Ni LAZIMA Kamanda Kamuhanda naye apande kizimbani...

mimi mwenyewe naunga mkono ya kuwa kamhanda naye anatakiwa aende polisi ijapokuwa na yeye ni askari kwani amefanya maovu makubwa najiuliza tume iliyoundwa ni kweli ni tume iliyo huru kiasi kwamba sisi wananchi tuiamini kwa upande wangu ni kitu ambacho hata siafiki kwani watuhumiwa wanafahamika na wanaonekana kwenye picha je hapo tume ya nini kikubwa ni kuawa wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo husika kama walivyo watuhumiwa wngine
jamani watz wenzangu kumbe siku hiyo yanatokea mauaji huko ilinga ccm pia ilikuwa na mkutano wao wa chama na hakuna aliyewaingilia kwenye kikao chao au ndo kusema kuwa wao wako juu ya sheria kuliko vyama vingine pia siku hiyo nasikia kuwa tindu lisu alikuwa arusha kwenye mkutano wa hadhara lakini fujo haikutikea kwa nini iwe ilinga peke yake hapo bado mimi bado sijaelewa na kama suala lilikuwa ni sensa mbona wao walifanya mkutano je suala la sensa ni kuwa lilikuwa ilinga peke yake kwa nchi ambazo zinafuata utawala wa sheria sual hili waliohusika wangekuwa tayari wamekwisha kwenye vyombo husika lakini kwa kuwa ni tz ndo maana linapigwa danadana kila kukicha
kuna suala la waandishi wengine watatu ambao hadi sasa tunasikia kuwa wanatafutwa na polisi kama watuhumiwa je wamekosa nini mbele ya hawa polisi dhalimu mmoja wa hawa waandishi wa habari alipokwenda mwenyewe kujisalimisha kwa polisi polisi walikana ya kuwa walikuwa hawamtafuti lakini ukweli ni kuwa walikuwa wanamtafuta kwa udi na uvumba
lakini pia ilithibitika ya kuwa polisi wenyewe walikiri kwa vinywa vyao ya kuwa walikuwa wanashinikzwa na wakuu kutoka juu bila ya matakwa yao wenyewe
jambo jingine ni kuwa RPC wa wa mkoa alitaarifiwa na mmoja wa raia ya kuwa anayepigwa si mwanaharakati bali ni mwandishi wa habari lakini polisi waliendelea kumpiga hadi kumtoa uhai
kwa namna hii tutafika kweli
 
Ina-aminika nae alipokea maagizo toka juu sasa hapa MMM itakuwaje, watu wa juu wamkandamize ama wampongeze kwa kutekeleza maagizo yao. hii ni ndoto! kama Kamuhanda akipanda inabidi na IGP,Chagonja na Nchimbi wawe wa kwanza. ( watoa maagizo)
 
Ndo kawaida yetu kufanya mambo kinyumenyume!Yani tunaanzia chini kwenye uwajibikaji kama tatizo liktokea,only in Tanzania hilo linaonekana kuwa ni kawaida.Aliyetoa order yuko kazini na aliowatuma wanashitakiwa,halafu tunakubali kabisa kuwa itatendeka ama imetendeka.Sijui ni kufikiri kwa aina gani huku.
 
Bila Kamanda Kamuhanda kusimamishwa kazi na kuunganishwa katika kesi ya mauaji ya Daud Mwangosi hatua yoyote dhidi ya askari waliokuwa chini yake itakuwa ni ya uonevu. Na yeye apandishwe kizimbani kama mshirika wa mauaji. Ni mtu pekee aliyekuwepo eneo la tukio ambaye angeweza kuzuia mauaji lakini hakufanya hivyo.

Alitakiwa awe na yeye amesimamishwa kazi na kutokuwa sehemu ya uchunguzi wa polisi isipokuwa kama mtuhumiwa na mshukiwa wa mauaji ya Mwangosi. Kutomshtaki au kujaribu kutengeneza mashtaka nje ya yale yanayowakabili askari waliokuwa chini yake.

Naweza hata kwenda mbali zaidi - mtu pekee ambaye anatakiwa awe wa kwanza kutiwa pingu na kushtakiwa kijeshi kwanza ni Kamanda Kamuhanda. Avuliwe kwanza vyeo vyake vyote halafu atiwe pingu kusimamishwa katika mahakama ya kiraia...

Kamuhanda aliorder wale askari wamuue na akasimamia mauaji hadi mwisho. Picha zinaonyesha vizuri sana kuanzia David alivyokuwa anamjoji.
Tanzania kwa sasa hakuna sheria wala nini. Ameua na anasonga mbele kuuwa wengine kama alivyoanzia huko Songea na kwingineko. Kama ana dhamira na anaamini kuwa kuna Mungu wa wanyonge, ajisalimishe na awajibishwe. Kama kwake mwisho wa Yote ni Mwema na Kikwete, basi anaendelea kudunda na kuuwa watanzania wasio na kosa ilimradi watawala wa nchi wanafaidi chini ya CCM.
Mimi ninamshauri aangalie mbali zaidi kwani siku yake ya hukumu haiko mbali. Mungu aliyewaumba hao anaowaua atamkuta angali bado kazini. Anaijua leo haijui kesho. Kwake kifo kitakuwa kigumu kuliko hao wote ambao ameshawaua na kuwatesha kwa kutumia nguvu ya walipakodi. Watanzania hatujalala kiasi hicho. Tunamlilia Mungu na atajibu kilio chetu na cha hizi familia alizoziliza kiasi hiki! Mungu ibariki Tanzania.
 
