Ni LAZIMA Kamanda Kamuhanda naye apande kizimbani... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni LAZIMA Kamanda Kamuhanda naye apande kizimbani...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 8, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Bila Kamanda Kamuhanda kusimamishwa kazi na kuunganishwa katika kesi ya mauaji ya Daud Mwangosi hatua yoyote dhidi ya askari waliokuwa chini yake itakuwa ni ya uonevu. Na yeye apandishwe kizimbani kama mshirika wa mauaji. Ni mtu pekee aliyekuwepo eneo la tukio ambaye angeweza kuzuia mauaji lakini hakufanya hivyo.

  Alitakiwa awe na yeye amesimamishwa kazi na kutokuwa sehemu ya uchunguzi wa polisi isipokuwa kama mtuhumiwa na mshukiwa wa mauaji ya Mwangosi. Kutomshtaki au kujaribu kutengeneza mashtaka nje ya yale yanayowakabili askari waliokuwa chini yake.

  Naweza hata kwenda mbali zaidi - mtu pekee ambaye anatakiwa awe wa kwanza kutiwa pingu na kushtakiwa kijeshi kwanza ni Kamanda Kamuhanda. Avuliwe kwanza vyeo vyake vyote halafu atiwe pingu kusimamishwa katika mahakama ya kiraia...
   
 2. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hiyo ngumu Mzee Mwanakijiji,kwa tz hii bado sana! Mikono yake ina damu ya watu wale wa Songea,haikuchukuliwa hatua yoyote akahamishwa Mkoa tu.
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Si ajabu na yeye akaongezwa kwenye kamati ya uchunguzi, yaani akawa mwanakamati.
   
 4. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni nani wa kushikilia jalada la upelelezi dhidi yake
  ikiwa wanaohusika na upelelezi ni polisi wenyewe, tena
  inawezekana ikawa ni wale wale aliowatuma...
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Hapa ndio naona kupwaya kwa feleshi
   
 6. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,731
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Si nasikia eti alidai umri wake umesogea na anakaribia kustaafu na pia eti anaipenda kazi yake kwa hiyo alihakikisha ubinafsi huo huo unamfanya awatumikie mabosi zake walioko madarakani kwa gharama yoyote?Na kwa watawala hawa dhalimu hakuna sadaka inayowapendeza kama damu ya raia wema kwa kisingizio cha kuwathibiti CHADEMA. Sasa MM huoni hapo Kamuhanda atapatikana na kile kitu alichokuwa anakiogopa na kujiepusha nacho?

  Sote hapa tunajua kuwa ni vigumu sana haki na ukweli kufahamika kutoka upande wa serikali. Kwa sababu tokea mwanzo kabisa nia ya Jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla vilionekana vizuri tu....KUFICHA UKWELI kwa KUPOTOSHA. Rejea kauli ya Chagonja na baadye Nchimbi. Ukiunganisha kauli zao pamoja na za Nape, Shigella na Tendwa ni wazi Kamuhanda hata akisimama Mahakamani bado yatakuwa ni maigizo na mazingaombwe kwani nia ya serikali sio kupata ukweli wala kutenda haki ktk hili au ktk mojawapo ya mfululizo wa mauaji nchini.

  Itakuwa kama kumlazimisha punda kunywa maji....
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,731
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Nasikia hii ni nchi ya tume. Wengine hii ni police-state. Kwa ufupi suala la utawala bora ni kiini macho. Haki haitendeki wala kuonekana ikitendeka ndio maana Nchimbi, Mwema na Kamuhanda bado wako ktk ofisi za umma mpaka dakika hii.
   
 8. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Labda atapona tu, kama atamtaja aliyemtuma. Nafikiri hili suala linahitaji aliyewatuma, kuzuia maandamanano na mikutano ya CDM tu, Mafiesta na mikutano ya CCM vikaendelea. Kuna kirusi kimeingiza mkenge hawa Mapolisi wa juu. Hivi kwali kamati nzima ya ulinzi na usalama inaweza kuingia chaka namna hii? Basi hii nchi inakuenda ni hatari.
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Labda atapona tu, kama atamtaja aliyemtuma. Nafikiri hili suala linahitaji aliyewatuma, kuzuia maandamanano na mikutano ya CDM tu, Mafiesta na mikutano ya CCM vikaendelea. Kuna kirusi kimeingiza mkenge hawa Mapolisi wa juu. Hivi kweli kamati nzima ya ulinzi na usalama inaweza kuingia chaka namna hii? Basi hii nchi inakuenda ni hatari.
   
 10. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Ni kupwaya kwa katiba mzee sio Feleshi, Manumba wala IGP Mwema, tukiweza kuwa na katiba mzuri
  (ambayo ni ndoto kwa watanzania) hutakaa uone uozo huu
   
 11. U

  Udaa JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 727
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mda utafika tu,majambazi yote ya haki zetu chini serikari dhaifu tutayasurubu.NA TUNAUSONGO NAYO SANA.
   
 12. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  i heard the same story ndugu yangu,anataka astaafu kwa amani na mafao yake yote ndio maana anatumika ata pale pasipostahili kutumika hivyo.
   
