Ni kweli ufisadi ni ajali ya kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli ufisadi ni ajali ya kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dotto, Jun 27, 2011.

 1. d

  dotto JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Ansbert Ngurumo


  WIKI hii, kuna mtu amejitambulisha kwangu kama msomaji mwaminifu wa safu hii; na amenitania akisema:

  "Mzee wa Maswali Magumu… naona umekuwa kiongozi wa uasi dhidi ya kauli za wakubwa. Matunda ya kazi yako na wengine tumeanza kuyaona. Endelea… nchi yetu inahitaji ukombozi wa kifikra. Sasa tumegundua kuwa akina ‘ndiyo mzee' wanachangia kuizamisha nchi yetu kwenye ufisadi…"

  Kwangu, haya ni maneno mazito sana. Yanatoka kwa mtu nisiyemfahamu. Yanaweza kupata tafsiri zaidi ya 100 kutoka kwa watu mbalimbali.

  Tungeweza kujadili na kuchambua kwa kirefu maneno kadhaa katika kauli hiyo, kwa mfano, uasi, kauli za wakubwa, matunda yaliyopatikana, ukombozi wa kifikra, kina ndiyo mzee, ufisadi na mengineyo yanayojitokeza kwenye ujumbe huu nliotumiwa.

  Lakini msingi mkuu wa ujumbe huu ni mmoja. Na unaweza kuelezwa kwa neno moja - uasi.
  Wakati umefika, Watanzania wanapaswa wajifunze kuasi. Si uasi wa hovyo hovyo, bali uasi katika mambo ya msingi; uasi unaoonyesha kwamba wamekua; wamekomaa.

  Watanzania wanahitaji kuonyesha kwamba sasa wanajua; wafanye uasi unaoonyesha kwamba sasa wapo tayari. Ndiyo ishara ya kuonyesha kuwa wamechukia, na wanaweza kuchukua hatua.

  Uasi wa wananchi ndiyo umejitokeza katika ripoti ya Kamati ya Bunge iliyokuwa inaichunguza kampuni ya kitapeli ya Richmond. Bila uasi, Bunge lisingeunda kamati hiyo.

  Ndiyo! Wakati wa kushangilia makosa ya wakubwa umepita. Hizi ni zama za uasi dhidi ya utawala mbovu unaoambatana na matumizi mabaya ya madaraka. Ni uasi dhidi ya ufisadi.

  Watanzania wameanza kuasi. Wabunge wameanza kuasi. Nchi imechangamka. Viongozi bado wamezubaa; hawajui kinachoendelea!
  Na faida mojawapo ya uasi huu imeonekana wiki iliyopita. Mawaziri wamejiuzulu, na Baraza la Mawaziri limevunjwa. Kama tungekuwa watiifu, kina ‘ndiyo mzee,' nina hakika hili lisigetokea.

  Ndiyo! Nakubali. Uasi wa Watanzania umeanza kuzaa matunda. Juzi waliwazomea mawaziri wa Kikwete; jana wameshangilia anguko lao. Leo wana kazi nyingine; kesho ni mapinduzi. Huu ni mwanzo, si mwisho.

  Sasa Rais Kikwete amesikia, kinyume cha matarajio yake, kwamba nguvu ya wananchi imeshinda. Wananchi wamethibitisha kuwa ‘kelele za mlango' zinaweza kumzuia mwenye nyumba kulala.

  Lakini kuna jambo bado linanipa wasiwasi. Mwenye nyumba wetu (Kikwete) hajapata tafsiri sahihi ya kishindo cha nguvu ya umma. Walau hadi Alhamisi wiki hii, alipokuwa anawahutubia wazee wa Dar es Salaam, alikuwa hajatambua hisia halisi za Watanzania.

  Vinginevyo, angeepuka kabisa kuwamwagia sifa kemkem mawaziri waliolazimishwa kujiuzulu kwa sababu ya tuhuma za ufisadi. Walau asingewataja kwa majina, kuwasifu na kuwasikitikia.

  Zaidi ya hayo, asingewaita "waadilifu, wazalendo na waaminifu" katika mazingira ambayo ‘kila mtu' anajadili ufisadi wao. Kwa hili, Kikwete amejitenga na Watanzania. Maneno haya yamemchafua.

  Watanzania wanashangilia anguko la ‘mafisadi,' huku baadhi yao wakidhani rais yuko upande wa wananchi; kumbe mwenzao yuko kambi nyingine kabisa. Anaonyesha masikitiko ya wazi.

