Ni kweli tovuti ya gazeti la UHURU imechakachuliwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli tovuti ya gazeti la UHURU imechakachuliwa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bantugbro, Oct 5, 2010.

 1. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wanajamvi usiku huu nilikuwa napitia gazeti la CCM na nimeshengazwa na kukutana na kichwa cha habari kwamba tovuti yao imechakachuliwa na wahuni na waliofanikiwa kuendesha KURA YA MAONI ya URAIS wa JMT ambapo Dr. Slaa ameibuka mshindi.

  Kwakweli hali si nzuri na jamaa wanajaribukujikosha ili kibarua chao kisiote nyasi. Naamini kabisa ni wao wenyewe ndio walioendesha hiyo poll na wakadhani wapenzi wa CCM watawapiga tafu ilikupata matokeo wanayoyataka wao. Kipigo walichopata ni kielelezo tosha kwamba watanzania wamechoka na ubabaishaji wa CCM na mwaka huu lazima kieleweke!!:loco:

  Chanzo hapa chini:

  Tovuti ya Uhuru yachakachuliwa
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tovuti ya Uhuru yachakachuliwa

  Tuesday, 05 October 2010 21:01
  NA MWANDISHI WETU

  WAHUNI wameingilia tovuti ya magazeti ya Kampuni ya Uhuru Publications LTD (UPL) na kuendesha utoaji maoni yanayodaiwa kutoka kwa wananchi, juu ya hali ya kisiasa nchini wakilenga kuhoji utendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika utoaji huo wa maoni, wahuni hao wa kisiasa wamepanga kuonyesha utendaji wa serikali si mzuri, na kwamba inahitaji yafanyike mabadiliko, wakilenga kuwalaghai wananchi washawishike kupiga kura za kuikataa serikali ya CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.

  Kitendo hicho cha kuchakachua tovuti ya gazeti la Uhuru, kimefanywa kwa makusudi wakidhani wakitumia gazeti hili ambalo wanatambua uhusiano wake na Chama kilichopo madarakani na serikali zake, wataweza kuwayumbisha Watanzania wengi, kwa kuwafanya waamini ghilba hizo za kisiasa, ili wabadili msimamo na kuunga mkono upinzani, hususan chama cha CHADEMA. Wahuni hao wamefanya hivyo wakitambua Chama Cha Mapinduzi ndicho chenye nguvu kubwa nchini, kina hakika ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao, na hakuna namna yoyote ya kukizuia kuendelea kuunda serikali, ndipo walipobuni mbinu hiyo chafu kwa kupitia tovuti ya gazeti hili ili waweze kuaminika.

  Gazeti la Uhuru halijawahi kujihusisha na kura yoyote ya maoni yenye kutaka kuonyesha maoni ya watu juu ya hali ya kisiasa nchini, au kuhoji juu ya utendaji wa serikali, kama ilivyoonyeshwa na wahuni hao. Baada ya uchakachuaji wa maoni hayo na kuwekwa kwenye tovuti ya gazeti hili, na kuonyeshwa pia katika mtandao wa 'bidii forum', baadhi ya magazeti yameyachangamkia kwa nia ya kutaka kuyachapisha matokeo hayo.

  Mhariri Mtendaji wa magazeti haya, Josiah Mufungo, alisema jana kuwa mchakato mzima wa maoni hayo hauhusiki na gazeti la Uhuru, kwani huo si utaratibu wake na halina utaratibu wa aina hiyo, ila huo ni usanii wa kisiasa unaopikwa kwa nia ya kuwababaisha Watanzania juu ya imani yao kwa Chama Cha Mapinduzi na serikali zake za Jamhuri ya Muungano, na ya Mapinduzi Zanzibar. Amewataka wananchi kupuuza kinachodaiwa kuwa 'matokeo' ya maoni hayo, ambayo wahuni hao wanataka kuyaonyesha kuwa yametolewa kupitia gazeti hili.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Huo upumbavu utamwambia mtu aiyejua IT pekee akakuelewa.

  Nani anaweza kuweka entry kwenye website ya watu bila kuwa na credentials au access rights? Ni wao wenyewe wameweka na wameumbuka.

  Mimi binafsi nisikuwahi kujua kama kuna website ya Uhuru

  Hivi hawa CCM wana akili nzuri kweli?
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  CCM IMEKUFA RASMI.
  SALAMU ZA RAMBI RAMBI ZIMFIKIE MALARIA SUGU NA KUNDI LAKE LA WAPIGA KAMPENI.:whoo::hail::A S-rap::pound::closed_2:
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hawa jamaa walidhani utani naona wakajaribu kuweka kura za maoni, hatima yake ikawa DR. wetu akambwaga huyo Mkwere sasa wanamashaka na kibarua chao ndo maana wanasingizia hacker! hahaha jamani mbna mnakuwa kama watoto? acheni ukweli uchukue nafasi yake!
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ayaaa kivipi sasa?? inawezekanaje watu wakachakachua mi mwenyewe nimeona jana tuu leo wanasema hivyo, haaa muda woote mpaka watu wanapiga kura hawakuona haingiingiii akilini kabisaa. Sijui labda watu wa IT watusaidie kwa hili. kumbe inawezekana kuchakachuliwa?? NAOMBA MSAADA KWA WATAAALAMU WA IT KWA HILI.
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Siku za CCM madarakani sasa zahesabika zimebaki siku 24 tu. Papara zao kamwe safari hii hazitazaa matunda. Uhuru wangependa watu waseme wanaridhika na utawala uliopo lakini raia wao wanasema kweli tu na kwa vile majibu hayo hawayataki ndio maana wanajikosha.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Bila kumsahau Maggid!!!
   
 9. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hii kali mhuni ajijui kama yeye ni mhuni! Nijuawavyo website, kwanza inakuwa na 'master' na 'content manager'. Sasa siku zote hizo hawa jamaa wawili walikuwa wapi mpaka maoni yanaendeshwa na majibu kupatikana? Pili, websites nyingi sasa hivi zinaandikwa kwa kutumia 'content management system' ambayo inamtaka mtu ambaye anataka kubadilisha content awe na access permission/ login details. Hivyo ni nyinyi wenyewe Uhuru mmefanya mambo hayo wala si Chadema wala nani. Kama waliofanya kitu hicho ni wahuni basi ni nyie wenyewe. Na taarifa yenu ingekuwa nzuri kama mngesema 'tunahujumiana wenyewe' lakini matokeo yanatoa picha halisi ya maoni ya wananchi.

  Website inaweza kuwa 'hacked' kama ilivyokuwa ile ya Bunge kwa maana ya kutumia domain name kuweka content nyingine. Je, ya kwenu imekuwa 'hacked'? Sasa mnataka kusema Chadema wameandika kirusi ambacho kimeweza kuingia kwenye computer system zenu na kutoa data za permission? Kama ndio ni ujinga wenu wa kutokuwa na current 'anti-virus' software! Kwanza mmejuaje kama ni Chadema?

  Kuonyesha kuwa website yenu ilikuwa-hacked basi wekeni tena hiyo poll ilituone matokeo kama yatakuwa na tofauti na yale ya mwanzo. Wenzenu Daily News waliweka na kutoa kimya kimya baada ya kuona Dr. Slaa anaongoza na baadaye kusema hawezi kuwa Rais yaani wakibishia poll walioweka wenyewe!

  Kwa kifupi CCM wanataka kuhalalisha wizi wa kura Okt 31 2010. Wamechelewa!!!
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Subutu!!
   
 11. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  LAST TIME I CHECKED KWENYE TOVUTI YA UHURU HALI ILIKUWA HIVI....

  Inahitaji uongozi Mpya 106 37.5%
  Ni Ubabaishaji 67 23.7%
  Katiba Irekebishwe 39 13.8%
  Inaridhisha 31 11%
  Inahitaji Kuboreshwa 26 9.2%
  Hairidhishi kabisa 14 4.9%

  Number of Voters : 283 First Vote : Wednesday, 10 February 2010 13:38 Last Vote : Tuesday, 05 October 2010 15:37
   
 12. M

  Miruko Senior Member

  #12
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hatudanganyiki. Hakuna cha kuchakachuliwa. Mimi nilipoona matokeo hayo, nilijua yataondolewa kwa vizingizio. Niliamua kuyanakili ili kubaki na ukweli wake. Poll hiyo iliwekwa kwenye website hiyo tangu saa 7: 30 mchana Februari 10, 2010 na kura ya mwisho ilipigwa jana October 5, 2010 saa 9:14. Muda wote huo kama website ilikuwa imechakachuliwa ingeshajulikana na kurekebishwa. Narudia: Hatudanganyiki.

  Mambo yalikuwa hivi:

  Hali ya Kisiasa Tanzania

  Inahitaji uongozi Mpya
  103 37.1%

  Ni Ubabaishaji
  67 24.1%

  Katiba Irekebishwe
  38 13.7%

  Inaridhisha
  30 10.8%

  Inahitaji Kuboreshwa
  26 9.4%

  Hairidhishi kabisa
  14 5%

  Number of Voters : 278
  First Vote : Wednesday, 10 February 2010 13:38
  Last Vote : Tuesday, 05 October 2010 15:14
   
 13. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #13
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  wakati tunaanzisha blogu ya friendsofslaa.blogspot.com hii ilivamiwa na kufungwa kwa dakika chache tu toka kuanzishwa na kufungua nyingine Friends of Slaa | FOS | na kuanza kuandika makala kwenye magazeti kadhaa kuhusu dhihaka na dharau nyingine lakini ilirudi hewani baada ya masaa machache na kwa kweli nimeshatoa malalakiko kwa blogger wanayafanyia kazi huku kuruhusu blogu hizo zote mbili kufanya kazi .

  hata wao wana uwezo wa kushitaki kwa sababu tuna vyombo vyetu vya kushugulikia mambo hayo uziri wa IT mengi yapo hauhitaji mganga au utabiri
   
Loading...