Ni kweli Vidonda vya Tumbo vinaweza kupelekea Umauti?

Kipenseli

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
800
1,050
Habari zenu wana JF.

Mimi ni Muathirika wa tatizo la Vidonda vya Tumbo Almost Mwaka sasa lakini kutokana na kuutibu huu ugonjwa bila mafanikio nimepata comment mbali mbali ambazo nyingine zimenipa khofu.

Nataka niamini tunkwa ushuhuda ni kweli vidonda vya tumbo vinaweza kupelekea kifo? na je ikifikia stage gani ya maambukizi mpaka kupelekea kifo? je ni nini dawa mujarabu ya tatizo hili?
 
mo effect,
Ukweli ni kwamba itakupa saratani ya utumbo, Mimi nina mzee wangu lishamtokea Hilo, akafariki kwa saratani au cancer, kuhusu hayo matibabu sina uhakika, ila angalia ushauri wake USIPUUZE, Watu humu jf ndivyo wanavyosaidiana..
 
Mkuu usihofu sana, tambua abnormality yoyote kwenye mwili isipokuwa ulemavu inaweza kupelekea kifo,usipozingatia mashariti ya namna ya kuishi na vidonda vya tumbo yaweza pelekea kifo, but kwa nadra sana, ukiwahi kuna operations huwazinafanywa kwa watu wa tatizo kama hili.

But Mimi mwenyewe ni mgonjwa au mwathirika wa madonda ya tumbo huu ni mwaka wa tatu,nimejitahidi sana kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya hivyo hata maumivu siyasikii kwa mwaka wa pili sasa.

Kuna mama yangu mdogo yeye ameishi na madonda ya tumbo kwa 20 yrs ,juzi alienda kufanyiwa kipimo cha OCG kujua maendeleo yake ili kama imefikia hatua ya kufanyia operations wamfanyie lakini madaktari walisema yuko kawaida na wala hahitaji huduma hivyo,

So usiwaze sana mkuu,kifo kipo tu,kikubwa zingatia ushauri wa wataalamu wa afya na pia zingatia vyakula vya asili,Mimi ninayeandika hapa Nina miaka miwili bila kutumia dawa za hospitali kwa watu wenye madonda ya tumbo kwa sababu tu nazingatia ushauri wa kitabibu
 
Habari zenu wana JF.

Mimi ni Muathirika wa tatizo la Vidonda vya Tumbo Almost Mwaka sasa lakini kutokana na kuutibu huu ugonjwa bila mafanikio nimepata comment mbali mbali ambazo nyingine zimenipa khofu.

Nataka niamini tunkwa ushuhuda ni kweli vidonda vya tumbo vinaweza kupelekea kifo? na je ikifikia stage gani ya maambukizi mpaka kupelekea kifo? je ni nini dawa mujarabu ya tatizo hili?
Mshana Jr njoo ujibu huku
 
Nmesumbuka na hl tatzo snce 2012. Last year ikawa chronic kulazwa kila baada ya mwezi. Washaur n weng na dawa utaambiwa nying sanaa.

Zote n story tu dawa zpo hospitali. Utatakwa pata specalst, vpmo then kuanza clinc. Baada ya hapo utakua shwr kbsaa
 
Habari zenu wana JF.

Mimi ni Muathirika wa tatizo la Vidonda vya Tumbo Almost Mwaka sasa lakini kutokana na kuutibu huu ugonjwa bila mafanikio nimepata comment mbali mbali ambazo nyingine zimenipa khofu...

Tatizo la vidonda vya tumbo ukikaa nalo mda mrefu unapata complications kuu tatu(ya nne na ya tatu zinafanana kimantiki na kidalili).
1. Hemorrhage/Utaanza kutapika damu au kunya kinyesi cheusi au chenye damu(Vidonda vinakua vinachimba zaidi kuta za tumbo/utumbo na kupasua mishipa ya damu).

2. Perforation(Uchimbaji ukiendelea tundu litatokea na uchafu(Vyakula na enzymes) utaingia kwenye peritonium(Mfuko uliobeba viungo vya tumboni).

3. Gastric Outlet Obstruction/ Chakula kushindwa kutoka nje ya tumbo na utakua unashiba haraka na kutapika mara kwa mara.

4. Gastric cancer(Sana sana kama vidonda vyako vimesababishwa na Helicobacter Pyroli).

Katika hizo complication hakuna ambayo inaweza isikuondolee uhai iwapo hautachukua matibabu mapema, mfano ukitapika damu unaweza kufa kwa sababu zilizo wazi, kuta za tumbo zikitoboka vyakula na enzymes zikaingia kwenye peritoneum, viungo vyote vitaathrikika na usipofanyiwa upasuaji unakufa ndani ya siku chache tu.

Complications mbili za mwisho zina kuua taratibu(utaacha kula sababu chakula hakiondoki tumbo unhisi umeshiba, kutapika mara kwa mara, cancer itakunyonya na inaweza kusambaa na mwisho utakufa) ila mbili za mwanzo unaweza kufa mara moja.

Mimi ni daktari mjasiriamali nimefungua Medical clinic mwezi mmoja wa kwanza nimekutana na wagonjwa 14 wako Positive na Helicobacter Pyroli ambae ndo cuprit zama hizi na anawapa dalili zote za vidonda vya tumbo wagonjwa hao.

Kati ya hao kumi na nne, wagonjwa watatu ndo wamekubali kuanza dose na Mmoja tu ndo amendelea na dose mpaka stage ya mwisho hao wawili walipopata haueni kidogo katika week ya kwanza wakaacha dawa, na ambao hawakuanza dawa wanasema eti watatibu kwa miti shamba, wengine eti watafata masharti ya chakula wengine wanasema huo ni ugonjwa wao wameuzoea.

Watanzania tuache hii dhana ya kijinga ya kusema mm ni mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kuishi na vidonda vya tumbo kama vile ni ugonjwa usiotibika, asilimia zaidi ya 90 ya wagonjwa wenye vidonda vya tumbo husababishwa na Bacteria(Helicobacter Pyroli) na huyu bacteria anaweza kuuliwa kwa dawa na sio masharti ya chakula.

Tuache ujinga wa kufata dhana za mitaani kutanenI na madaktari wanaolewa medicine wawape dynamics mpya za Gonjwa hili, madaktari wengi wa zamani wametuachia dhana mbaya na ugonjwa huu.

Tuachane na dhana za kizamani pia kuwa vidonda vya tumbo husababishwa na kutokula kwa wakati na nyingine nyingi zilizopitwa na wakati.

Vidonda vya tumbo vinatibika hospitalini ni wewe kumeza dawa utakazo pewa, kulingana na vidonda vyako unaweza kuitaji kumeza dawa hata miezi miwili na wengine mpaka kwenda kufanyiwa kipimo cha OGD.

ukiacha dawa bila kumaliza dose utatengeneza usugu wa dawa kwa huyo bacteria na itakua ngumu kukutibu na itabidi ufanye vipimo vya culture and sensitivity na dawa zake lazima zitakua expensive kama za mwanzo zilikushinda
 
Nasikia maziwa ya mbuzi ni tiba ya vidonda vya tumbo pia yanaongeza kinga ya mwili, jaribu kutumia uone kama yatakusaidia. Source: radio TBC
Hii ndo inatumaliza watanzania, maziwa ya Mbuzi hayawezi kuua bacteria ambae ndo anasabaisha vidonda kwa zaidi ya 90%
 
Tatizo la vidonda vya tumbo ukikaa nalo mda mrefu unapata complications kuu tatu(ya nne na ya tatu zinafanana kimantiki na kidalili).
1. Hemorrhage/Utaanza kutapika damu au kunya kinyesi cheusi au chenye damu(Vidonda vinakua vinachimba zaidi kuta za tumbo/utumbo na kupasua mishipa ya damu)...
Upo sawa Dr .. Me nlfanya ogd, vdonda vlkuwa vngi na vkubwa kwa mfuko wa chkula. Nmeattend clnc 6 Moth bla kukosa pluz dose..... Now am fine. God s good
 
Habari zenu wana JF.

Mimi ni Muathirika wa tatizo la Vidonda vya Tumbo Almost Mwaka sasa lakini kutokana na kuutibu huu ugonjwa bila mafanikio nimepata comment mbali mbali ambazo nyingine zimenipa khofu.

Nataka niamini tunkwa ushuhuda ni kweli vidonda vya tumbo vinaweza kupelekea kifo? na je ikifikia stage gani ya maambukizi mpaka kupelekea kifo? je ni nini dawa mujarabu ya tatizo hili?
Habari,
Ni kweli kuwa kama una vidonda vya tumbo, vyaweza kupelekea mtu kupoteza maisha. Hii hutokana na matatizo yanayofuatia/ complications za vidonda vya tumbo.

LAKINI:
Kabla ya yote ni vyema kuelewa kuwa ni pale tu unapofanya vipimo husika kama yule aliyefanya OGD, ndiye anaweza kusema ana vidonda vya tumbo. Hivyo kama haujafanya vipimo, ni vyema kufika hospitali na kusikilizwa vyema ili upate tiba kulingana na hali yako.

Kuna matatizo mengine mengi ambayo yanashabihiana na shida ya vidonda vya tumbo kwa dalili.

1: Si wote wanaopata maumivu kwenye eneo la tumbo chini ya kifua huwa tatizo ni vidonda vya tumbo.

2: Si kila mwenye H. Pylori/wadudu wanaosababisha vidonda vya tumbo tayari ana vidonda vya tumbo.

3: Si kila mwenye vidonda vya tumbo ana H. Pylori

4: Si kila mwenye dalili ya kuwa na vidonda vya tumbo anastahili muunganiko wa antibiotiks na dawa ya kupunguza acid kwa pamoja.

4: Usitumie dawa kwa sababu mtu aliyekuwa na dalili kama zako alipona.

SABABU:
1:Matibabu hutegemea na unaumwa nini?
Itasaidia aina ya matibabu.

2: Chanzo cha tatizo?
Itasaidia nini ufanye au usifanye ili upate kupona.

3: Hatua ya ugonjwa?
Aina ya tiba na kwa muda gani.
 
Ikifika stage unajisaidia vibonge vya damu hiyo haijakaa poa Mkuu.

Ila vidonda vya tumbo nasikia vinatibuka kwa mifumo ya tiba lishe mkuu.

Alafu pia vinaambukiza sababu ni bakteria.

Pole sana mkuu, zingatia ulaji wenye masilahi kiafya mlo kiasi ila uliokamilika mara kwa mara.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom