Ni kweli watu walionywa kabla ya Mkutano na JK?

Tafiti,
None of the above...and this is serious. By the way, akijibu swali kuhusu "Hali ya kisiasa Zanzibar"...
"Kwa sasa niseme tu kwamba ile timu ya wataalam, ambamo marehemu Profesa Chachage alikuwa mmoja wao kufanyia kazi suala hilo mpaka mauti yalipomkuta pale Kibaha, imemaliza kazi yake na "sirikali" inapitia kwa makini ripoti yao ili hatimaye suala la Zanzibar/CCM na CUF lishughulikiwe kwa kasi mpya na ikiwezekana lifikie hatma yake kabla ya mwisho wa mwaka huu..."

Kimya kidogo baada ya umeme kukatika, na baada ya sekunde chache umeme wa jenereta ya dharura unachukua nafasi yake. JK, huku akitabasamu, "Marekani hamna mambo haya..."
Waandishi wote wanaangua kicheko wengine mpaka wanaanguka chini! Yeye anaendelea "Suala la kero za Muungano nalo linashughulikiwa. Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi na wasaidizi wao washakutana, na niseme kwamba tumepiga hatua kubwa. Asanteni kwa kunisikiliza."

Waandishi wanaenda kujichana mapochopocho!
 
Mheshimiwa tungependa kazi hiyo imalizike haraka...

Rais Kikwete athibitisha kupokea orodha ya vigogo wa mihadarati Dar

Na Jesse Kwayu
RAIS Jakaya Kikwete amethibitisha kupokea orodha ya vigogo wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini na kwamba taarifa hizo sasa zinafanyiwa kazi.Kauli hiyo aliitoa jana alipozungumza na wahariri wa vyuombo vya habari, Ikulu Dar es Salaam, ambako alikuwa ameitisha mkutano nao kwa ajili ya pamoja na mambo mengine, kuwahutubia wananchi. Alisema orodha hiyo ameikabidhi kwa vyombo husika ili waishughulikie.

“Kuhusu swali kama nimepokea waraka wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya, ndiyo nimeupokea,” alisema Rais akijibu moja ya swali aliloulizwa katika mkutano huo, uliorushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni ya Taifa (TvT)na Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD).

Alisisitiza kama alivyopambana na tatizo la ujambazi nchini, nalo la biashara ya dawa za kulevya ni moja ya vipaumbele na atahakikisha waletaji na wasambazaji wanashughulikiwa ili hatimaye watu waliokuwa wameathirika kwa utumiaji waweze kutibiwa.

Rais pia alithibitisha kwamba katika waraka huo unaoelezwa kuandikwa na watu waliojitoa katika shughuli ya kusambaza na kutumia dawa hizo, kuna taarifa muhimu ambazo zitasaidia sana tume ya kupambana na dawa za kulevya.

Gazeti hili Septemba 19, mwaka huu, kwa mara ya kwanza lilifichua habari za Rais kupelekewa waraka huo na wananchi waliokuwa wamejitokeza kumsaidia katika kupambana na biashara hiyo, ambayo imeleta madhara kwa vijana wengi nchini kugeuka ‘mateja’ na hivyo kupoteza nguvu kazi kubwa ya nchi.

Walioandika waraka huo ambao Mwananchi iliuona, ni wananchi 15 na waliweka saini zao mwisho wa waraka huo.Wananchi hao katika baraua hiyo yenye kurasa 10, wanadai kwamba walikuwa wakitumiwa na vigogo hao kufanya biashara hiyo, lakini sasa wameamua kuachana nayo. Barua hiyo iliandikwa Septemba 8, mwaka huu.

Kwa mujibu wa barua hiyo, majina 58 yameorodheshwa yakiwa katika makundi matatu makubwa, la kwanza likiwa ni waagizaji wakubwa wa dawa hizo; la pili ni wafadhili ambao majina yao hutumika kusafirisha dawa hizo; na la tatu ni wauzaji walioko Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.

Katika orodha hiyo, yamo majina ya wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa, wakuu wa taasisi nyeti, baadhi ya viongozi wa dini na maafisa wa juu serikalini.Kundi la kwanza lina majina 12, miongoni mwao ni wafanyabiashara maarufu katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Arusha na Bagamoyo na baadhi ya viongozi wa dini wa madhehebu fulani.

Kundi hili linadaiwa kuwa linaingiza dawa za kulevya kwa njia mbalimbali zikiwamo, kutumia mipira ya kondomu, majokofu, vifaa vya hospitali, meli na marobota ya mitumba.Katika kundi la pili kuna watu 19, miongoni mwao wamo wanasiasa wakubwa nchini wakiongoza kundi hili, wafanyakazi kutoka taasisi ya fedha nchini na wafanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam na Zanzibar.

Kundi la tatu lina majina 27, ambayo si ya watu wenye majina makubwa, lakini ndio wanaotumika kusambaza mitaani kwa watumiaji wa dawa za kulevya.Mbali ya kushiriki katika kusambaza dawa za kulevya, kundi hili pia lina baadhi ya majina ya watu waliotajwa kushiriki katika kuingiza silaha nzito zinazotumika kwa ajili ya ujambazi kutoka nchi jirani.

Ufukwe wa pwani ya Bahari ya Hindi eneo la Muhoro wilayani Rufiji, inaelezwa kuwa unatumika kuingizia silaha hizo kutoka nchi jirani pamoja na dawa za kulevya chini ya ufadhili wa mmoja wa wanasiasa nchini.

Uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere unatajwa kuwa unatumiwa na watu hawa kuingiza dawa hizo nchini kutokea nchi za nje, huku baadhi ya maafisa wa polisi watatu wakitajwa kuwa ndio wanaotoa ulinzi kwa watu wanaopitisha dawa hizo.

Nyumba ya afisa wa juu mstaafu katika idara nyeti iliyopo jijini Dar es Salaam, inatajwa kuwa inatumika katika kuhifadhi vijana wanaoingiza dawa za kulevya, huku nyumba ya mfanyabiashara mmoja iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikitajwa kuwa ndiyo inayotumika kama kituo cha kutolea pipi tumboni kwa vijana wanaoingiza dawa hizo kutoka nje ya nchi.

Mipaka ya Tunduma mkoani Mbeya, Horohoro mkoani Kilimanjaro na Namanga mkoani Arusha, nayo imetajwa kuwa inatumika kupitisha dawa za kulevya kwa kutumia mabasi na magari mengine. Kuna kampuni mbili za mabasi nchini zinazotajwa kuongoza kutumika katika usafirishaji.

Katika mkutano wake na wahariri jana, Rais alitoa angalizo kwamba taarifa zilizoko kwenye waraka huo zitafanyiwa kazi na uchambuzi, kwani inawezekana watu wengine wakaandikwa kwa kukomoana.
 
Nyumba za serikali maeneo maalum kuchukuliwa-JK

http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2006/10/03/75674.html

2006-10-03 09:48:57
Na Mwandishi wetu




Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Bi. Flora Wingia akimuuliza swali Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati Rais alipokutana na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari Ikulu Jijini Dar esSalaam jana

Rais Jakaya Kikwete amesema nyumba zote za serikali zilizouzwa kwenye maeneo maalumu, zitachukuliwa. Rais Kikwete, alisema hayo jana alipokutana na wahariri wa vyombo vya habari nchini ikiwa ni utaratibu wake aliojiwekea kila mwisho wa mwezi wa kulihutubia taifa kwa njia ya radio na televisheni.
"Hatukusudii kuzichukua nyumba zote, kuna maeneo tuna matatizo maalum", alifafanua.

Akitoa mfano alisema , ''OCD kauziwa nyumba eneo la kituo cha polisi, OCD yule akahama kutoka Mafia kwenda Mtwara au kastaafu, akaipangisha hapo kituoni.

"Tunaangalia maeneo yale ambayo lazima tuyafanyie marekebisho," alisema Rais Kikwete.

Kuhusu mikopo ya elimu ya juu kuwabagua yatima na wavulana wenye ulemavu ambao walipata daraja la pili lakini hawakupata mikopo hiyo.

Rais Kikwete alisema kwamba kama wapo waliosahauliwa, "hili la yatima na walemavu tutaliangalia."

Alipoulizwa kuhusu Muswada wa Sheria ya Uhuru wa Habari utawasilishwa lini bungeni ili usaidie sekta ya habari, rais Kikwete alisema kuwa upo tayari, kinachosubiriwa ni majadiliano na wadau wa sekta hiyo na kuahidi kuwa utawasilishwa katika kikao cha Bunge la mwezi Aprili, mwakani.

Hata hivyo, rais aliwataka waandishi wa habari kuwa wavumilivu wakati wanapotafuta habari na kupata vikwazo.

"Nimewaambia watu wangu kuwa vyombo vya habari vinatusaidia. Wengine ni waoga hasa pale yanapokosewa matamshi yao?wengine wanafikia hatua wanajibu "mwambie sipo" huku mwandishi mwenyewe anasikia majibu hayo," alisema rais Kikwete na kuwafanya wahariri wakiangua vicheko.

