Ni kweli Wizara ya Fedha ilitoa rushwa kwa Kamati ya Zitto Kabwe?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Nikiwa kama mmoja wa wananchi wanaofuatilia siasa za Tanzania, nilikuwa na kiu ya kufahamu hatima ya sakata la Tegeta Escrow Account kutokana na kelele zilizokuwa hasa zinapigwa na wanasiasa wetu huku mataifa ya Magharibi yakionekana kulishikia bango kupitia Development Partners Group mpaka kupelekea kusitisha mchango wao wanaouita Budget Support .

Nilisikitika sana baada ya kusomwa kwa repoti ya PAC ndani ya bunge siyo kwa sababu sikupata kile nilichokuwa ninakifikiria bali ni kutokana na mapungufu yaliyojitokeza ndani ya repoti huku yakichagizwa na hoja kinzani ndani yake. Repoti haikuwa fair and balanced.

Kwa upana, Repoti ya CAG na hoja za PAC ziligusa Wizara tatu ambazo ni Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Nishati na Madini lakini cha kushangaza, mapendekezo ya PAC kuhusu uwajibikaji yakawa yamejikita katika Wizara ya Nishati na Madini.

Hata pale baadhi ya wabunge walipohoji kuhusu wajibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusiana na kampuni iliyotajwa ambayo imesajiliwa na BRELA wakati inaonyesha katika ripoti kuwa wahusika walioisajili hawakuweka majina yao, bali waliweka saini tu. Kamati ya PAC ilionekana kuitetea Wizara hiyo huku wakitumia hoja za nguvu kuwa hiyo ni kazi ya Wizara ya Nishati na Madini kulitambua hilo suala.

PAC waliendelea vile vile kuitetea Wizara ya Fedha kuhusiana na ukiukwaji wa malipo ya kodi ya ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa stempu (stamp duty) katika mlengo wa kuutupa uchafu huo kwenye shimo la uozo la Wizara ya Nishati na Madini.

Hoja kama hizi zilinifanya nipate maswali mengi na katika kutafuta majibu nilikumbuka baadhi ya maneno ya wanasiasa mbali mbali.

Russia President Vladimir Putin once said, Those who fight corruption should be clean themselves.

Former President Olusegun Obasanjo echoed the thoughts of many by saying fighting corruption is not a one-night affair.

Former President of the World Bank, Paul Wolfowitz summed up by saying, ''Sometimes corruption is slowed by shedding light into what was previously shadowed''.

Katika kuyatafuta majibu nikajikuta nagongana na picha hii ambayo inaonyesha Naibu Waziri wa Fedha akionekana kuwa ndani ya Kamati ya PAC katika maongezi ya kirafiki (jokes) and relaxed wakati pia Wizara yake ilikuwa ni mtuhumiwa mkuu.
Baadaye tukasikia Mhe. Mwigulu Nchemba akiwapongeza Mhe. Zitto na Luhaga Mpina, mbunge wa Kisesa wilayani Magu.
Wataalam wa masuala ya rushwa wanasema, moja ya corruption indicators is conflict of interest.

Katika kusimamia maadili ya kazi, baadhi ya wajumbe wa PAC hawakutakiwa wawe ndani ya kamati katika kutafuta majibu ya suala la Tegeta Escrow Account kwa sababu ya mwingiliano wa maslahi.

Mmoja wa wajumbe hao ni Mhe. Zitto Kabwe kwa sababu alikuwa ana uhasama binafsi na Viongozi wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Tumeona marumbano yake na Viongozi Wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini katika account yake ya Facebook, Twitter na pia kwenye blog yake hata kabla ya CAG kuwasilisha repoti yake ndani ya bunge. Mhe. Zitto alikuwa tayari ametoa hukumu wakati hata faili la uchunguzi halijaletwa kwake.

Mwingine ambaye hakupaswa kuwepo kwenye PAC ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Mhe. Luhaga Joelson Mpina kwa sababu Kamati yake inajihusisha kwa ukaribu na Mawaziri wa Wizara ya Fedha na pia Wizara ya Viwanda na Biashara.

Kama nilivyosema hapo juu, matokeo ya mwingiliano wa maslahi huzaa chemichemi ya rushwa kama ilivyofanywa na baadhi ya wajumbe wa PAC ambapo matokeo yake ni Abuse of discretion, Favoritism, nepotism and clientelism.

Abuse of Discretion refers to a failure to take into proper consideration the facts and law relating to a particular matter; an Arbitrary or unreasonable departure from precedent and settled judicial custom.

Favoritism is defined as the act of giving preferential treatment to someone or something.

