Ni kweli... Uwekezaji wa namna hii, hautatusaidia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli... Uwekezaji wa namna hii, hautatusaidia.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanakili90, Jan 23, 2012.

 1. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jaribio la januari 5, 2012, la kutaka
  kuiteka dhahabu iliyokuwa
  inasindikizwa kutoka kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita
  ikipelekwa kwenye uwanja
  mdogo wa ndege kwa ajili ya
  kusafirishwa nje ya nchi.

  Mwanzoni ilielezwa kwamba
  dhahabu iliyokumbwa na
  msukosuko huo ilikuwa na
  uzito wa tani moja (kilo elfu
  moja), kabla ya Wakala wa
  Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) kuingilia kati na kutoa
  ufafanuzi kwamba dhahabu
  hiyo ilikuwa na uzito wa nusu
  tani, yaani kilo 569.672.

  Wakala hao wakazidi kueleza
  kwamba dhahabu hiyo
  ilikuwa na thamani ya dola za
  Marekani milioni 26.16 sawa
  na shilingi za Kitanzania bilioni
  43.5.

  Wakala hao wakaongeza kwamba kati ya hizo shilingi
  bilioni 43.5, Tanzania
  inaambulia shilingi bilioni 1.18
  tu kama mrabaha (loyalty).

  Baada ya ufafanuzi huo wa
  TMAA ndipo maswali
  yanapojitokeza. Swali la
  kwanza ni kwamba jaribio
  hilo la kutaka kuteka dhahabu
  lilikuwa limelenga kupora au kuzuia uporaji?

  Source:TANZANIA DAIMA.
   
Loading...