Ni kweli unaweza kusajiliwa line zaidi ya moja bila kujua?

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
51,719
107,834
Jana nimejaribu ile namba *106# kuangalia namba zilizosajiliwa kwa NID yangu. Lahaula nimekuta imesajili laini mbili za wale YATOSHA!

Leo kitu cha kwanza asubuhi nimepita ofisini kwao nikafuta laini moja ambayo sijawahi kuitumia hata siku moja.

Tuwe makini wakuu unaweza kula mvua kimasihara kabisa
 
Wengi sana wamekutana na tatizo hilo kupitia mawakala vishoka
Mimi nilisajili ofisini kabisa,ila mtandao ulikuwa unasumbua tulirudia kama mara tano,nahisi hapa ndio laini mbili zikakubali bila kujua.
 
Ni hatari sana mtu uwe na namba ipo hewani alafu huijui.
Mimi kuna laini ya miamala niliitengeneza mwisho wa siku ikauzwa,jamaa akanambia laini haijatoka.na laini imetoka na inafanya miamala.
Naandaa nyuklia ya ICBM nikiifyatua huyo mwenye laini na aliemuuzia watanipa mtaji wa kubetia.
 
Aisee nilishtuka sana kuona namba imesajiliwa hata siijui wala kuitumia. Sema process ya kuifuta ni rahisi Sana ukifika kwenye ofisi zao.
 
Jana nimejaribu ile namba *106# kuangalia namba zilizosajiliwa kwa NID yangu. Lahaula nimekuta imesajili laini mbili za wale YATOSHA!

Leo kitu cha kwanza asubuhi nimepita ofisini kwao nikafuta laini moja ambayo sijawahi kuitumia hata siku moja.

Tuwe makini wakuu unaweza kula mvua kimasihara kabisa!
Usajili wako mwanzoni ulifanyia wapi mzee

Ova
 
Back
Top Bottom