Ni kweli Wahehe hula Mbwa??

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Kwa miaka mingi kumekuwa na dhana ya Wahehe kula mbwa,wapo waliogoma kula nyama ktk naeneo ya mkoa wa Iringa kwa hofu ya kula nyama ya mbwa,Wapo waliooa au kuolewa na wahehe,na walipofika ukweni wakagoma katakata kula nyama,hata walipoona mbuzi akichinjwa ”live“,ni bahati nzuri au mbaya hata wahehe wenyewe huona fahari kuitwa wala mbwa,sbb kwao ni utani,na wao hawajachukua juhudi zozote za kuuweka wazi ulaji wao wa mbwa.
Wahehe si mila yao kula mbwa,haijawahi kutokea...japo watani wa wahehe uwahusisha wahehe na ulaji wa mbwa,Mtani wa mhehe ni Mngoni na Mmanda si Mnyakyusa wala Mbena kama wengine wanavyodhani.Hutaniana ktk misiba na harusi,utani wao huenda mbali kama kumwagiana maji,kuwaanika wafiwa juani mpaka kiasi fulani cha pesa kitolewe ambacho huchangia shughuli za msiba,hupakana unga au majivu kama sehemu ya utani.Wapo ambao hunyang'anywa viatu au kanga ili watoe pesa,lengo la utani ni kuwafariji wafiwa,kuchangamsha eneo la msiba lisigubikwe na wimbi la majonzi na wakati mwingine kuburudisha.
Wahehe chakula chao kikubwa ni ugali wa kiwerege,nyama na matofu(viazi mviringo),hakuna wazee wapenda nyama kama wazee wa zamani wa kihehe,wakati wa kula ilikuwa ni kosa sana kwa mtoto kuanza kuchukua nyama kabla ya mzee,na wakati mwingine mzee ndio alikuwa na jukumu la kukuchagulia nyama ya kula,kwa kuitoa ktk mchuzi na kuinyonya ndio akupe.Kinywaji chao kikuu ni pombe ya ulanzi na komoni...haikuwahi kutokea mhehe kufuga mbwa kama kitoweo.
Mbwa hufugwa kama mlinzi na msaidizi machungoni,wahehe wana miiko ktk vyakula(lusilo) kulingana na ukoo,wapo wasiokula kanga(ndege),bandama,nyopolwa(ndama),moyo wa ng`ombe,firigisi n.k n.k!!
Ktk maisha yao ya kijamii wahehe huwatenga watoto wa kike na wa kiume,baba hukaa mbali na watoto wa kike,haikutokea watoto kujua au kuchangia choo na baba,wala watoto walikuwa hawajui kama baba huenda chooni,baba akijisikia haja,hubeba kajembe kake na kupiga mruzi kuita mbwa wake na kutokomea porini...hali hii iliwafanya watoto waamini wakubwa hasa baba haendagi chooni wala kujisikia ”kupumua”,ndio maana wahehe wana msemo wanasema ”mvina siafula= mkubwa hajambi(asha kumu si matusi“
Kwa asili wahehe hawataili,si mila yao kwenda jando,baadae baada ya muingiliano na wamisionari ndio wakaanza kutahiri,huoa mitala,ni fahari kuwa na wake zaidi ya mmoja.Ni wakulima wazuri ktk kipindi chote cha mwaka...nyakati za kiangazi hulima ktk ”finyungu“ mazao ya mbogamboga.Wameathiriwa na dini ya kikristo ktk dhehebu la Katoliki,na hasa baada ya ujio wa wamisionari wa Benedictin ktk maeneo ya Tosamaganga,na baadae ujio wa wamusionari wa Consolata.Uislamu kwa asili upo ktk eneo Kalenga na Pawaga, na maeneo ya Pawaga lilifikiwa na Waarabu kutokana na uwindaji wa Pembe za Ndovu kandokando ya iliyokuja baadae kuwa mbuga ya Ruaha...si ajabu wahehe waislamu wengi hutoka maeneo haya.
Eneo la Uhehe ndio liliokuwa tishio kivita,liliwatisha wavamizi wa kigeni na wenyeji..'uzuri wa jeshi la kihehe analijua kiongozi wa wasangu na wabena,kutoka nje adhabu aliyoipata Jemedari wa kijerumani Zelewisky kwa kuuwawa na askari wa kihehe imebaki mpaka kesho ktk vitabu vya historia vya Wajerumani.
Wanawake wa kihehe ni wachapakazi,wachamungu na waadilifu sana,wameumbwa na utii na hofu kwa wanaume,sio wahuni lkn wana huruma kila waombwapo...wao huamini ktk hofu ya Mungu,ndio mana ukiwaomba watakujibu ”vee niangusage elaa ulyee,isambi sa kwako“....yaani we niangushage ule,zambi za kwako.Ni wachapakazi ndio maana wadada wengi wa ndani hutoka Iringa.Tatizo lao ni hasira,wana hasira sana...ukimuuzi hataki tabu,anakuachia dunia kwa kujinyonga ili wewe uishi kwa amani.
Wana uwezo wa kuongoza lkn si hawana spirit ya ”ubepari“,i.e aggressive in investment,lkn wakipata mtu wa kuwaongoza ni wasimamiaji na watekelezaji wazuri sana ktk uwekezaji.
Tatizo lao ni pombe,kukuta muhehe hanywi ni nadra sana,kukuta hana hasira ni nadra,lkn wanajua kupenda na kumjali mwanamke,ni wasiri sana,yamkini hufaa ktk kazi za kishushushu.Hawapendi kunyanyasika au kuona mtu ananyanyaswa,mfano wa Mwamwindi kwa Mkuu wa mkoa Dr.Wilbert Kleruu inaeleza jinsi wasivyopenda kuonewa,makofi aliyokula mkuu wa mkoa Said S. Shamshama akiwa jukwaani toka kwa mzee wa kihehe miaka ya 1960's baada ya kuwadhihaki ni alama halisi ya hawa watu kuikataa dharau,si ajabu ktk muitikio wa mfumo wa vyama vingi wahehe walikuwa ni moja ya mkoa uliopokea mabadiliko kwa kumpa ushindi mbunge wa Upinzani.
Wahehe wana kiburi,wao huita ”kidada“,hawapendi kujipendekeza hata kama hawana kitu...wao hutumia msemo wa ”ndimgaya sidaa“,hata kama hana mia mfukoni ni mara chache kijishusha.
 
Back
Top Bottom