Ni Kweli "Tiles" zinazotengenezwa hapa Tanzania hazina square?

Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
3,156
5,652
Nimekuwa na Tatizo la kuona kila niki weka tiles, zinapishana. Mara nyingi na nunuaga tiles za makampuni ya hapa nyumbani Tz, kwa sababu ya Urahisi, lakini pia kuinua viwanda vya ndani.

Ila mara zote naona mistari haija nyooka, mara zote nikiwauliza mafundi wananiambia tiles za kichina na za Tanzania zinapishana. Sasa najiuliza je hii ni kweli?

Na sababu inakuwa nini? Maana nilidhani tiles zinatengenezwa kwa frame maalumu ambayo ina vipimo sawa. Hebu watalaamu wetu mtusaidie ukweli wa hili.
 
Sina uhakika. Ila nikiwa saidia fundi wa tiles na block tulikua tunafuata tiles na gypsum kiwanda kinaitwa Good One maeneo ya Ilala.

Hiko kipo ndani ya Tz na tulifanya kazi vizuri tu sijawahi kuona hivyo.

Pia kuna wachina wapo Makumbusho yaani wazia nyumba ya mtu ila iwe kiwanda kidogo cha tiles. Sasa kama wale tiles zao zilikua sawa tu sioni kivipi kwingine zisiwe sawa.
 
Ni kweli ,tiles ambazo hazina kasoro ni za spain tu,na bei yake imesimama hatari.nyingine zina kawaida ya kupishana ukubwa 1inch.

Sasa kabla ya kuanza kuweka tiles ni vyema fundi kutoa tiles moja kwa kila boksi kisha kutenganisha boksi zenye tiles zilizozidi ukubwa,na zile zilizopungua ukubwa,(huwa ni kidogo sana).

Kisha fundi aanze na zile tiles ndogo kwa kutumia spacer kwenye mistari.zikiisha ndio atumie zile kubwa bila spacer.

Matokeo huwa yana nafuu na mistari kunyooka ingawa mingine itakuwa mipana kidogo (yenye spacer),na mingine itakuwa mwembamba(isiyo na spacer).

Ni changamoto sana kwa mafundi kuweka hizo tiles za bei nafuu.hayo ndio maujanja ya kuweka hizo tiles.

Huwa hazipishani squre(zile kona nne),zinapisha upana/urefu.
 
Nimekuwa na Tatizo la kuona kila niki weka tiles, zinapishana. Mara nyingi na nunuaga tiles za makampuni ya hapa nyumbani Tz, kwa sababu ya Urahisi, lakini pia kuinua viwanda vya ndani.

Ila mara zote naona mistari haija nyooka, mara zote nikiwauliza mafundi wananiambia tiles za kichina na za Tanzania zinapishana. Sasa najiuliza je hii ni kweli?

Na sababu inakuwa nini? Maana nilidhani tiles zinatengenezwa kwa frame maalumu ambayo ina vipimo sawa. Hebu watalaamu wetu mtusaidie ukweli wa hili.
Fundi kakupindishia nyumba yako.
Nyumba yako, yaani kila chumba hakina mita za mraba kamili. Kuna error ya zaidi ya 1%.
 
Kwa kawaida unaposeti tiles vipande huwa vinakaa pembeni ukutani,na vinakatwa kulingana na sakafu umekaaje,sidhani kama kuna uhusiano na kunyoosha au kupindisha mistari,tiles unaweza kuzi shape kulingana na eneo unalozibandika.

Nadhani tatizo analoongelea mtoa mada ni namna ya kuweka mlolongo wa tiles na tiles, hapa ukiangalia utagundua tu makosa baada ya fundi kuweka mistari miwili tu,si lazima nyumba nzima.
 
Ni kweli ,tiles ambazo hazina kasoro ni za spain tu,na bei yake imesimama hatari.nyingine zina kawaida ya kupishana ukubwa 1inch.

Sasa kabla ya kuanza kuweka tiles ni vyema fundi kutoa tiles moja kwa kila boksi kisha kutenganisha boksi zenye tiles zilizozidi ukubwa,na zile zilizopungua ukubwa,(huwa ni kidogo sana).

Kisha fundi aanze na zile tiles ndogo kwa kutumia spacer kwenye mistari.zikiisha ndio atumie zile kubwa bila spacer.

Matokeo huwa yana nafuu na mistari kunyooka ingawa mingine itakuwa mipana kidogo (yenye spacer),na mingine itakuwa mwembamba(isiyo na spacer).

Ni changamoto sana kwa mafundi kuweka hizo tiles za bei nafuu.hayo ndio maujanja ya kuweka hizo tiles.

