Ni kweli Zitto Kabwe anatembea maneno yake na kutenda anayonena?

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
594
1,827
Mwaka 2010 chama chake cha zamani waliweka katika Ilani yao ya Uchaguzi kupinga posho ya kukaa Bungeni kama hatua ya kubana matumizi ya Serikali. Wakakubaliana kuwa wabunge wa chama chao (CHADEMA) hawatapokea posho ya kukaa (sitting allowance).

Hata hivyo, ilipokuja katika utekelezaji wenzake wote wa CHADEMA wakagwaya na Ndugu Zitto Kabwe ni mbunge pekee aliyepinga posho za vikao na kuzikataa kata kata kwa miaka mitano (5) mfululizo, ambazo ni takribani shilingi milioni 21 kila mwaka.

Katika kipindi hicho cha miaka mitano Zitto alikataa kuchukua jumla ya Shilingi Milioni Mia Moja na Tano (105,000,000)!!

Kukataa pesa yote hii kwa sababu ya ‘principle’ tu ni jambo nadra sana kutokea katika mazingira yetu.

Hakika Zitto anatembea maneno yake. Zitto anatenda anayonena. Sasa kwa yote hata kwa nini wasimchukie wenye roho zao za kwa nini?

Zitto kabwe kwasasa ndio Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo baada ya kufurumushwa CHADEMA.
Tunachoomba Watanzania tumhukumu Zitto kwa rekodi zake na si kwa propaganda za mahasimu wake.

KITENDO CHA ZITTO KABWE KUKATAA POSHO ZA KUKAA BUNGENI NI TENDO LITALOBAKIA KWENYE HISTORIA YA NCHI HII.


zitto-pic-data.jpg
 
Back
Top Bottom