Hatua kubwaaaa itakayochukuliwa kwa kamuhanda itakuwa kumrudishaa makao makuu akastafu vizuri,nchi hii bwana chini ya ccm ni balaa tupu na laana!
 
Waziri Nchimbi ni tatizo kuliko ukoma katika siasa`za nchi hii, ana umafya na hila na IGP asipoangalia itakula kwake kama atafanyia maelekezo yake bila tahadhali.
 
Bila Kamanda Kamuhanda kusimamishwa kazi na kuunganishwa katika kesi ya mauaji ya Daud Mwangosi hatua yoyote dhidi ya askari waliokuwa chini yake itakuwa ni ya uonevu. Na yeye apandishwe kizimbani kama mshirika wa mauaji. Ni mtu pekee aliyekuwepo eneo la tukio ambaye angeweza kuzuia mauaji lakini hakufanya hivyo.

Alitakiwa awe na yeye amesimamishwa kazi na kutokuwa sehemu ya uchunguzi wa polisi isipokuwa kama mtuhumiwa na mshukiwa wa mauaji ya Mwangosi. Kutomshtaki au kujaribu kutengeneza mashtaka nje ya yale yanayowakabili askari waliokuwa chini yake.

Naweza hata kwenda mbali zaidi - mtu pekee ambaye anatakiwa awe wa kwanza kutiwa pingu na kushtakiwa kijeshi kwanza ni Kamanda Kamuhanda. Avuliwe kwanza vyeo vyake vyote halafu atiwe pingu kusimamishwa katika mahakama ya kiraia...

Usishange ukisikia alisha staafu.....wapi Zombe?
 
"Sin by omission", anaangukia hapo huyo Kamuhanda!
Yani dhambi kwa kutokutimiza wajibu.
Na atendewe kama inavyostahili!
 
Anayeua polisi, anayepeleleza polisi na anayefikisha jalada kwa Feresi ni nani? Conflict of interest! hakuna kitu hapo
 
Nothing will make sense kwenye huu uchunguzi wa mauaji ya Daudi Mwangosi kama RPC Kamuhunda atabakia ofisini. Nothing. Na kadri siku zinavyopita na huyu mkubwa bado yuko ofisini ndivyo jeshi la polisi na serikali nzima inazidi kuchafuka.
 
Waandishi wa habari, njia pekee ya kuhakikisha viongozi wakuu wa jeshi la polisi nchini na waziri Nchimbi wanawajibika ni kususia kuandika habari zote za jeshi hilo nchi nzima.

Huu mkakati wenu wa kutoa siku 40 si dawa hata kidogo, kwani siku 40 si nyingi na zitakwisha na baada ya hapo mtaendelea kuandika.

Sasa hapo nani atakuwa mshindi?Polisi au wanahabari?

Msitarajie watawajibishwa.Jiulizeni hawa walifanywa nini
1.Jairo.
2.RPC wa Arusha.
3.Watekaji wa Dr.Ulimboka.
4.RPC wa Morogoro.
5.Wezi wa fedha za EPA,kagoda,richmond,meremeta n.k.

Hii ndio sera ya watawala wetu.

Na msisahau kuwa wana uzoefu wa kutosha wa kufunika kombe mwanaharamu apite.
 
Ni mwaka huu miezi ya mwanzo,yalitokea mauaji songea,police kuua raia,kamanda wa mkoa akiwa ni Kamuhanda,tume ikaundwa akahamishiwa Iringa, Iringa nako mauaji yametokea akiwa kamanda wa mkoa,,je ni nini hiki? Atahamishiwa wapi baada ya mauaji ya Iringa?
 
Hata IGP yalipotokea mauaji ya mahabusu kule Rujewa kapandishwa na cheo, Na Mahita alipompiga mabomu Mrema kapata Ukuu wa polisi, Haka kamchezo kakukuua kanapandisha cheo Tanzania
 
Ni sawa yule askari kuburuzwa kotini maana ndo tulichokuwa tunakitaka, lakini hakuwa mwenyewe, alikuwa na kundi la askari wengine. Lakini Muuaji mkuu RPC Kamuhanda anapaswa kuburuzwa kotini mapema, yeye ndiye aliye mchochea yule police kumlipua Mwangosi. Kamati ya Nchimbi haiwezi kuendelea kuchunguza jambo lililoko mahakamani, wananchi walisema wauaji wanajulikana tume ya nini?
 
Ni mwaka huu miezi ya mwanzo,yalitokea mauaji songea,police kuua raia,kamanda wa mkoa akiwa ni Kamuhanda,tume ikaundwa akahamishiwa Iringa, Iringa nako mauaji yametokea akiwa kamanda wa mkoa,,je ni nini hiki? Atahamishiwa wapi baada ya mauaji ya Iringa?

atahamishiwa mwanza kwenye upinzani
 
Back
Top Bottom