Kila mwenye uelewa wa suala la Tegeta Escrow account atafahamu kuwa moja ya taasisi ambayo ilikuwa inatakiwa kuwa indicted kwenye majumuisho ya PAC ni Wizara ya Fedha ambayo kimsingi ilitakiwa iwe pia main focus katika sakata la IPTL. Cha kushangaza, Kamati ya PAC haikutoa mapendekezo kuhusu wakuu wa Wizara hiyo.

Kama hiyo haikutosha, Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo imesajiri kampuni bila kuweka majina pia haikuguswa katika mapendekezo ya PAC.

Hata Jaji Warioba baada ya kuisoma repoti ya PAC alishangaa sana na kuikosoa sana katika makala inayopatiakana
HAPA au HAPA

Kama mazingira hayo hayakuwa ni rushwa zilizozaa Abuse of discretion, Favoritism, nepotism and clientelism, itakuwa ni nini?

Kama repoti ya PAC haikuwa political witch-hunt, itakuwa ni nini?

TUSEMEZANE BILA JAZBA WALA KEJELI AU MATUSI ILI KUJENGA TAIFA LETU SOTE.
 

Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
9,604
2,000
hatuko hapa kutetea vibaka na majambawazi ccm
Hebu shirikisha ubongo wako na mwili wako, una jump in to conclussion wakati hujasoma hata hoja yenyewe! bavichwa bana, upeo wenu wa uchambuzi ni hewa kabisa yaani Mbowe atakachosapoti na nyie mnafuata bila hata utashi wa akili zenu.
 

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,876
2,000
Mkuu tangu zaman wadau walisema zitto si mtu wa kuaminika
Anang'ata na kupuliza,wanasiasa wenzake wanaenda mbali na kusema ZITTO siyo mtu wa kufanya naye business. Anapenda vyote kwa wakati mmoja, umaarufu na utajiri
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Sasa ripoti ya ESCROW kaiharibu kwa kumuacha waziri wa fedha, viwanda na biashara, je hajahongwa kweli maana kama pesa za mwiiigulllu anachukua itawakuwa za mama fedhaaaaa
 

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Msaliti hawezi acha kula usaliti wake
Mkuu,
Msaliti ni nani?

Hata hivyo, huwa sipendi kulitumia neno USALITI kwa sababu ni neno la laana hata kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu(Kwa wanaoamini kuna Mungu).

Sitaki kumhukumu binadamu kama mimi ili sijiwe hukumiwa!
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,795
2,000

Nilisikitika sana baada ya kusomwa kwa repoti ya PAC ndani ya bunge siyo kwa sababu sikupata kile nilichokuwa ninakifikiria bali ni kutokana na mapungufu yaliyojitokeza ndani ya repoti huku yakichagizwa na hoja kinzani ndani yake. Repoti haikuwa fair and balanced.
Mkuu Ng'wamapalala, asante kwa uchambuzi wa mapungufu, kama ilisikitikia mapungufu ya ripoti hiyo mara tuu baada ya kusomwa, ulipaswa kuyaweka mapungufu hayo humu jf mapema, ili angalau kuwasaidia wale baadhi ya wabunge wetu vilaza, angalau wangeweza ku rais concern kwenye majadiliano,

Japo mimi tangu mwanzo niliitetea BOT, lakini baada ya PAC nao kuiengua, nilitoa msimamo wangu hapa!, Sakata la Escrow: Did "BOT Had a Role to Play?, or Just An .

Pia nilizungumzia mapungufu mengine makubwa ya ripoti ya PAC hapa Escrow: Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!.Tuache

Na kuzungumzia mapungufu ya wabunge wetu hapa!.Pamoja Na Ufisadi Wake Wote, Chenge is One of Best Brains

Yote haya niliyasema mapema wakati waheshimiwa wabunge wetu bado wako Dodoma!.

Pasco
 

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Na maaskofu nao wameanza kusafishwa, sijui ni kwa maslahi ya nani?
Mkuu,
Hata mimi bado ninajiuliza sana.

Yaani wao wametoa hukumu halafu tena wanaanza kuitengua hukumu yao.

Nini kimewatokea hawa vijana wetu ambao baadhi yao wanajitangaza kutaka kupewa ofisi kuu ya nchi?
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Mkuu,
Msaliti ni nani?

Hata hivyo, huwa sipendi kulitumia neno USALITI kwa sababu ni neno la laana hata kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu(Kwa wanaoamini kuna Mungu).

Sitaki kumhukumu binadamu kama mimi ili sijiwe hukumiwa!
USIOGOPE MAANA hakika kuzuia CDM kukomboa watu na nchi ni usaliti mkubwa sana, ZZK.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom