Ni kweli Watanzania sio wawazi kwenye masuala nyeti au ya kufa au kupona?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli Watanzania sio wawazi kwenye masuala nyeti au ya kufa au kupona??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ambiente Guru, May 25, 2012.

 1. Ambiente Guru

  Ambiente Guru JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 2,276
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kumekuwepo na mjadala juu ya ukali wa matangazo yanayobandikwa au kutolewa na vyombo vya habari, kwamba yanakiuka maadili pale yanapotangazwaau kusikilizwa na watu wa rika tofauti au familia.

  Niwakumbushe, IPS/ Salama kondom walianza matangazo kwa kuwatumia watoto (wakionyesha alama ya dole kwa kondom). Kanisa la RC likapiga kelele matangazo yakaondolewa. Wimbo wa Dkt. Remi Ongala vaa soksi njia panda nao ulipigwa marufuku Redioni.

  Ikafikia Mfanyabiashara maarufu (M****) akaitwa na Maaskofu kuwa ni nabii wa kondom, sasa amekuwa/ wamekuwa mashujaa "Whisle blowers". Waliyofanya yalilenga kutoa tahadhari juu ya adhari za Ukimwi.

  Tutathnini kati ya madhara ya muda mfupi na yale ya muda mrefu wakati tunalinda maadili, mila na desturi.

  Campaigners believes that in order for a messege to have an impact it must be provocative. But the effect of provoking may be disastrous.

  Je jamii yetu bado sisi hatuna tabia ya uwazi "openness"?. You have to call a stone a stone and a spade a spade without mincing words where appropriate. Bora mchawi afe bali anayetahadharisha/onya watu (mwinkimbi) aishi.
  Nawasilisha
  Candid to my Country
  Richard Mazingira
   
Loading...