Ni kweli Sugu kataka wawakatae hata kwa mawe viongozi wabovu?

Ukweli utabaki palepale kwamba wabunge wa cdm wakikosea tuseme ili wajirekebisha kwakuwa tuna malengo ya mbali na si hii miaka mitano waliyoipata sasa. Haijalishi alisema au hakusema ila muanzisha thread kasema amesikia kwenye radio na kama ndivyo tunaomba ikemewe na kama sivyo ikanushwe hakuna sababu ya kujua ni gazeti lipi ilimradi imeingia kwa jamii tuifanyie kazi hiyo ndio siasa
 
Mimi kwa sasa niko Mbeya, na bahati nzuri nilikuwepo uwanjani. Ni kweli nilimsikia Sugu akisema mafisadi wapondwe mawe. Mwanzoni nilihisi anasema kinadharia, lakini baadaye ikaonesha kama kweli ni mawe halisia, kwa kuwa hakufafanua nadharia niliyodhani, na watu wote tumetoka viwanja vya Ruanda Nzovwe tukijua tuwaponde mawe mafisadi. Sentensi ya mwisho ya salamu zake, Sugu alisisitiza tena kwamba mafisadi wapondwe mawe na hasa Mwanjelwa (Kkoo ya Mbeya). Sitaki mafisadi, ila pale Sugu alinichefua. Inakuwa kama siasa za kihuni. Bahati mbaya haikufafanuliwa na viongozi waandamizi waliomfuatia kutoa nasaha zao. Heri angesema wazomee tu. Wanasiasa wanatakiwa kuwa makini sana na maneno wayasemayo, kwani ama yatawabomoa wao mbele za uso wa jamii au yawabomoe wananchi.
 
Gazeti lililoandika habari hiyo ni Mzalendo. Ulitegemea kuipata habari hiyo kwenye gazeti gani kama si Mzalendo/Uhuru?
 
hata wavuta bangi wanapewa ubunge Tanzania. CDM ndio mnataka ishike nchi? Watashika wapi kama wabunge wenyewe ndio hawa kina sugu.
 
Mwizi ni adui mkubwa sana wa maendeleo yetu,tunajitahidi kujikwamua kutoka kwenye hali ngumu,mwisho nguvu zetu zote zinaishia kwenye mifuko ya wachache,tunalia hali ngumu wao wanatusanifu sasa tufanyeje jamani,
dawa ya mwizi ni................................
 
Mimi kwa sasa niko Mbeya, na bahati nzuri nilikuwepo uwanjani. Ni kweli nilimsikia Sugu akisema mafisadi wapondwe mawe. Mwanzoni nilihisi anasema kinadharia, lakini baadaye ikaonesha kama kweli ni mawe halisia, kwa kuwa hakufafanua nadharia niliyodhani, na watu wote tumetoka viwanja vya Ruanda Nzovwe tukijua tuwaponde mawe mafisadi. Sentensi ya mwisho ya salamu zake, Sugu alisisitiza tena kwamba mafisadi wapondwe mawe na hasa Mwanjelwa (Kkoo ya Mbeya). Sitaki mafisadi, ila pale Sugu alinichefua. Inakuwa kama siasa za kihuni. Bahati mbaya haikufafanuliwa na viongozi waandamizi waliomfuatia kutoa nasaha zao. Heri angesema wazomee tu. Wanasiasa wanatakiwa kuwa makini sana na maneno wayasemayo, kwani ama yatawabomoa wao mbele za uso wa jamii au yawabomoe wananchi.
Too sad indeed, nakumbuka Mkapa aliita wapinzani kokoto na ilinikera, basi na hii imenikera!!
 
Gazeti lililoandika habari hiyo ni Mzalendo. Ulitegemea kuipata habari hiyo kwenye gazeti gani kama si Mzalendo/Uhuru?
Sawa,haijalishi imeandikwa na gazeti gani,cha muhimu ni ukweli wa hoja yenyewe,
huyu hapa shahidi alokua uwanjani

Mimi kwa sasa niko Mbeya, na bahati nzuri nilikuwepo uwanjani. Ni kweli nilimsikia Sugu akisema mafisadi wapondwe mawe. Mwanzoni nilihisi anasema kinadharia, lakini baadaye ikaonesha kama kweli ni mawe halisia, kwa kuwa hakufafanua nadharia niliyodhani, na watu wote tumetoka viwanja vya Ruanda Nzovwe tukijua tuwaponde mawe mafisadi. Sentensi ya mwisho ya salamu zake, Sugu alisisitiza tena kwamba mafisadi wapondwe mawe na hasa Mwanjelwa (Kkoo ya Mbeya). Sitaki mafisadi, ila pale Sugu alinichefua. Inakuwa kama siasa za kihuni. Bahati mbaya haikufafanuliwa na viongozi waandamizi waliomfuatia kutoa nasaha zao. Heri angesema wazomee tu. Wanasiasa wanatakiwa kuwa makini sana na maneno wayasemayo, kwani ama yatawabomoa wao mbele za uso wa jamii au yawabomoe wananchi.

Cha muhimu ni huyu sugu kugundua madudu alo ongea na kujirekebisha!
Siipendi ccm,lakini kwa style hii,hata wanao ona kauli za makada wa ccm ni za ajabu wataanza
kuwaamini
 
Too sad indeed, nakumbuka Mkapa aliita wapinzani kokoto na ilinikera, basi na hii imenikera!!

kumbe na mkapa yume eh?

hata wavuta bangi wanapewa ubunge Tanzania. CDM ndio mnataka ishike nchi? Watashika wapi kama wabunge wenyewe ndio hawa kina sugu.

Omr,na mkapa utamuitaje kwa kutoa matusi kwa wapinzani?
 
Kama kasema kuwapiga mawe mafisadi mi naona km hajakosea hv!labda angesema viongozi wote wa serikari.Hebu fikiria km mapacha watatu wamesababisha vifo na mateso ya watu wangapi kwa kukwapua pesa iliyotakiwa kwenda ktk huduma za kijamii?
 
Una kumbuka Pinda aliwahi kulia bungeni 29 januari 2009?
unajua ni kwanini?

Yule mbunge wa CCM B alimuuliza kuhusiana na utata wa kauli yake
kuwa wauaji wa ma-albino wauawe pia,...ilikua kinyume na haki za nini sijui.......

Kila mtu ana haki ya kuishi,kusema wapondwe mawe bado ni kosa
ambalo wataalam wakili valia njuga sugu anaweza kulia kama pinda!

kasome hapa: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=1971
 
mbona vibaka wanaoiba kuku wanapigwa mpaka kufa. Cha ajabu nn mafisadi wanaoangamiza taifa kupigwa mawe?
 
Kwa hili Sugu inabidi aombe radhi...
Ni kweli sugu alisema maneno hayo, ila yupo sahihi kwakuwa mwizi siku zote ni adui na hafahai kwenye jamii na wote aliyo wataka wapigwe mawe ni mafisadi na hawafai, pli wanambeya wenyewe walikuwa wakiimba kabla hata ya sugu hajaongea, kwa mf: kikwete usije mbeya , kama siyo usenge wako kikwete na mafisadi wangetoka wapi, shitambala ameolewa, sasa kwa haya ulitegemea sugu akae kimya asiwaunge wananchi wake mkono?
 
Chadema ni chama cha wahuni, wavuta bangi, wachukua wake za watu, wapayukwaji na viongozi wenye kutanguliza nafsi zao kwanza kuliko maslahi ya taifa na wanachama wao

sishangai hata kidogo kwa wabunge wa chadema kufanya hayo
 
Kuna kauli alitoa sugu mby jana, ya kutaka mafisadi wapigwe mawe, watu wengi wanailalamikia, kisa sio sahii, lakini watu hao hao hakuna analayelalamika vibaka wanapochomwa moto, kisa kaiba cmu na kuku kutokana na ugumu wa maisha unaosababishwa na hao mafisadi. Na wakumbuke kuwa china mafisadi wananyongwa. Mafisadi kupigwa mawe ni kosa, ila wezi wa kuku sawa. Yangu macho
 
Sugu ameongea lugha ninayoiamini, hatuwezi kuwaandalia sherehe wezi wa mali ya umma kwa kuwa tu wanapitishwa na misafara mikubwa. Mwizi ni mwizi tu na kwa kuwa tumekuwa na mfumo corrupt kwa sasa hili ndo jibu pekee wale wanaoitwa 'watanzania wa kawaida' wanapaswa kufundishwa kulifanywa, uasi wenye sababu unakuwa na maana kubwa kwa wanaoumizwa.
ANTIVIRUS inakwenda mbali zaidi ya yaliyoimbwa
 
We need source of the information kama source ni gazeti la uhuru, mzalendo ama habari leo tutaelewa hizo ni propaganda za CCM we need a reliable source otherwise zipotezee kiutu uzima.
 
Chadema ni chama cha wahuni, wavuta bangi, wachukua wake za watu, wapayukwaji na viongozi wenye kutanguliza nafsi zao kwanza kuliko maslahi ya taifa na wanachama wao

sishangai hata kidogo kwa wabunge wa chadema kufanya hayo

pamoja na yote hayo .... serikali ya ccm hailali usingizi .... hofu tuuuu .... ha haaa haaa kumbe serikali inaogopa hoja za bangi na wahuni, kweli wewe ni pimbi
 
Back
Top Bottom