Ni kweli Sugu kataka wawakatae hata kwa mawe viongozi wabovu?

Nilikua ndani,mwenye radio yuko nje sijajua ni redio gani,..
ila kaongelea mda mrefu habari ya sugu na uhamasishaji wake
Eti ulikuwa ndani hujui ni redio gani, kama wewe mwenyewe unaona aibu kutaja source huoni kuwa kuna walakini na habari yenyewe.
 
wewe unataka gazeti gani liandike ili ujue kama ni tatizo? Mtu anapochemka kwenye masuala ya msingi anatakiwa kusemwa ili asirudie kwani ni aibu kubwa kwa mbunge kunena hayo. Niliwahi sikia mtu akivuta bangi hata akiacha ile athari humtoka baada ya miaka 40.kwahiyo asiwe alipanda jukwaani akiwa amesha pandisha mzuka. maana siamini kama mtu mzima wa akili anaweza kuongea hayo mbele ya wapiga kura wake.Ivi anadhani wapiga kura ni mazuzu?mara nyingi ukiwa pale jukwaani ongea uwezavyo lakini ukitoka pale ujue ima umejijenga au umejibomoa kwani wanachi watabaki wanayajadili maneno yako na kujua kama unawafaa kwa maendeleo au la

Mkuu vp kuhusu kutaja hicho chanzo cha habari yako. Mbona unazunguka na maneno mengi Mkuu? Tutajie chanzo ili tuchangie kwa uhakika.
 
vibaka = majambazi= wezi= wanyang'anyi= majangiri= mafisadi= magamba

kama anavyofanywa kibaka basi sio tatizo kama hatua hizo hizo zitachukulia kwa wote hapo juu, wala huu sio uchonganishi au kuvunza amani, mbona vibaka wanachomwa moto kila siku huku mafisadi wakishangilia kwa kukwapua mahela B.O.T,
Kama sugu kasema hivyo basi mafisadi wasiende mbeya na kama wataenda na ieleweke kwamba hiyo ni sawa na kuingiza mbwa msikitini lazima chamoto utakiona.
lakini pia taarifa inasema kama hawawapendi sugu hakusema kila mtu apingwe mawe ila wasiopendwa, mimi ni hakika wanajijua wote maana wana magamba,
kwa hivyo na wao wasilazimishwe kupendwa walipewa miaka 49 ya utawala walimeshindwa kuonyesha upendo ila wizi na matusi kwa wananchi,
kwa kweli mawe ni haki yao hakuna aliyewalazimi kutuibia.
mbaya zaidi baadhi ya yao hao mafisadi DINI/asili yao inaruhusu kupiga mawe MWIZI
 
Kama ni kweli sugu katamka maneno hayo viongozi wa juu wa CDM wanapaswa kumkanya kumpa adhabu maana anakiweka chama pabaya. Ni kauli mbovu ambazo hata wana chadema hawawezi kuzifurahia.
 
Ni kweli ameyasema haya, na ni makosa makubwa sana kwake kisiasa....tatizo ameshindwa kutofautisha ethics za Bongo Fleva na Ubunge..mwenyekiti alifanya kazi ya ku-qualify statements za Sugu palepale jukwaani..ilikua ni aibu sana aiseee..
 
kwa wakati huu mi naona wabondwe mawe tu...na ikibidi hata mapana wacharazwe,sio watu wa kuwaonea huruma wahujumu uchumi...na sugu nae akiboronga acharazwe mapanga,hadi kieleweke.The leaders need to serve the people and not their stomach and family.

Mkuu hii safi sana, na sugu mwenyewe ajue kuwa akiboronga atapigwa mawe pia!!
 
sugu uwezo wake ni miziki ya kufokafoka na sio siasa, hata hivo sugu kushinda ccm walimpambanisha na mtu aliyekuwa hakubaliki ndani ya ccm yenyewe. Nilisha wahi changia kuwa Sugu uchaguzi ujao hawezi shinda tena, kwani uwezo wake ni mfinyu mno.Maneno aliyoyaongea ni kama tulivosikia na mara baada ya yeye kuchemka Slaa na Mbowe wakaona aibu na mbowe pale pale akasimama na kumkosoa vikari kwa upupu aliouongea,yaani anazidi kujizika yeye mwenyewe.waswahili tunasema mazoea hujenga tabia, sugu alizoea toka akiwa mwana muziki katika majukwaa ni kuimba miziki ya kupaka(kutukana,kujisifu ...) kwahiyo nawashauri viongozi wa chadema watu kama hao musiwape nafasi ya kusimama kwenye majukwaa.
Acha wivu wa kike wewe... Sugu alipata kura 48,000 na kumuacha mpinzani wake kwa kura 27,000. Sio ushindi wa kubeza hata kidogo na hapo uchakachuaji ulifanyika. Kura za sugu ni nyingi kuliko za wabunge wote wa CCM Zanzibar ukizijumlisha kwa hiyo sio wa kubahatisha kama akili yako mbovu inavyokudanganya. Suala la kuelezea hisia halizingatii kuwa watu kama wewe watafurahia au la, kama kiongozi hamumpendi mzomeeni tu, na hao viongozi tusiowataka wakija Mbeya tunawazomea vilevile. Mbona hata Slaa alizomewa na mujahidina pale Tabora, kwani kuna mtu alilalamika? Watu walikuwa wanatoa hisia zao za kiislam
 
Kama ni kweli kasema aonywe,Kama ni uongo viongozi Chadema fuatilieni hili sivyo mtachafuka
 
Wheather amesema au hajasema -lazima tuanze kubadilika naona speaker umelishikia bango saana suala hili thread nzima ni wewe -hawa mafisadi hawastaili kupigwa mawe tu wanastaili kupelekwa mahakamani wawajibishwe lakini kwa kuwa wamechakachuwa mpaka huo mkondo njia rahisi ni wananchi kuwakataaaa na kuwaambia hutuwataki mnatunyonya, mnatukandamiiza na mnatufanyahali zetu za maisha kuwa ngumu saana. Sugu sio mnafiki -nchi hii inaporomoka shimoni kwa sababu ya unafiki unafiki unafiki uliopitiliza, wewe unajua hawa ni mafisadi na ndio wanaotupeleka shimoni halafu unasema wabembelelezwe mpaka lini?????? tuache unafiki jamani utatua ----big up Sugu songa mbele -vita ya kulikomboa taifa toka kwa mafosadi sio lelemamama lazima tutambue.
 
Kama vyombo vya usalama kama polisi na takukuru wameshindwa kawachukulia hatua wezi/majambazi/mafisadi sisi tufanyeje !!?
 
Hii Kauli ya sugu haijakaa vizuri But ni hisia wanazo wengi sababu ya kuonekana serikali haichukui hatua.

Sasa juzi juzi juzi nimesikia DPP anaomba wananchi wenye ushaidi wa KAGODA waende wapeleke ushaidi. Kauli hii ilinitia kichefu chefu. Na ni vitu kama hivi vinaweza kuyapa uhaali matamshi kam ya kina SUGU.

Sio siri wananchi wengi tunawaponda mawe kina chenge, Lowasa RA kwa maneno hata hapa Jf tunawaponda sana mawe kidiplomasia but as time goes on kama ndio style za kina DPP kutosoma upepo mhhhhh mawe halisi yatarushwa. japo siungi mkono but sitashangaaa.


Yaani DPP anakosa kutafutaushaidi wa Kagoda anaomba msaada wa wananchi. Ni kama yeye kishajionyesha yuo upande wa mafisadi
. Narudia tena though siungi mkono kauli hiyo ya sugu sometime its disgusting
 
itakuwa njia nzuri ya kurudisha hizo hela na kujitakasa mapema mbele ya umma.
wakijua kuwa wananchi wanawajua na wanachukia ufisadi wao hakuna
atakaethubutu kupita mtaani kwa amani wataogopa na hao ndio wanasababaisha maisha kuwa magumu,
majambazi kuwa wengi kila uchao na maisha ya mtanzania yanazidi kuwa magumu..
 
Bush alipigwa na kiatu usoni iraq kwa sababu ya ujinga wake. mi sioni cha ajabu kupigwa mawe. kama hawatendi waliyotumwa na wananchi wapigwe mawe wafie mbali. Bukoba tarehe 6/5 wameanza kwa sababu ya ujinga wa viongozi wetu. watumwa na wananchi kuchapa kazi wanasubili posho tu za vikao. matatizo lukuki yanatusonga hawayaoni.
 
hivi ukimuona mtu kama Rostam Aziz barabarani unategemea umpigie makofi..watanzania tuache unafiki kama mama, dada, baba au ndugu yako yoyote angesha kufa kwa kukosa huduma hospitali ungejiuliza ni kwanini na ukipata jibu mafisadi ungetamani kuwapiga mishale siyo mawe tu
 
Mimi kwa sasa niko Mbeya, na bahati nzuri nilikuwepo uwanjani. Ni kweli nilimsikia Sugu akisema mafisadi wapondwe mawe. Mwanzoni nilihisi anasema kinadharia, lakini baadaye ikaonesha kama kweli ni mawe halisia, kwa kuwa hakufafanua nadharia niliyodhani, na watu wote tumetoka viwanja vya Ruanda Nzovwe tukijua tuwaponde mawe mafisadi. Sentensi ya mwisho ya salamu zake, Sugu alisisitiza tena kwamba mafisadi wapondwe mawe na hasa Mwanjelwa (Kkoo ya Mbeya). Sitaki mafisadi, ila pale Sugu alinichefua. Inakuwa kama siasa za kihuni. Bahati mbaya haikufafanuliwa na viongozi waandamizi waliomfuatia kutoa nasaha zao. Heri angesema wazomee tu. Wanasiasa wanatakiwa kuwa makini sana na maneno wayasemayo, kwani ama yatawabomoa wao mbele za uso wa jamii au yawabomoe wananchi.
Wewe hukuwepo uwanjani vinginevyo ungekiri kwamba Mh Mbowe alifafanua maana ya kupiga mawe kuwa ni kususia mambo yanayofanywa na mafisadi. Hata Sugu mwenyewe alifafanua kwamba kupiga mawe ni kutokwenda kwenye matamasha ya wasanii mafisadi, mikutano yao na hata magazeti yao ni kususia. Sugu aliongea kisanii lakini Mbowe alifafanua kirefu sana tena kwa kina. Tuache ushabiki
 
Mleta mada kasikia mtu anapita na redio nje,ikasema maneno ayo,mleta hoja kakaa kaandika mada! Kazi ipo! Fuatilia ujumbe mzima jaman,aya great thinkers.
 
Nimesikia kwenye habari za magazetini asubuhi
hii kwamba mbunge wa mbeya mjini
ame hamasisha wana nchi wa mbeya kwamba
akija kiongozi ambaye hawamtaki,...
au kiongozi yeyote,hata kama "ni raisi" ni haki yao kumkataa
haka kwa kumpiga mawe!

Kama hii ni kweli,basi Dr.Slaa na wazee wengine ndani ya chadema
mna kazi ya kuwafundisha wabunge vijana
jinsi ya kuongea kwenye public na jinsi ya kutembea "normal" ukiwa na uheshimiwa!

Hizi sio kauli za kutolewa na kiongozi yeyote yule,...
kuna watu walio kuwa wanataka kujiunga na chadema,au walio
muunga mkono sugu,..na ambao ni wastaarabu watakua hawaja furahiswa na
kauli hii,...

na hao wataendelea kuamini kuwa chadema wana hamasisha vurugu!

Ombi:
Naomba viongozi wa chadema,walioko huko kwenye maandamano
wakanushe maneno haya (kama sio kweli kwamba sugu haku yatamka)
maana naamini kila alosikia habari hii kasikitishwa sana,...

kama ni hayo magazeti na wasipo kanusha haitakua na impact au?

Ivi kweli kuna mtu atachagua ufisadi over comments za namna hii? Huyo mtu atakuwa mjinga kupita kiasi! Yani kweli kuna mtu mwenye akili timamu anasema ni bora niibiwe hela kuliko kuchagua mtu anayetoa comments za namna hii?
Sidhani...
 
CCM wakiendelea hivi watapigwa mawe tu!! Watu hawana cha kupoteza kwa sasa...revolution sio tamu hata kidogo, angalia French revolution, Romania, n.k.

You mess with people's lives they deal with you there and then!! Na wakijua kuwa wanapondwa mawe they will begin to change, lakini wakiiba na kupigiwa makofi hawataacha hawa!!
 
Back
Top Bottom