Ni kweli wanafunzi wasio na ada au fedha zinahitajika wakienda shuleni hawarudishwi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli wanafunzi wasio na ada au fedha zinahitajika wakienda shuleni hawarudishwi?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Magobe T, Jan 26, 2012.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Ndugu wanaJF, nimekuwa nikisikia kauli za viongozi mbalimbali wa serikali wakidai kila mtoto aliyechaguliwa kwenda sekondari lazima aende "hata kama hana nguo, viatu au ada." Nijuavyo, mbali na ada kuna fedha nyingine, ambazo inabidi mtoto aende nazo anapoenda kuanza Form I (zinakaribia/fika laki moja). Halafu kauli hizi za viongozi wanazitamka tu kwa kutumia vyombo vya habari na hawawaandikii wakuu wa shule kuwa mtoto atakayekuwa hana ada au uniform aruhusiwe kusoma na asirudishwe nyumbani.

  Lakini kuna mzazi mmoja alikuwa ananiambia kuwa mtoto wake amekosa 30,000/- kufikisha kiasi chote anachotakiwa kwenda nacho shuleni lakini walimu wamesema mpaka aende na kiasi chote kinachotakiwa ndipo atakaporuhisiwa kuandikishwa Form I (hizi shule za Kata). Je, hawa viongozi wanaotumia vyombo vya habari kuwadanganya Watanzania kuwa hakuna mtoto atayerudishwa nyumbani kwa kukosa ada au uniform wana nia gani? Hivi serikali yetu imefikia hapo kuwadanyanya wananchi kama kwamba hawana akili?
   
Loading...