Hata hivyo, alisisitiza kwamba ataendelea kuwasisitizia watendaji wake umuhimu wa kuwa karibu na vyombo vya habari.

Aidha, wahariri hao walitaka kujua ni hatua gani zinachukuliwa kwa wabunge waliobainika kuwa na vyeti feki.

Rais Kikwete alijibu kuwa suala hilo limeshakabidhiwa kwa Spika wa Bunge ili lifikishwe kwenye Kamati za Maadili kwa uchambuzi. "Siyo mtu ana cheti cha kidato cha nne kumbe hata darasa la nne hajafika," alisema rais na kusababisha kicheko.

Kuhusu mikataba, wahariri walitaka kujua suala la mrahaba wa asilimia tatu unaotokana na sekta ya hiyo na rais alisema litaangaliwa upya ili kuanzia mwezi Desemba isiwepo mikataba inayotajirisha wachache.

Alisema kuanzia mwezi huo migodi itaanza kulipa asilimia 15 ya mrahaba. " Tusiwe na mikataba ya kunufaisha makampuni ya nje na sisi tukabaki kuwa maskini," alisisitiza.

Aidha, swali lingine lilikuwa kuhusu NGOs hasa zilizoanzishwa kwa ajili ya kushughulikia watu wenye matatizo ya Ukimwi, serikali inazidhibiti vipi kuhakikisha walengwa wanafikishiwa mahitaji.

Rais Kikwete alisema eneo hilo lina matatizo. "Baadhi ya wenzetu wanaunda NGO kama ajira. Baadhi ya wenzetu wanaanzisha NGO akiwa na dhamira yake, ataishi vipi."

Aliongeza "upo udhaifu. Bahati mbaya hatuna sheria ya kudhibiti NGOs. Lakini kama NGOs hizo zina-demand transparency (zinataka uwazi) kutoka serikalini kwa nini serikali nayo isi-demand transparency toka NGOs?"

Alisisitiza kuwa wanaoanzisha NGos wasukumwe na dhamira ndani ya mioyo yao, wasianzishe NGO kama ajira. "Wengine wanaganga njaa kupitia NGO."

Akizungumzia mgao wa umeme unavyoathiri uchumi wa nchi, rais Kikwete, mpaka sasa athari zake hazijawa kubwa sana.

Hata hivyo, alitahadharisha mgao huo usimkandamize mzalishaji. "Msimuue bata wa dhahabu anayetaga yai la dhahabu."

Akizungumzia mpasuko wa kisiasa Zanzibar, rais Kikwete, alisema tatizo hilo lazima lipatiwe ufumbuzi na kwamba kuna kazi kubwa ya mashaurino hata hivyo, alisema serikali imefikia mahali pazuri.

Kuhusu kushuka kwa shilingi ya Tanzania , rais alisema kwa maelezo ya Benki Kuu, kumekuwa na mahitaji makubwa ya fedha za kigeni hasa katika kipindi cha mwezi Machi, mwaka huu, kwa ajili ya kuagizia chakula toka nje ya nchi.

Tatizo lingine alisema, limesababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.
Hata hivyo, rais alisema, serikali itabidi iingilie kati kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.

Rais Kikwete aliwaahidi wahariri hao kuwa atakuwa na utaratibu wa kukutana nao kila baada ya miezi mitatu na kwamba mkutano mwingine utakuwa Desemba, mwaka huu.

SOURCE: Nipashe
 
Mbona mmepandisha na kubananisha mada bila ya sababu ? Kichwa habari hakiendani na mambo mengi ambayo mmeanza kuyaleta maana yake ni kitu gani ?
 
Nikiwa palepale kwenye mkutano wengine walishangalia na wengine walishangaa na kusema kwamba kumbe ndiyo maana tuliandikiwa mails za kuonyowa na kuambiwa you must behave mbele ya Rais kama utakuja kwenye mkutano wake .Je Es na wengine ambao kama mlipata mails hizo maana mimi sikuipata .Je watu walionywa in advance ku behave ? Ina maana kuacha maswali mazito na walipo kaidigi kijana akaitwa na shahidi ni ES baada ya mkutano na JK .Nisaidieni maana nilisikia wengi wakati wa vinywaji wanasema haya .
What is the big deal? Si ni sawa Baba yake akwambie unawe kabla ya kula? Kushika adabu ni vibaya siku hizi?
 
Back
Top Bottom