Ni kweli ukiwa hujatahiriwa huruhusiwi kuchinja?

Status
Not open for further replies.

luswaguty

Member
Oct 13, 2017
86
29
Jamani mimi nina swali, Hivi mpaka uwe na uhalali wa kuchinja mnyama, mpaka uwe umetahiriwa, uwe muislam au kama ni muislamu halafu hujatahiriwa pia unaruhusiwa?
 
Mkuu yote yanawezekana( lakini hapo kama wewe ni muislam afu hujatahiriwa mimi sifahamu) inategemeana na muktadha, mtazamo na imani yako pia, mfano wewe ni mtu wa imani flani au unachinja kwa ajili ya watu wa imani flani then nimuhimu kufanya kulingana na matakwa yao
 
Hivi nguruwe pia huchinjwa na muislam? Na imani ya kiislam nguruwe haramu kuliwa. Kwani kama hujatahiriwa inakuwa haramu? Kama ndio jee mkristo akisilimu haruhusiwi kusali mpaka afanyiwe tohara?
 
Kutahiriwa kwa muislamu si wajibu bali ni sunna iliyotiliwa nguvu, kwani kuanzia kwa mtume Ibrahim hadi Isa na Muhammad rehma na amani ziwe juu yao mitume wote walitahiriwa ndiyo maana sisi waislamu tunatahiriwa kwa kufuata (mwenendo) sunna yao. Ndiyo maana utasikia umepata sunna? yaani umetahiriwa? Lakini kutahiriwa si lazima na kama hujatahiriwa hupati dhambi. Na kwa kuchinja katika imani ya kiislamu ni lazima mnyama achinjwe kwa kutajwa jina la Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye aliyeviumba viumbe vyake na katika kuvitoa uhai (kuchinja) kwa ajili ya chakula ni lazima akusudiwe Yeye katika kuchinja huko, hivyo basi dini za watu wa vitabu (ahlu al kitaab) yaani mayahudi na wakristo wakichinja wao katika wanyama waliyohalalishwa katika vitabu vyao hata waislamu wanaweza kula, muislamu amekatazwa kutokula nyama ya mnyama aliyechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
 
Ahsante kwa jibu murwa lakini bado bado nahitaji jibu moja tu.
Jee nguruwe huchinjwa na muislam? Mimi ni mwislam lakini nahitaji kujua jibu hilo tu.

Sent from my SAMSUNG-SM-G900A using JamiiForums mobile app
 
Hivi nguruwe pia huchinjwa na muislam? Na imani ya kiislam nguruwe haramu kuliwa. Kwani kama hujatahiriwa inakuwa haramu? Kama ndio jee mkristo akisilimu haruhusiwi kusali mpaka afanyiwe tohara?
nguruwe hachinjwi bali anakatwa shingo, ndio maana hata shoka anapigwa
 
Jamani mimi nina swali, Hivi mpaka uwe na uhalali wa kuchinja mnyama, mpaka uwe umetahiriwa, uwe muislam au kama ni muislamu halafu hujatahiriwa pia unaruhusiwa?
hakuna muislamu anaefikia hatua ya kuchinja bila kutahiriwa, we muislamu gani unanipa mashaka. we hujatoa damu unataka uwatoe wenzio we vp. no kuchinja katahiriwe kwanza
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom