Ni lazima kumwita mbunge mheshimiwa?

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Jamani, mi nimezaliwa nkakuta wabunge, madiwani na kwa hali ya juu mawaziri na rais wakiitwa waheshimiwa. Napenda nijue kuna hadhabu gani ya kisheria au kikanuni iwapo ntamwita kwa jina lake?

Mi sipendi kwakuwa waliowengi hawana vigezo. Mnisaidie
 
they never deserve tht title. They don perform as hons.
Hakuna sheria wala kanuni inayomlazimisha raia (mpiga kura) kumwita mbuge wake au mwingine Mheshimiwa. Wao wenyewe ndio waliamua kuitana hivyo wakiwa ndani ya Bunge. Sisi haituhusu. Kwa hiyo ni rukhsa kumuita mbunge ndugu, hullo, au mshikaji kama mmezoeana, n.k.
 
halafu wanapoteza muda mwingi kuitana mheshimiwa spika,mara mheshimwa ..........,.....this is stupid
 
Muhashimiwa Paulo, hata wewe ndiye muheshimiwa. kila mtu anastahili heshima. Vinginevyo wengine ni wadharauliwa.
 
ukimwita mbunge mheshimiwa automatic wewe unakua mdharauliwa.
 
Hivi ni lazima kumuita mzazi wako wa kiume baba? au usipomuita atabadilika kuwa baba au ukimuita ndio ubaba unazidi? nauliza tu
 
Kwakuwa wana JF wamechangia kwa umakini mkubwa hoja zinazogusa maslahi ya nchi,
Na kwakuwa serikali inafuatilia hoja za wanaJF kwa umakini mkubwa,
Na kwakuwa tuna wabunge wanaosoma na kuchangia hoja JF,
Je,bunge halioni wakati umefika na sisi wanaJF tutambuliwe rasmi bungeni kama WAHESHIMIWA?
 
Hivi ni lazima kumuita mzazi wako wa kiume baba? au usipomuita atabadilika kuwa baba au ukimuita ndio ubaba unazidi? nauliza tu
Sio lazima ila unatakiwa umuite Baba, inapendeza zaidi hii inasaidia kumtofautisha na mtu mwingine. Ni vizuri Wabunge kuitwa Waheshimiwa ili wajiheshimu na kuheshimu kazi yao.
 
Sio lazima ila unatakiwa umuite Baba, inapendeza zaidi hii inasaidia kumtofautisha na mtu mwingine. Ni vizuri Wabunge kuitwa Waheshimiwa ili wajiheshimu na kuheshimu kazi yao.

Nakubaliana na wewe asilimia 100, ila tatizo linalojitokeza ni wananchi sasa hivi kuchagua vituko badala ya wawakilishi ndio maana wengi wetu tnaona ukakasi kulitumia hili jina, hivi hata Maji marefu kweli nimuite Mheshimiwa mganga maji marefu?
 
si lazima............ especiaaly kutokana na maigizo wanayocheza bungeni
 
Back
Top Bottom