  Hivi hakujiuliza kwa nini wananchi nchi nzima walishangilia sana kujiuzulu kwa mawaziri wake, hasa waziri mkuu? Na alipozitazama nyuso za wazee alikuwa anawahutubia aliona wanakubaliana naye? Mwitikio alioutarajia ndio waliompa?

  Kwa maneno haya, hata waliokuwa wameanza kudhani kwamba Kikwete alishirikiana na Spika wa Bunge, Samwel Sitta kuitumia Kamati ya Bunge kama njia ya ‘kuondokana' na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, wamepata jibu.

  Wao walidhani kwamba isingekuwa rahisi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Dk. Harrison Mwakyembe, kuwa jasiri na muwazi hivyo, bila kuwa na baraka za Rais Kikwete. Walikosea. Katika zama za uasi mtakatifu kama huu, hilo linawezekana.

  Bahati mbaya, walichelewa kujua msimamo wa Rais Kikwete kuhusu suala la Richmond; kwamba katika hili yuko na Lowassa.
  Yeye mwenyewe anabaki kuwashangaa wabunge na wananchi wanaowazomea na kuwashindilia maneno mazito watuhumiwa wa Richmond, hata baada ya kujiuzulu. Kikwete haoni ufisadi wa Lowassa katika suala hili.

  Bahati nzuri ametamka mwenyewe kile anachokiona kwa Lowassa – ajali ya kisiasa! Ni sababu hiyo hiyo iliyonifanya niandike Jumapili iliyopita kwamba, Lowassa amebeba mzigo wa Kikwete.

  Nilisema Lowassa hakufanya uamuzi wa kuibeba Richmond peke yake. Ndiyo maana aliweza kujiamini, na hakuchukuliwa hatua yoyote kwa miaka miwili hadi Bunge lilipoamua kufanya uasi kwa kuitikia nguvu na kauli ya wananchi.

  Na hii kauli ya juzi ya Rais Kikwete (kwamba hii ni ajali tu ya kisiasa), ni kichocheo kingine cha uasi wa Watanzania ambao unakuja. Ndiyo maana baadhi yetu hatubaki tu kushangilia na kupigia makofi hotuba za rais.

  Tunajua kwamba katika kauli zake nyingi, ukweli unawekwa pembeni, propaganda inatangulizwa, ili kuwahadaa au kuwapoza wananchi. Ni maneno mengi, matamu; hakuna hatua. Na hatua zinapokuwapo, hazilingani na maneno yaliyotamkwa.

  Nitatoa mfano wa hivi karibuni. Mwishoni mwa Januari, Rais Kikwete alilihutubia taifa akidokeza ubaya wa kuwa na mawaziri na wabunge wafanyabiashara. Alidokeza kwamba ataanzisha mchakato wa kisheria ili kuhakikisha wenye biashara wanakaa mbali na madaraka ya kisiasa.

  Kina ‘ndiyo mzee' waliwahi kupiga makofi. Tena baadhi ya waandishi wakasema sasa ‘tunarejea enzi za Azimio la Arusha.' Wengine wakathubutu kusema ‘sasa Kikwete kawa Nyerere!'

  Wanaolijua Azimio la Arusha vizuri, na wanaomfahamu fika Julius Kambarage Nyerere, wataendelea kuiona hii kuwa ni kufuru!

  Baada ya ripoti ya Mwakyembe kuja na mapendekezo kadhaa, mojawapo likifanana na hilo alilotoa Kikwete juu ya wanasiasa wafanyabiashara, baadhi ya wadadisi wa mambo wakasema: "Kikwete alipata taarifa za kikachero kuhusu ripoti ya Mwakyembe kabla haijawasilishwa bungeni, akalichomoa hilo ili kupoza machungu ya wananchi wanaomlaani kwa kuiuza nchi kwa rafiki zake wafanyabiashara, ambao naye aliona kwamba mwisho wao serikalini unakaribia, ingawa hakujua mwisho wao ungekuja lini na kwa namna gani."

  Baadhi yetu tulitarajia kwamba maswali tuliyomhoji yangemsaidia kutuonyesha alivyo makini. Fursa ya kuonyesha umakini alikuwa nayo hasa baada ya Lowassa kumsaidia kuvunja baraza.

  Alipounda upya baraza lake na kuwatangaza wateule wapya, sikuona waziri asiye ‘mfanyabiashara.' Lakini wale waliokuwa wanadhani kuwa mfanyabiashara lazima afanane na Nazir Karamagi au Rostam Aziz, au hata Lowassa, wakasema "ameunda baraza lisilo na wafanyabiashara." Kweli?

  Kwani mfanyabiashara ni nani? Mfuga kuku? Mwenye mashamba ya tumbaku au miwa? Mmiliki wa daladala? Mmiliki wa shule binafsi? Mwenye mgodi wa dhahabu? Mwenye hisa katika kiwanda chochote? Mwenye duka la mitumba au bidhaa zozote? Mwenye saluni ya urembo? Mwenye kampuni yoyote binafsi? Ni nani huyo mfanyabiashara tunayemlenga, au anayezungumzwa na Kikwete? Mbona ndio hao wamejaa kwenye baraza jipya la mawaziri?

  Lakini hoja yangu mimi ni tofauti. Sichukii wafanyabiashara wanasiasa. Sikubaliani na Kikwete (na wanaofanana naye katika hili) kwamba wafanyabiashara wasiwe wanasiasa au wanasiasa wasiwe wafanyabiashara.

  Sitaki wanasiasa malofa na ombaomba ambao ni rahisi kutumiwa na wenye pesa. Wao hawatakuwa wafanyabiashara, lakini watawatumikia ‘wafadhili' wao na njaa zao. Tunayo mifano mingi ya wafanyabiashara waliowatumia wanasiasa baada ya kufadhili kampeni zao na kuhakikisha ushindi wao.

  Wako mbali kabisa na Ikulu, wizara na Bunge. Lakini wana nguvu kuliko mawaziri na wabunge wenyewe. Kisa?

  Pesa yao.
  Hatujasahau yanayosemwa kuhusu mzozo wa mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga. Wanasiasa wametumika, na wanaendelea kutumika, kuuza rasilimali za taifa kwa wafadhili wao.

  Hatutaki siasa zinazopendekezwa za kuwatumikia wafanyabiashara, bali tunataka biashara zinazotumikia siasa.

  Wapo baadhi ya wafadhili wa CCM wasiopenda kujitaja, na wasiopenda kutajwa na mtu. Lakini vitabu vyao vya hundi vinawataja. Tunawajua. Wako karibu na wakubwa kwenye chama na serikali. Wao si wanasiasa wa waziwazi, ingawa dalili zipo kwamba wanazengea kuingia kwenye siasa.

  Lakini kila tenda kubwa serikalini ikitangazwa, wamo! Wenye mahoteli wanapelekewa mikutano mikubwa mikubwa na yenye pesa nyingi za serikali. Wenye biashara za kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi, wanapewa upendeleo maalumu au msamaha wa kodi. Kisa? Ni wafadhili wa wakubwa.

  Haya ndiyo mambo ambayo Kikwete alipaswa ayatazame na kuyafanyia kazi. Hawa ndio wafanyabiashara wanaokomaza ufisadi. Wanawatumia wanasiasa wetu, hasa hasa wale wenye njaa na tamaa.

  Tunao wanasiasa wajanja wajanja na wakwepa kodi pia. Wengine wamejipenyeza pole pole kutoka kwenye ufadhili wa CCM na kuwa ‘vigogo' wa chama. Baadhi yao wamo serikalini. Wengine ni aibu ya rais mwenyewe; na wengine ni aibu kwa taifa. Ni mzigo!

  Baadhi yao wamekuwa na biashara zao huko nyuma, lakini zimekua kwa kasi katika miaka ya karibuni, hasa katika kipindi ambacho mabilioni yamechotwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania, wakiwa karibu na wakubwa!

  Wengine, tena katika miaka miwili iliyopita, waliteuliwa kuongoza wizara zenye uhusiano wa moja kwa moja na biashara zao au za ndugu zao. Njia ya kuwandoa hawa na kuwazuia wengine kuwa kama wao ipo, lakini si kuharamisha biashara.

  Kelele alizodhamiria kuzipoza Rais Kikwete zina mizizi yake. Hoja isiwe biashara ya mtu, bali uadilifu unaoambatana na biashara ya mtu; na uhusiano wake na wakubwa serikalini.

  Kuwanyanyapaa wafanyabiashara kwa sababu tu ya biashara zao ni kuwaonea wivu, na ni ujinga. Ni udhaifu wa kushindwa kuona tatizo halisi. Au labda ni ujanja wa kuwasaidia wafanyabiashara ambao baada ya kuwa serikalini kwa muda sasa, wameamua kujiweka mbali ili kufanya mambo yao gizani.

  Wakiwa nje ya serikali, wanajielekezea mifereji ya rasilimali zetu, mithili ya wakoloni na uchumi wetu tegemezi. Waliondoka, lakini ndio wanaofaidi rasilimali zetu wakiwa kwao Ulaya na kwingineko.

  Na hata wanaporejea, hawaitwi wakoloni, bali wawekezaji. Wanapewa viti vya mbele; wanatukuzwa na watawala wetu wale wale wanaojivunia ‘uhuru' wa nchi yetu!

  Dhamira ‘nzuri' ya Kikwete imekuja wakati usio wake. Hata akipunguza tena ukubwa wa baraza, ni vigumu kuwapata mawaziri 20 au 15 wasio wafanyabiashara.

  Kwa hali ilivyo sasa, ni vigumu kuwa na viongozi na washauri wao wasio wafanyabiashara. Uteuzi wake wa juzi, umeonyesha kwamba hiyo ndoto atakufa nayo.

  Ni vema atambue kuwa dunia ya sasa na tunayoiendea, ni dunia ya biashara. Wakati ujao ni wa biashara. Tunachohitaji si kuwanyanyapaa wafanyabiashara, bali kutafuta njia na sera mwafaka za kuhakikisha biashara hizi zinatumika kulinufaisha taifa.
  Tuondoe na kudhibiti migongano ya kimaslahi katika biashara za wanasiasa wetu. Rais atumie vizuri mamlaka yake ya uteuzi kuhakikisha hashiriki kuuza nchi kwa wafanyabiashara wasio waaminifu.

  Lakini atambue pia kuwa kimsingi, ufumbuzi halisi wa tatizo hili ni vema uwe wa kikatiba kuliko tu wa kisheria na hisia.

  Ni dhana inayopaswa ijadiliwe kwa upana wake, si kwa mtazamo wa Azimio la Arusha, ambalo halipo; wala Azimio la Zanzibar, la kijambazi ambalo halijafutwa; bali kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kitaifa, si ya watawala peke yao.

  Na hata litakapoletwa, lisifanywe tu ajenda ya propaganda za walio madarakani, katika jaribio la kujikosha na ufisadi.

  Litekelezwe kwa kuzingatia visheni pana ya kitaifa, na vita dhidi ya ufisadi, si kwa nia ya kuepusha ‘ajali za kisiasa' za wakati huu.

  WANAJF: YAWEKANA VIPI TZS.152m IKAWA AJALI YA KISIASA NA MAJIBU MARAHISI NAMNA HIYO??????? CHANGIA
   
 2. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dah napita njia hapa.
   
 3. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2015
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,821
  Trophy Points: 280
  Hii kauli inahitaji ufafanuzi na ndugu zangu waandishi mkipata fursa ya kukutana na yule alieitoa hii kauli mwambieni watanzania tunataka aitolee ufafanuzi.

  Waandishi mumuhoji afafanue kauli hii kabla ya uchaguzi mkuu haujafanyika alafu tuone kama watakuwa na "moral authority" ya kuendeleza jambo hili kwenye mikutano ya campaign.
   
 4. Kansigo

  Kansigo JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2015
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,664
  Likes Received: 1,467
  Trophy Points: 280
 5. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2015
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,821
  Trophy Points: 280
 6. N

  Ngoso JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2015
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 521
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Warejee tamko la serikali lililotolewa na waziri mambo ya nje kuwa wawe watazamaji tu na sio wasemaji
   
 7. Exaud

  Exaud JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2015
  Joined: Oct 12, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Hii ni habari ya kutungwa, chunguza hata jina la gazeti halipo, pia content yake ni dhaifu sana haina hata takwimu
   
 8. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2015
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Kama hii habari ni ya kweli, basi inathibitika kabisa hii nchi ni ya kifisadi na ya wizi kwa maana kwamba hao watu wa EU Wameshasaini mikataba ya kilaghai na Serikali yao pendwa ya CCM na wanaogopa akiingia Lowassa aataifutilia mbali hiyo Mikataba hivyo watakosa gasi na Mafuta ya bure

  cc: Ngoso, Exaud, Kansigo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. SUPER PREDATOR

  SUPER PREDATOR JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2015
  Joined: Apr 29, 2014
  Messages: 2,090
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh. Membe alikanusha Mara moja kuwa hakuna kiongozi yeyote anayeshiriki kwenye biashara hiyo baada ya kudaiwa kuwa ndege ya rais wa China ilitumika kubeba meno ya tembo alipotembelea hapa nchini kwetu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. e

  emalau JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2015
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hii habari imetungwa siku nyingi sana, nimeshaisikia watu wanaongea mtaani nikwaambia EU hawana sera ya kuingilia mambo ya ndani ya nc hi kwa kiasi hicho.

  Huyo mtu atuwekee jina la gazeti, ni lanchi gani na toleo namba ngapi na tarehe gani
   
Loading...