwa mfano, utakuta mtu anaongelea kuhusu kutokuwepo kwa Mungu, anaadika hivi "kiuhalisia hakuna Mungu THERE'S NO GOD......"

Kwani ukitumia kiswahili tu hutoeleweka? Yaani sababu kuu kwa kutumia kiingereza katikati ya uzi wako ni nini? Ingekuwa labda kuna neno unataka kulisema lakini hujui kwa kiswahili sawa ila sio kutafsiri kile kile. Yaani umeandika sentensi ya kiswahili alafu mbele unaandika hiyo hiyo ila kwa lugha ya kiingereza

Sisemi kwamba msitumie kiingereza hapana, tumieni. Maneno yangu mimi sio sheria.

Karibuni kwa maoni.
Habari nzuri,
Nahisi ni madhara ya ukoloni mamboleo manake wahusika wengi sasa ni wale ambao hawakutawaliwa na wakoloni. Lingine la kufanana ni msisitizo wa mavazi ya suti na tai kuwa ndo umetoka kistaarabu... nahisi bungeni utatimuliwa ukivaa lubega ila utapigiwa makofi ukitinga na suti kali ya ng'ambo.

Ukoloni mamboleo umepanuka. Hauteki nchi tu, unateka bongo za wananchi na kuwatengenezea fikra na imani mpya. Hautumii bunduki mara nyingi siku hizi - unatumia dini, vitabu, vyombo vya habari na vya burudani, na sasa mfumo wa digitali kiujumla.

Bongo zetu zikiwa chonjo tutajifunza kimombo ili wasitutete ama kutupa mikataba lugha mzunguke. La sivo, tutajifunza kimombo kwao pamoja na tabia afu tukirudi tunataka kuitwa John Smith na tunaishi kama hatujawahi kukanyaga matope wala kula kwa mama ntilie.
 
Umeongea point sana kiongiz. Shukrani
 
mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
7,037
2,000
Mkuu unapaswa ujuwe kwamba hii lugha ya Kiswahili unayozungumza Leo bado inaendelea kukuwa kwa maneno mapya Kasi Sana ya 5G,,

kila siku kuna maneno mapya yanaingizwa ktkt kamusi ya Kiswahili..

Mawazo yako unayoleta Leo hapa,,kama miaka 100 nyuma wangekuwa na mawazo kama yako Nina Imani Kiswahili kisingekuwa kimepanuka hata sasa.

Kumbuka Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha zaidi ya 4 na kote ni ktk kukikuza na kukifanya Kiswahili kiwe kipana zaidi.

Hata baada ya miaka 100 ijayo, kuna maneno ambayo yatazidi kuongezwa ktk kamusi..
English.
French.
Arabic.
Hindi.
Zote zimechangia kukamilisha lugha ya Kiswahili.

Kuongeza maneno ya kingereza ktk kuelezea Jambo ,ni ktk njia moja wapo ya kukuza Kiswahili kwa maneno mapya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom