Ni kweli "Yeyote" anaweza kuwa "Mhalifu"

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
YEYOTE ANAWEZA KUWA MHALIFU.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Nimemsikiliza Kamanda Siro Kwa umakini mkubwa, nikaona nami nitoe machache haya Kwa ajili ya kujifunza Kwa wapenda kujifunza, andiko hili halitamlenga yeyote, isipokuwa ni andiko linaloweza kumlenga yeyote aliye mwanadamu, iwe Mimi mwenyewe, wewe usomaye au hata Yule ambaye hatasoma hapa.

Uhalifu ni uhalifu tuu! Hii inaweza kusomeka pia; Mhalifu ni Mhalifu tuu!
Pengine ingenifaa nifafanue maana ya Uhalifu Kwa kifupi;
"Uhalifu ni utendaji wa jambo lolote lililokatazwa kutendwa Kisheria au kwa sheria ndogondogo(By Laws) za Mtaa,Kijiji,Kitongoji,Kata/Shehia au Halmashauri." (Owago Steven, 2013)

Hivyo Uhalifu ni kwenda kinyume na sheria zilizowekwa,
Kiimani Uhalifu huitwa Dhambi(Uasi) yaani kwenenda kinyume na amri za kimungu.
Uhalifu Kwa lugha ya kawaida ni kufanya makosa, hata hivyo sio kila kosa ni Uhalifu.

Kila mwanadamu huweza kufanya makosa/Uhalifu Kwa sababu kadha wa kadha.
Sababu zinazopelekea Binadamu afanye makosa au Uhalifu zinaweza kuwa Kama ifuatavyo;

1. Maslahi
Kwa sehemu kubwa Uhalifu mwingi husababishwa na maslahi binafsi au kikundi cha watu.
Binadamu wengi hujikuta wakivunja sheria aidha Kwa makusudi au Kwa bahati mbaya kwa sababu ya maslahi yao binafsi ya kikundi cha watu.

Kwenye maslahi pia tamaa unaingia humo.

2. Kulaghaiwa
Baadhi ya watu huingia kwenye Uhalifu Kwa kushawishiwa. Sababu za kulaghaiwa ziko kuu mbili. Mosi, Tamaa na pili, Ujinga yaani kutokujua.

3. Kutotendeka Kwa HAKI.
Sababu kuu ya tatu ya binadamu kufanya Uhalifu ni kutotendeka Kwa haki. Kutokana na Ongezeko la udhalimu, dhulma, Rushwa, na ukosefu wa uadilifu. Baadhi ya watu hufanya Uhalifu kutokana na kutotendeka Kwa haki.
Hali hii husababisha athari Kama vile
I) watu kulichukulia sheria mkononi.
ii) Kulipana visasi pasipo kujali sheria.

Hii hutokana na kundi moja kujiona halitendewi haki. Kuona kuwa mmoja anapendelewa wakati mwingine anakandamizwa.
Hii ilijitokeza pia Kwa KAINI na nduguye Habili. Ambapo KAINI aliona mwenzake anapendelewa na Mungu zaidi.
Pia Yakobo na Essau ambapo Yakobo anamdhulumu kakaake baraka, Hali inayomfanya Essau atake kumuua Yakobo, lakini hakuweza Kwa Sababu Yakobo alikimbia.

Yeyote anaweza kutenda Uhalifu.

Iwe ni Mimi Taikon, iwe ni Mchungaji au Sheikhe,
Iwe ni Mwanajeshi au Polisi, Mwanasiasa au Jaji, mtu yeyote anaweza kuwa Mhalifu Kwa sababu Sisi wote ni wanadamu.

Sababu za kuwa wahalifu nishazieleza hapo,

Kitu pekee ambacho niliweza kujifunza kwenye maisha yangu ni kuwa yeyote anaweza kukosea, na ikiwa ni hivyo basi niliweza kujifunza kuwa nisimuamini yeyote Yule isipokuwa Mungu pekeake.

Mimi ni muumini wa Haki, lakini haimaanishi kuwa Asilimia 100 Mimi ni mtenda haki, isipokuwa najitahidi Sana kuwa mwenye haki.
Mimi ni muumini wa Ukweli pasipo unafiki, lakini haimaanishi mara zote nasema ukweli, ingawaje napambania Hali hiyo.

Haki itendeke, na mtu mpenda haki haogopi haki inapotendeka. Jambo moja watu wasilolijua ni kuwa Haki ni ngumu Sana pale inapotekelezwa Kwa 100%.
Kibinadamu hasa Kwa Karne hii, kutenda haki 100% ni kuifanya dunia isimame, dunia iishe na maisha yakome.

Haki 100% Duniani ni kuiua Dunia. Kama ilivyo Uhalifu 100%. Hatuwezi kuishi ikiwa kiwango cha Uhalifu kitakuwa 100%.
Hata hivyo hatuwezi kuufanya Uhalifu uwe 0% kwani maisha hayawezekaniki.

Haki inatabia ya kujitetea ikiwa hakuna wa kuitetea. Haki IPO radhi ishirikiane na Uhalifu ili ijitetee Kama ilivyo Kwa Uhalifu.
Halikadhalika, Uhalifu nao unatabia ya kujitetea asipokuwepo wa kuutetea, upo radhi ushirikiane na Haki ili uendelee kuwapo. Hivyo ndivyo Dunia ilivyo.

Kushtakiwa Kwa Mbowe na wengineo ni matokeo ya Haki au Uhalifu kujipigania.
Mtu anaweza ingizwa jela Kwa haki yake, halikadhalika mtu huweza ingizwa jela Kwa Uhalifu wake.

Haki humnoa Mhalifu. Na Uhalifu humnoa Mwenye haki.

Taifa linalotenda haki huinuka, lakini isiwe haki iliyopitiliza, Kwa sababu haki ikipitiliza huumiza haki za wahalifu.
Msingi wa haki, huenda ukapiganiwa na wahalifu zaidi kuliko wenye haki.
Wahalifu hufahamu umuhimu wa haki kwani bila haki wasingeweza kuwapo.

Kimaandiko, Shetani alidai Haki zake, ambazo aliona ni stahiki zake. Msingi Mkuu wa Shetani ulikuwa Uhuru uliopitiliza, hiyo kwake ilikuwa ni haki kwake kuipata. Hakujali gharama alichojali ni matokeo ambayo kimsingi aligewa.

Haki huweza kuwa dhana, kwa upande mmoja inaweza ikawa haki wakati upande wa pili ikawa si haki. Halikadhalika na Uhalifu.

Mtu anaweza akatangaza haki lakini akawa ni Mhalifu.
Lakini mtu hawezi kutangaza Uhalifu akawa mwenye haki.

Polisi na serikali wanaweza tumia Uhalifu kuilinda haki.
Pia Wananchi wanaweza kuutumia Uhalifu kudai haki zao.
Au pengine kutumia neno haki kutenda Uhalifu wao.

Kiasili, wanaotangaza na kusema maneno ya Haki ndio huwa wahalifu.
Huitumia haki Kama chambo kuchota/kulaghai watu wapendao mambo mazuri ambayo ni matokeo ya Haki.

Serikali huahidi Haki iendelee kuwepo madarakani, lakini huweza kutumia Uhalifu kulinda haki ya kuendelea kuwapo madarakani huku ikiwaumiza wananchi.

Upinzani huweza kutumia haki Kama chambo kuyataka Madaraka, na ikishindikana kutumia Uhalifu kuyateka Kwa nguvu.

Haki ikikutana na Uhalifu huweza kupigana.
Na Kama zikiungana basi hakuna usalama.

Niishie hapa...

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Chalinze,
 
Back
Top Bottom