 13. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,937
  Likes Received: 37,425
  Trophy Points: 280
  Mkuu tatizo kubwa la nchii kwa sasa ni kuwa na raisi ambaye si muwajibikaji.Ni kiongozi asiyejali kabisa na ndio maana hachukui hatua kwa walio chini yake.Raisi kama angeguswa angemuagiza IGP amsimamishe kazi huyo RPC.Hata hivyo, huyu IGP nae alitakiwa asimamishwe kazi na raisi.

  Watanzania kuanzia wabunge,waandishi wa habari,wanaharakati na makundi mengi tumekuwa na tabia ya kila siku kulaumu mawaziri,makatibu wakuu na viongozi wengine ila tumekuwa waoga wa kumnyooshea kidole raisi ambae ndio analea uzembe huu.Kila siku tunalia na madaraka makubwa ya raisi lakini hebu tujiulize anayatumia vipi kuwaadhibu walio chini yake.

  Tangu awamu ya nne ianze ni viongozi wangapi wamejiuzulu kuanzia waziri mkuu na mawaziri tena wote ni kwa shinikizo la wananchi na wala si kwa raisi yeye kama yeye kuchukua hatu kwa utashi wake ama kuguswa na madhambi ya walio chini yake.Nasema sasa kilichobaki ni raisi naye aondoke kwani ameshindwa kutimiza wajibu wake na hasa kuhusu kufanya maamuzi magumu na matokeo yake kila kukicha watanzania tumekuwa watu wa kulalama tu na hakuna cha maana kinachofanyika.
   
 14. k

  kwitega Senior Member

  #14
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Mwanakijiji, ulichokisema ndicho tunatamani sana kifanyike. Lakini kwa uoza uliopo katika nchi yetu; siamini kama hilo linaweza kufanyika. Kitendo cha Kamuhanda kuwepo kwenye tukio na kuacha yaliyotokea yatokee, kisha akaondoka pale ni kama yeye ndiye alikuwa ametoa amri ya kuuawa kwa Mwangosi na akawa pale anasimamia zoezi zima ili kuhakikisha kuwa linakamilika. Kitendo hicho ni cha kujiamini kupita kiasi. Je, kujiamini huko kunatokana na nafasi yake kama RPC, kwamba ameshazoea kuua na hakuna mtu wa kumgusa au alikuwa anatekeleza amri ya nani?. Hivyo, Kamuhanda mwenyewe anajua chanzo cha ujasiri huo wa kijinga. Kingine ni kwamba kuna madai kuwa, ndani ya Jeshi la Polisi kuna mambo mengi tu ya hovyo hovyo yanayowahusisha wakubwa wa Jeshi hilo na Ma RPC. Hivyo ni ngumu sana Kamuhanda kutoswa na kufikishwa Mahakamani.
   
 15. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ingawa waislam wana matatizo yao flan flan,me nawakubali tu kwenye suala zima la misimamo,ili kuwawajibisha hawa viongozi inahitajika roho kama ya waislam na kuna siku itafika tu.
   
 16. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  .. Ndio maana mi nikasema waliomuua mwangosi watashinda kesi wakipelekwa mahakaman kwa kuwa serikali haina nia ya dhati ya kuwawajibisha waliotenda kosa hilo. Wangekuwa na nia, wangeanza na Kamhanda mara moja-angalau hata kwa kumsimamisha kazi, la sivyo hii kesi imeisha kabla haijaanza!
   
 17. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Kamhanda na Chagonja niwaovu mithili ya SHETANI. hasa hili Paul Chagonja. kwanza tayari lilikuwa limeshaanza kupindisha mambo kwa kusema eti mlipuko ulisababishwa na kitu kilichorushwa kutoka mbali, PICHA TU NDO ZIMETUSAIDIA KULIFUNGA DOMO HILI LI-AFANDE MNYWA DAMU ZA WATU. Sioni tofauti ya Chagonja na Hitler, kwenye baadhi ya kauli za Chagonja unaweza usiamini kama huyu jamaa huwa hata ana chembe ya huruma, HE IS COMPLETELY AN ANIMAL. SIJUI KAMA KWENYE MISIBA HILI JAMAA HUWA HATA MACHOZI YANAMLENGALENGA, HE IS SO MEAN. HILI JAMAA LINAWEZA KUMCHINJA HATA MAMA YAKE MZAZI AKIENDA KINYUME NA MATAKWA YAKE.
   
 18. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,731
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Huo ndio ukweli mchungu.
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,731
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Lazima tukatae kuwa na mamluki na wababishaji kama Chagonja, Nchimbi, Kamuhanda, Tendwa nk.

  Ni kwa kuwa na katiba imara, sera madhubuti na viongozi makini ndipo hii nchi itabadilika. JK hana nia hata kidogo ya kuitendea nchi jema lolote kwa sasa, mark my words! Dear friends.
   
 20. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #20
  Sep 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,731
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Lazima tukatae kuwa na mamluki na wababaishaji kama Chagonja, Nchimbi, Kamuhanda, Tendwa nk.

  Itawezekana iwapo tutakuwa na katiba imara, sera madhubuti na viongozi makini. Hii inaita mabadiliko hivyo lazima tuitendee haki kwa kuwezesha mabadiliko chanya kutokea ikiwezekan yatokee kwa amani na utulivu.

  Kwa sasa ni wazi JK hana nia wala uatashi hata kidogo wa kuitendea nchi hii jema lolote hata atakapoondoka. We gonna pay in full after his miserable reign ends! It's another sad fact to live with.
   
Loading...