Ni kweli waswahili ni wavivu wa kufikiri ?

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,948
2,000
Jibu ni hapana.
ila hatutaki kufikiri kwa kuwa tayari hatujiamini.
nakumbuka mfano mmoja wa Mrisho Mpoto aliwahi sema kwamba kuna kizazi fulani kinasaidiwa kufikiri.
kwa mawazo yangu ni hiki kizazi cha instagram,whatsap,google,nakadhalika.
kizazi cha wavivu wa kutafakari,kuwaza na kufikiri.
leo unamkuta kijana mtanzania alozaliwa uswahilini yani eneo wazungumzao kiswahili.
kwa majaliwa ya mungu akabahatika kwenda shule kidogo tena kwa kuunga unga akiwa shule akajua maneno machache ya kingereza.
kijana kwa uvivu wa kufikiri,kuwaza na kutafakari akajifanya kujiaminisha uongo kuwa lugha ya kiswahili eti ni ndefu na kuliko atumie kiswahili ni bora achanganye na maneno aloyabahatisha katika kamusi ya kingereza.
huu ni uvivu wa kufikiri,kuwaza,kutafakari na kujifunza.
uvivu ambao wote tunao,lakini kwanini tubaki hapo bila ya kutoka ?
sababu sisi ni wavivu,wa kufikiri,kutafakari na kujifunza.
hatujiamini,hatujui kama hatujui na pia hatujui kama tunaweza,hatupendi kuamini katika yale ambayo ni asili yetu.
 

Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
1,736
2,000
Sasa mboma unauliza halafu unajijibu mwenyewe..?? Hapo tu umeshaonesha wewe ni mvivu wa kufikiri, kwa sababu umeshindwa kufikiria "kwann nawauliza watu halafu nawapa jibu..??"

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom