Ni kweli Tumpe Dr. Slaa urais Mwaka 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli Tumpe Dr. Slaa urais Mwaka 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MTWA, Jul 23, 2010.

 1. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wana JF mimi Binafsi nimefurahishwa sana na suala la CHADEMA Kumteua Dr. wetu achuane na "mbayuwayu" katika uchaguzi mkuu mwaka huu. Nimefurahishwa kwa sababu atatoa changamoto na kama siyo kumng'oa kabisa. (hahahaaaaaa!!!!!!)
  Najua na wewe umecheka kidogo.
  Lakini nimesikitika kwa sababu utamu wa Bunge mwakani hamna kabisa. Fikiria ule ubishi wa Marehemu Chacha, hoja zake doctor, sasa si itakuwa ziiiiii, na ndiyo tu?
  Lakini pia licha ya CCm mwaka huu kuwa na upinzani mkali wao kwa wao, CHADEMA wamejipanga vyakutosha maana nijuavyo mimi ni kwamba sehemu nyingi za rural vyama vya upinzani havipo. wala hakuna modalities zozote. Nadhani labda wangewashawishi vijana wengi wajiunge na watengeneze matawi mengi kama ilivyo kwa CCM, na vijana hao wagombeee nafasi mbalimbali kwa rural areas. Lakini wakati umefika wa kuamka na kufanya mabadiliko
  TUMPE DR. SLAA URAIS
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chini ya Katiba iliyotungwa na CCM ambayo ndio inayoendesha mifumo ya aina zote hapa Tanzania usitegemee kama Slaa au Lipumba au kiumbe mwengine yeyote yule kuwa atashinda uchaguzi ,hilo sahau au sahauni ,ila ikifika siku na ukasikia kuwa kuna joto la mabadiliko ya Katiba limeanza na vyama vyote vinapiga makelele kushinikiza mabadiliko ya katiba basi hapo ndio uanze kuweka tamaa ya kuanguka kwa Sulutwani CCM = Chama Cha Mashetani. Hawa jamaa ni washirikina ile mbaya ,si mliona yale mauza uza ya bungeni mchana kweupe
   
 3. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Huo ni ukweli mtupu, Lakini unafikiri kama watanzania tungekuwa hatujalala kutambua mahitaji yetu ingewezekana hilo? HAPANA

  Kwa sababu hivi leo watu kibao wanajua kuwa tukichagua chama kingine kutakuwa na vita ya wenyewe. Tangu lini?
  Yaani ni asilimia kubwa sana hawajaona kama kuna haja ya mabadiliko, na hata wasomi wengi nao pia. lakini kama watu wangekuwa na uchu wa maendeleo na kuchukia haya maendeleo ya "sama soti' kuelekea nyuma na majigambo kibao,
  basi watu wote wangependelea kuwa tufikie maendeleo ya kweli.

  lakini kama usemavyo hawa jamaa huwa wanadiriki hata kutafuta ajali, majambazi na mengineyo kwa wale wanaoonekana wanataka kuleta uelewa kwa watu wengi.
  Na kwa vile watu wengi bado umasikini umekithiri basi wakiwapa vijisenti kidogo tu wanaona hamna taabu.

  La mwisho watanzania ni wavivu sana- kufikiri nini kifanyike lini, na pia kwa serikali ambayo haitoi mbinyo wa kufanya maendeleo kwa nguvu tunapenda sana. angalia jinsi watu maofisini wanavyokula mda na kupokea mishahara bila kuleta impact ya maana na wako comfotable
  Ni kwamba kama serikali leo itawabinya watu wafanye kazi kwa nguvu basi watu watachukia.

  Pia hatuna uchungu na maendeleo ukipata leo basi subiri kesho uone jinsi itakavyokuwa.
  "WE ARE NOT ENTREPRENEURS"
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Its high time for us to change this atitude, let's all become entrepreneurs kama usemavyo mkuu, let's go 4 Slaa come october!
   
Loading...