Huwa hazipishani squre(zile kona nne),zinapisha upana/urefu.
Hizo spacer baada ya kumaliza kazi huwa mnazitoa au zinabaki hapo hapo?
 
Kwa kawaida unaposeti tiles vipande huwa vinakaa pembeni ukutani,na vinakatwa kulingana na sakafu umekaaje,sidhani kama kuna uhusiano na kunyoosha au kupindisha mistari,tiles unaweza kuzi shape kulingana na eneo unalozibandika.

Nadhani tatizo analoongelea mtoa mada ni namna ya kuweka mlolongo wa tiles na tiles, hapa ukiangalia utagundua tu makosa baada ya fundi kuweka mistari miwili tu,si lazima nyumba nzima.
Ukiweka tiles nyumba nyingi ambazo zimejengwa enzi za mkoloni, kama tiles hizo siyo pieces kubwa, huwa zina fit na kama hazifit, huwezi kuona tile yoyote ambayo haipo straight. Na kama zipo zimekatwa basi zote pembezoni zitakuwa na shape ileile.

Neno linaloleta maana nzima ya mada ni "kupishana". Kwanini zipishane kama chumba kipo straight kila corner?

Mimi siyo mjenzi ila nimegundua hili nilipojengewa na fundi wa mtaani. Tiles ilibidi zichongwe na nilipouliza wataalam wa ujenzi, hilo ndio jibu nililopewa na kwangu lilileta maana.

Jaribu siku moja kuweka tiles nyumba za mkoloni, mfano zile za chang'ombe uhindini.
 
Yaani akajaribu tu kuweka tiles kwenye nyumba za watu!!
 
1605010118966.png
 
Ukiweka tiles nyumba nyingi ambazo zimejengwa enzi za mkoloni, kama tiles hizo siyo pieces kubwa, huwa zina fit na kama hazifit, huwezi kuona tile yoyote ambayo haipo straight. Na kama zipo zimekatwa basi zote pembezoni zitakuwa na shape ileile.

Neno linaloleta maana nzima ya mada ni "kupishana". Kwanini zipishane kama chumba kipo straight kila corner?

Mimi siyo mjenzi ila nimegundua hili nilipojengewa na fundi wa mtaani. Tiles ilibidi zichongwe na nilipouliza wataalam wa ujenzi, hilo ndio jibu nililopewa na kwangu lilileta maana.

Jaribu siku moja kuweka tiles nyumba za mkoloni, mfano zile za chang'ombe uhindini.
Kwanini zipishane wakati chumba kipo straight?

Mkuu hii ni kazi ya kiwanda sio ya fundi?hii ni changamoto sana ,ukinunua tiles box 50,cha kufanya huwa tunatoa piece moja kila box kisha tunalinganisha,lazima utakuta zina makundi mawili,zilizopungua kidogo na zilizozidi kidogo.tiles za kibongo na kichina ,huwa hazilingani zote,hata zikiwa za aina moja.

Hilo la vipande vyote kuwa sawa sidhani kama ni 100%,tofauti lazima iwepo hata kidogo tu,na ndo sababu ya kuviweka ukutani hivyo vipande,ili kuvi shape.
 
Nimekuwa na Tatizo la kuona kila niki weka tiles, zinapishana. Mara nyingi na nunuaga tiles za makampuni ya hapa nyumbani Tz, kwa sababu ya Urahisi, lakini pia kuinua viwanda vya ndani.

Ila mara zote naona mistari haija nyooka, mara zote nikiwauliza mafundi wananiambia tiles za kichina na za Tanzania zinapishana. Sasa najiuliza je hii ni kweli?

Na sababu inakuwa nini? Maana nilidhani tiles zinatengenezwa kwa frame maalumu ambayo ina vipimo sawa. Hebu watalaamu wetu mtusaidie ukweli wa hili.
Unatumia tiles za kampuni gani ambazo zinakupa changamoto ya square?
 
Hapa anamaanisha kupishana Kwa tiles zenyewe
Kipimo kimetajwa 40*40 ila unakuta mwenye mzigo huohuo unakuta kipimo cha 40*40.1
Kwa kawaida unaposeti tiles vipande huwa vinakaa pembeni ukutani,na vinakatwa kulingana na sakafu umekaaje,sidhani kama kuna uhusiano na kunyoosha au kupindisha mistari,tiles unaweza kuzi shape kulingana na eneo unalozibandika.

Nadhani tatizo analoongelea mtoa mada ni namna ya kuweka mlolongo wa tiles na tiles, hapa ukiangalia utagundua tu makosa baada ya fundi kuweka mistari miwili tu,si lazima nyumba nzima.
 
Nimewahi kushuhudia hili---ni kweli tiles za TZ zinapishana size.Fundi mjanja anagundua na kuzitumia kwenye sehemu ya vipande.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom