Ni kweli Website ya Uhuru yachakachuliwa?

dally

Member
Nov 4, 2009
19
0
Wanajamvi nilikuwa napitia gazeti la CCM na nimeshengazwa na kukutana na kichwa cha habari kwamba tovuti yao imechakachuliwa na wahuni na waliofanikiwa kuendesha KURA YA MAONI ya URAIS wa JMT ambapo Dr. Slaa ameibuka mshindi.

Kwakweli hali si nzuri na jamaa wanajaribukujikosha ili kibarua chao kisiote nyasi. Naamini kabisa ni wao wenyewe ndio walioendesha hiyo poll na wakadhani wapenzi wa CCM watawapiga tafu ilikupata matokeo wanayoyataka wao. Kipigo walichopata ni kielelezo tosha kwamba watanzania wamechoka na ubabaishaji wa CCM na mwaka huu lazima kieleweke!!

Chanzo hapa chini:

Tovuti ya Uhuru yachakachuliwa
 
Wanaotembelea tovuti ya CCM sio wote ni wapenzi na wanachama wa CCM.
 
Kwa mtu mwenye akili fintu bado ataendelea kuamini kuwa wanaoshabikia ccm kweli wanaipenda.............watu hawaipendi ccm ila tatizo ni njaa tu na wanajionesha kimwili lkn
 
Hakuna kuchakachuliwa ile ni hali halisi kuna mtu ana uchungu na ufalme wa kina Kkiwete akaamua kuiweka pale na watu wakasema JK hafai!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom