Ni kweli: Wengi tumevumilia maneno ya "kukatisha tamaa" kutoka kwa Rais wetu wenyewe, mwendo tunaumaliza na imani kwa utanzania wetu tumeilinda

We Lingamba dini ina faida gani?
Tulia dawa ikuingie soma namba vizuri acha kuleta mambo ya dini kwenye siasa.
 
Huyu dini hana msameni bure. Ukitenda mabaya utalipwa mabaya, ukicheka Leo ujuwe kesho utalia. Ni misemo lakini hutimia. Utaliaje na kwa lipi,AJUA MUNGU

amesema ukweli na viongozi wa kiafrika wanatabilika, lazima utulie dawa ikuingie ukirusha miguu utaumia.
 
Kuna mswaada wa microfinance Unakuja, atakayesalimika amshukuru Mungu.
ni kweli kabisa, watu wameumia sana, nyumba zimevunjwa, familia zimelala nje, biashara zimefungwa, watu wametekwa na kuuawa, watu wamepigwa risasi mchana kweupe, watu wamefutiwa ajira tena wengine baada ya kutumikia kwa miaka mingi, vyombo vya habari vimezimwa kama mshumaa, wimbi la miswaada ya sheria kandamizi limepelekwa bungeni, nchi marafiki na wahisani wametuchoka n.k. yooote haya chanzo ni mtu mmoja mwenye kiburi na majivuno!
 
We Lingamba dini ina faida gani?
Tulia dawa ikuingie soma namba vizuri acha kuleta mambo ya dini kwenye siasa.
Mche mungu sir khan,hahaha unaikana dini kwa sababu ya njaa sir!!! Yawezekana ni malezi yamekufikisha hapo. Ila IPO siku utatiwa ufahamu nawe utafahamu unachokifahamu na kukiamini sicho
 
Yeah mgawanyo wa hayo maumivu nimeutizama kwa namna nyingi kwa mfano kuisoma namba ya Lisu, wazazi wa Ben Sanane, Alfonce Mawazo, haiwezi kulingana na kuisoma namba ya kina Yusuf Manj, Nape, Mbowe, Matiko na wengine.....
Naongezea na No alivyokamuliwa mapesa ndo akaachiwa.kipara mnyang'anyi sana
 
....Tena mkiandamana muwatangulize shangazi zenu!:(:(:( mimi nimewafundisha watoto wangu kusikiliza hotuba za Nyerere pekee ! Nashukuru somo lieleweka kwa 100%:cool:
 
Ilituchukua takribani miaka kadhaa iliyopita ambapo ndani ya siku chache tu kutoka Rais wetu ndugu John Pombe Magufuli achaguliwe kuwa Rais wa tano wa nchi yetu, tulishuhudia kuiona miaka mitano ya uongozi wake kama kubanikwa jikoni. Ama kwa hakika wote tuliguswa na aina ya uongozi wake ingawa wapo baadhi wasioelewa.

Mimi binafsi ni miongoni mwa walioathiriwa na utawala wa Rais Magufuli muda mfupi tu baada ya yeye kuingia ikulu. Mamlaka anazoziongoza kutokana na uoga uliokuwa umewajaa walipeleka machungu kwangu na kwa jamii inayonitegemea. Narudia tena, ilikuwa ni uoga tu na kuogopa kelele walizokuwa wakipigiwa.

Nashukuru nilisimama muda mfupi tu baada ya kuandamwa na mikosi ya hapa na pale. Ama kwa hakika wengi waliumizwa kutokana na mashindano waliyokuwa wakiyafanya wasaidizi wa Rais John Pombe Magufuli. Ilikuwa ni patashika kwelikweli.

Niweke wazi kuwa ninafahamiana na wengi. Wengi wameumizwa kwelikweli na mashindano haya ya wasaidizi wa Rais, pengine siyo kosa lao bali aina ya boss waliye naye. Ulikuwa ukimsikia Rais akimshambulia msaidizi wake hadharani kuwa haendani na kasi yake kwa kutokuwashughulikia watu! Kutokonyang'anya watu mali nako kulimkera Rais kwa wasaidizi hawa "wazembe"

Wengi tulivamiwa maofisini mwetu, asubuhi akija NEMC, mchana anakuja TRA na jioni unamuona waziri kaja. Wote hawa waliugombania mtaji dhaifu wa mtanzania mzawa ambapo iliwalazimu kufanya hivyo.

La kumshukuru Mungu ni kuwa mwendo tunaumaliza na imani ya utanzania wetu tumeilinda. Wapo walioumia sana, wapo tulioumia kidogo na wapo waliopotea. Kwa kila mmoja wetu lazima tumshukuru Mungu kwa kila jambo lililotokea. Kumekucha na giza linatokomea. Yote kwa yote tunafunzwa kuwa kina somalia, Zimbabwe, Congo, Burundi, Iraq, Afghanistan na wengine wengi wapo katika dunia hii hii na wanakuwa hivyo kutokana na mtu mmoja tu! Kila mmoja wetu anaweza kuwa wao! Naam huo ndiyo ujumbe tunaopaswa kuuelewa.

Andiko lina kilo za kutosha. Asomaye na aelewe.
 
Back
Top Bottom