Ni laana kumkataa mtu, na Ni dhambi kubwa!

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,520
Kwanza nianze kwa kusema,hakuna jambo lenye kuumiza maishani kama kukataliwa ,kwa mwanadamu yeyote hujihisi na mapungufu tele iwe mwanaume /mwanamke ,hili jambo ni jambo lenye kuumiza sana ,

Naomba nieleweke hapa vizuri nachozungumzia hapa ni kule kukataliwa kiuchumba ,yaani umepeleka barua sehemu ukapigwa kidochiii au binti ana ahidiwa kuolewa mwisho wasiku jamaa ana ghairi..

jambo hili huwa linapoteza kujiamini kwa muhusika na kujiona mwenye kasoro maishani.ila pia upande wapili yule alolitenda kwa kumtendea mwenzio ubaya huu huishia kwenye laana kubwa .

Nitatoa mfano uliokuwa hai..
Nina Odo wangu mmoja enzi zake alikataa wachumba takriban wapatao kumi ,kwa kujiona bado anadai ,ila mpaka napoandika waraka huu Odo huyu amechena anatafuta hata wa kumchukuwa bure hapati..

maana alikataa watu wote kwa matajario ataolewa na jamaa flani hivi mwenye maisha yake mazuri ,matokeo yake yule bwana ,familia ilimtaftia mke na bwana akaowa ..

Mwisho wa siku Odo wangu akabaki hana pakushika..

Usia wangu huwezi kupata furaha kama kuna watu unawakosesha furaha lazima utalaanika tu na mwisho wa siku usipate unachokitaka.
 
Mbona kama unanisema mkuu INA mana mtu hana hali ya kuchagua ampendaye?
hapana mkuu sijakusema ila nakupa maneno ya akiba wengi walichagua sana mwisho wasiku juwa likawachwea

Nina mifano mingi hapa wapo wengi wamechezea bahati kwa kutegemea nina fulani ninayempenda na ndio nataka anaiowe mwisho wa siku asiolewe na huyo jamaa
 
Mi naonaga kama haya mahusiano hayana formula... 7bu unaeza sema usichague ukampta ukampeleka kwenu wakaongea.. Haya ukchagua pia wataongea! Ila vyote ni mipango ya Allah!
 
Vigezo ambavyo si vya juu sana ni muhimu kufikiwa. Sasa kama vigezo hivyo rahisi kufikiwa havifikiwi inakuwa ngumu mwa mhusika kukubali harusi. Kwa mfano anasema mie nataka anayejua kukwea/kupanda mnazi halafu anakuja mwenye sifa ya kupanda na kuvuna mpunga lakini hajui kupanda mnazi hapo inakuwa ngumu sana kukubaliwa.

Kwanza nianze kwa kusema,hakuna jambo lenye kuumiza maishani kama kukataliwa ,kwa mwanadamu yeyote hujihisi na mapungufu tele iwe mwanaume /mwanamke ,hili jambo ni jambo lenye kuumiza sana ,

Naomba nieleweke hapa vizuri nachozungumzia hapa ni kule kukataliwa kiuchumba ,yaani umepeleka barua sehemu ukapigwa kidochiii au binti ana ahidiwa kuolewa mwisho wasiku jamaa ana ghairi..

jambo hili huwa linapoteza kujiamini kwa muhusika na kujiona mwenye kasoro maishani.ila pia upande wapili yule alolitenda kwa kumtendea mwenzio ubaya huu huishia kwenye laana kubwa .

Nitatoa mfano uliokuwa hai..
Nina Odo wangu mmoja enzi zake alikataa wachumba takriban wapatao kumi ,kwa kujiona bado anadai ,ila mpaka napoandika waraka huu Odo huyu amechena anatafuta hata wa kumchukuwa bure hapati..

maana alikataa watu wote kwa matajario ataolewa na jamaa flani hivi mwenye maisha yake mazuri ,matokeo yake yule bwana ,familia ilimtaftia mke na bwana akaowa ..

Mwisho wa siku Odo wangu akabaki hana pakushika..

Usia wangu huwezi kupata furaha kama kuna watu unawakosesha furaha lazima utalaanika tu na mwisho wa siku usipate unachokitaka.
 
kwa maisha ya sasa.. mtu mpaka unapeleka barua.. bado hujaelewana tu na mwenzio mpaka ukataliwe... na nyie mabinti mnaokataa wachumba (japo kuna muda huwa ni sawa kutokana na kutofanana kitabia mf pombe) jitahidini kupunguza maringo... nimemaliza!
Mkuu tatizo lao huwa wanachaguwa sana mimi nimeshuhudia wengi wanapoteza bahati..

utakuta bint labda ana kajamaa kake hakana mbele wala nyuma ..wanakuja watu wako serias kutaka kumchumbia anawapiga cha mbavu ,matokeo yake uyo kijana aliyetegemea kuolea nae mwisho wa siku jamaa anapotea
 
Sijawahi kukaa na Odo wangu then tukapiga stori za namna hiyo, Mkuu umebarikiwa sana
Hahaha asante inategemea ,mkuu mimi Odo wangu kama Rafiki yangu so kuna wakat huwa anafunguka na kunieleza kuwa alibugiii ..

maana wakati akitaka kunijenga kwenye mahusiano huwa anatumia mifano mingi iliyomtokea .
 
"Mungu huwa haleti mara mbili"
Nilishuhudia mdada kakataa posa za watu kadhaa wenye kazi zao safi,

Heeee eeee ebabaaaaaaa,

Akaja jamaa mmoja mtoto wa mfugaji pale town katoa posa akakubaliwaa,

Akaolewa , wakarudi kwao jamaa kijijini kuishi pamoja,
Baada ya mwaka mmoja sikuamini macho yangu yaani lile futa lote sio futa tena ni ufuta,
So sad kwakwel ,

Mi naonaga kama haya mahusiano hayana formula... 7bu unaeza sema usichague ukampta ukampeleka kwenu wakaongea.. Haya ukchagua pia wataongea! Ila vyote ni mipango ya Allah!
Ni kweli unachosema ili nilichogundua

Hakuna ajuwa hatma yake ,pili usimtegemee mwanadamu kwa asilimia zote .

pia inapotokea nafasi ni vyema ukaichukuwa hiyo nafasi maana huwezi juwa kesho itakuweje?
 
Vigezo ambavyo si vya juu sana ni muhimu kufikiwa. Sasa kama vigezo hivyo rahisi kufikiwa havifikiwi inakuwa ngumu mwa mhusika kukubali harusi. Kwa mfano anasema mie nataka anayejua kukwea/kupanda mnazi halafu anakuja mwenye sifa ya kupanda na kuvuna mpunga lakini hajui kupanda mnazi hapo inakuwa ngumu sana kukubaliwa.
ni kweli mkuu ,ila nachojua mimi huwezi kupewa vyote kwenye maisha ..
yaani nachomaanisha ni ngumu kumpata unayemtaka kwa asilimia zote ..
wakat mwingine huwa inabidi kubeba kilichopo tu
 
Back
Top Bottom