Ni kweli watanzania tuna chuki au wivu kwenye uwekezaji wa viongozi wetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli watanzania tuna chuki au wivu kwenye uwekezaji wa viongozi wetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zing, Jun 21, 2011.

 1. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi mjadala. tuchangie bila kuweka ushabiki wa vyama

  Kuna PM (FS) aliijaribu kuwkeza tanzania lakini matokeo yake mambo tuliyosoma kwenye vyombo vya habari yalikuwa ni ngetive zaidi kuwa anatumia cheo chake kuwapiga bao wananchi maskini.S ijui uhalali w autaratibu uliotumika lakini kwagu niliona ni jambo bora kwa mtu kama PM kuwekeza nchini mwake. Je kwa nini viongozi wetu wanapowekeza nchini wanapata negative public image? Nimetumia PM F. S kama mfano nadhani tuna mifano mingi japo mazingira na uhalali wa investment zao unatofautiana.

  • Je kuna tatizo la kiongozi wa ngazi ya juu kuwekeza au kucontest investment na watanzania wengine ?
  • Je wananchi tunacholaumu ni utaratibu au ni chuki tu?
  • Utaratibu gani utumike kiongozi anapotaka kuwkeza nchini?

  Vile vile tunasoma viongozi wengine labda wanadhani wannchi wana wivu wameamua kuwekeza nje ya nchi Kuna PM ( EL)tunasoma anawekza kwa kununua majumbo nje ya nchi kupitia mwanae. Naamin kwa viongozi wengi wa ngazi ya juu hii ndio njia safe zaidi kwao

  • Je kiasi gani chuki ya wanachi juu ya investment za vongozi ndani ya nchi inachangia wengi waangalie investment za nje?
  • Je na hao viongozi wanaowekeza nje japo ni uhuru wao wanajisikiaje mara investmet zao amabzo mara nyingini siri na hata hawajazisajili kwelie Tume ya maadili yaviongozi zinapongulika. Je wananchi hawana uhalalai wa kuwa na "chuki"

  Wewe kama great thinker ni kitu au ni uwekezaji gani bora kama ungekuwa ni kiongozi wa ngazi ya juu? ungewekeza na kushindana na watanzaia kumuliki ranch kama alaivyoafanya PM bila kificho au njia salama ya kufuta ni ni kuwekeza nje. Kwa nini

  Tujadili?

   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kuna kitu kinaitwa 'Maadili ya Viongozi' nina hakika hayajabadilishwa kuruhusu hilo unalotaja.
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kujadili kitu kama hiki kwangu mimi ni kama kupoteza muda.Kwanza wewe unaishi wapi,Mars kwa akina Nibiru.Kama unaishi Tanzania na una akili timamu utashindwaje kuona kwamba tatizo sio wivu isipokuwa tatizo ni kwamba hawa watawala wanaojifanya wanawekeza si wawekezaji ni wezi.Wanachojifanya wanawekeza is actually our money.Ingekuwa ni hela yao ya halali,kusingekuwa na maneno yeyote.Wake up bwana.
   
 4. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alichofanya Sumaye kimsingi ni kizuri na kilihitajika kidumishwe,lakini kwa unafiki na wivu wa viongozi waliofuata alionekana hafai,ipi bora,kuwekeza ndani nakulipia kodi nchini mwako au kuwekeza nje nakulipia kodi kwa maendeleo ya wengine
   
 5. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Gurta una maana gani nadhani hatukokwenye zile zama za ujamaa As long as wanaanya kitu fairly kwa mapato halali sioni kwamba kuna tatizo. na ndivyo navyojua hayo maadili yaavyosema. JE niko sahihi ? Au ni maadili gani hasa specific

  Nashukuru kwa kutumia valuable time yako kupoteza muda kweye hii thread. Ndo tunajifunza tukisoma michango ya great thinkers kama wewe. teh teh teh

  Sikuwa na nia mbaya najaribu kungalia mambo kwa urefu na mapana. Wewe ukiwa kiongozi siku moja unaweza kuwa katika postion hiyo . Kuhusu wizi inawezekana hasa kwa wale wanawekeza nje. Lakini mfano mtu kama F Sumaye aliyenunua au aliyetaka kunua ranch kule Kongwa ni mfano wa kuigwa. Inawezekana utaratibu ulimpa ushindi ndio mbovu lakini sbinafsi kwangu kiongozi kuwekeza ndani ni mfano w akuigwa na inaonyesha kuwa sio mwizi. Vya wizi hawawekezi humu.

  Kwangu binafsi mbunge wa jimbo la rukwa hana hata shamba la mfano la ekari japo kumi ni usanii. wakati wnanchi wa rukwa ni wakulima. Anawakilisha wapiga kura gani

  Pia mimi niko Tanzania
  Laini elewa kuna watu wako USA wako more infomred mambo ya Tanzania kuliko walio Dar Es Salaam. Dunia ya sasa ni global village. It depend on what u have is data or infomation and waht u can do with it na sio uko wapi  Yes mkuuu na mimi nadhani viongozi wanapohubiri kilimo kwanza inabidi tuwahoji ni wabunge wangapi wana mashamba ya mifano.
  Kwa kesi ya sumaye nadhani wazo lake lilikuwa zuri lakini sina uhakika na utaratibu. But in some cases imetokea wananchi kwa sbabau za kisiasa wanatumiwa kuwachukia viongoziwanapotaka kuwekeza. may be kwa sumaye inawezekana ilikuwa ni mtandao. am not sure
   
Loading...