Ni kweli viongozi wa vyama vya upinzani `mavuvuzela?` | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli viongozi wa vyama vya upinzani `mavuvuzela?`

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MTWA, Jul 14, 2010.

 1. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana JF  Mimi binafsi sijafurahishwa na vile Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulivyotumika kuwananga viongozi na wanachama wa vyama vya siasa kwa kuitwa ‘mavuvuzela’.
  Vuvuzela ni aina ya tarumbeta zinazotumika katika kushangilia timu zinazoshiriki katika fainali za kombe la dunia zinazofikia kilele chake hivi karibuni. kwa timu za Taifa za Hispania na Uholanzi.
  Wakati wapinzani wakiitwa mavuvuzela, viongozi wake wakuu akiwemo Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti wa CUF), Augustine Mrema (Mwenyekiti wa TLP) na Said Arfi (Makamu Mwenyekiti wa Chadema) walikuwemo ukumbini Kizota mjini Dodoma.
  Pia walikuwepo viongozi kutoka vyama vya upinzani vya NCCR-Mageuzi, UMD, SAU, Demokrasia Makini, NRA, AFP, NLD, APPT, UPDP, Tadea) na UDP.
  Waliotoa tamko hilo ni wanafunzi wa Vyuo Vikuu walio wanachama wa CCM, wakati wakiimba na kuwasilisha salamu zao kwa wajumbe wa mkutano huo.
  Wakati wakiimba wimbo maalum, miongoni mwa maneno yaliyotamkwa ni “mwaka huu tutawacharaza wapinzani, tuwape adabu, tuwapige kwa kura ya ndiyo…shika kura yako juu, tandika sawasawa…mavuvuzela hao hawatuwezi,”
  SASA JE KAMA HII NDO TANZANIA TUTAKUJA FIKA WAKATI TUKAKOMBOLEWA NA HII HALI TULIYONAYO?
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unajua hili jina limewaangukia CCM na kama sikosei humu JF ndimo walimopachikwa cheo hicho au jina hilo,kilichotokea ni kuonekana kuwa kati yao amepita na kusoma ile kitu na kabla haijasambaa ,naweza kusema wamewahi ,lakini bado jina hili linawaandama tu na wala huko kutamka kwao katika kikao cha Dodoma hakutawasaidia kitu.

  Hebu iangalie CCM ,maana hio CCM peke yake inatosha kuirefusha na kusomeka kwa kirefu kama ..CCM= CHAMA CHA MAVUVUZELA ,sijui kama umeona hapo ,afu watazame wanapokuwa kwenye mikutano yao wanaweka rundo la mazungumzo lakini hayana maana hata moja, watu hawawezi kuyaepuka wala haiwezekani ukawambia sivyo maana hawaambiliki na hawasikilizi la mtu ,watu kila kona si walilalamika kuhusu mavuvuzela kuna alie wasikia ???
   
Loading...