Ni kweli tunategemea mikopo mpaka kwenye matumizi yetu ya kawaida??

Digaller

JF-Expert Member
Oct 20, 2009
745
427
Nimejaribu kwa muda mrefu sana kutafakari hotuba ya Bajeti iliyowasilishwa Bungeni lakini sijapata jibu mwafaka, nina maswali ambayo nataka tujadiliane wana JF:-
  • Je tunahitaji kupangiwa Bajeti na wazungu kwakuwa sisi imetushinda?
  • Je hatuna wataalamu wa kutosha kuweza kupanga bajeti yetu?
  • Je baraza la mawaziri lilishirikishwa kikamirifu wakati wa utungaji wa bajeti hii?
  • Kamati za bunge zilikuwa zinafanya nini mpaka tunaletewa madudu kama haya bungeni?
  • Je ni kwa vipi mtu anaweza kuishi kwa kipato cha 80,000 lakini matumizi yake kwa mwezi ni shilingi 100,000?
  • Je viongozi wetu wamelewa madaraka kiasi kwamba hawaelewi wapo pale kwaajili ya nani?

NOTE: Mapato ya Tanzania ya ndani kwa mwezi ni 8 Trillion, Matumizi 10 Trillion.
 
NOTE: Mapato ya Tanzania ya ndani kwa mwezi ni 8 Trillion, Matumizi 10 Trillion.

Hata haya mapato yakichunguzwa kama alivyotaka mbunge wa Simanjiro, Mh. Sendeka...nina uhakika itakuja kuonekana kwamba kuna pesa za kujaziwa humo nazo zimekopwa toka kwenye mabenki. TRA imekopa to sex up revenue
 
Mnyika; Mimi si dhaifu ila niko kwenye bunge dhaifu Lenye magamba mengi yanaoongozwa na m/kiti dhaifu anayeongoza serikali dhaifu, na aliyeteua mawaziri dhaifu waolioleta bajeti dhaifu na kuutetea kwa hoja dhaifu na mikakati dhaifu ya kumfukuza mbunge mzuri Mnyika anaowaambia ukweli kuwa wao wabunge ni dhaifu na Rais wao JK ni dhaifu.
 
Matumizi ya kawiada ndio huchukua sehemu kubwa ya bajeti za nchi nyingi duniani haiepukiki eneo hili kutumia misaada
 
Mnyika; Mimi si dhaifu ila niko kwenye bunge dhaifu Lenye magamba mengi yanaoongozwa na m/kiti dhaifu anayeongoza serikali dhaifu, na aliyeteua mawaziri dhaifu waolioleta bajeti dhaifu na kuutetea kwa hoja dhaifu na mikakati dhaifu ya kumfukuza mbunge mzuri Mnyika anaowaambia ukweli kuwa wao wabunge ni dhaifu na Rais wao JK ni dhaifu.

Kushindwa kumng'oa Johhn shibuda sio udhaifu??????????

kushindwa kujaza nafasi za mawaziri kivuli kwa muda mrefu sio udhaifu kama ya Regia Mtema????????

Udhaifu ni sehemu ya maisha ya binadamu.... kwenye masuala ya dini tunasema kila binadamu ni dhaifu ndio maana anatenda dhambi
 
Back
Top Bottom