Ni kweli Stanbic wanakata 12,000 kwenye accounts kwa mwezi?

melech

Member
May 29, 2013
62
125
Salamu kwenu wakuu, tumshukuru Mungu kwa kutufikisha mwisho wa mwaka, nasi tupige mahesabu yetu, tumefanikiwa kwa kiasi gani?

Swali langu, nataka kufungua Salary Account huko Stanbic Bank, kuna mtu ameniambia kuwa Stanbic kwa Salary account kila mwezi wanakata Tshs 12,000 ikiwa ni maintenance costs. Ila kuna staff wenzangu wana account huko wanasema siyo kweli, wengine wanasema ni kweli, hivyo nimeshindwa kujua ukweli haswa. Kama ni kweli, naona 12,000 ni nyingi sana for maintenance costs.

Naomba wenye ufahamu juu ya hili wananifahamishe, nataka kufanya maamuzi. Je, ni kweli kuna makato ya 12,000? Na je, vipi kuhusu makato mengine (ATM....)?

Asanteni.
 

epson

JF-Expert Member
Oct 1, 2012
554
500
Sina taarifa juu ya Salary Account, nafahamu Stanbic wana aina tano za akaunti ambazo ni Business Call Account, Business Current Account, Call Account, Personal Current Account na Transact Plus Account. Akaunti tatu za mwanzo nafikiri ni mahususi kwa wafanyabiasha. Mi nina Transact Plus Account ambayo walisema naweza kuitumia kupitishia mshahara, Monthly Management fee yake ni ths.9500 na makato mengine madogo madogo kama (9120000773598:WTax.Pd:01-07-2013to 31-07-2013 TZS 40.40), sijaona ATM withdraw charges kwenye bank statement, kwahiyo kama hakutakuwa na gharama za ziada za ku-process mshahara nakushauri fungua Transact Plus Account maana gharama zake kwa mwezi zitakuwa around 9500 otherwise wasiliana nao watakusaidia
[h=1]Customer care[/h] Tel: +255 (22) 266 6850
+255 (22) 266 6801
E-mail: tanzaniacustomercare@stanbic.com
service@stanbic.com
 

melech

Member
May 29, 2013
62
125
Asante sana epson, nashukuru kwa mchanganuo wako.Nitawaandikia e-mail hizo ulizonipa nione kama watajibu.

Kazi Njema.
 

mabwepand

Member
Jul 16, 2012
87
95
Mkuu hao stanbic ni wapuuzi tena sana mm natumia salary acount hiyo unayosema maintannace fee ni kweli kabisa Tzs 12,000 na atm charge Tzs 500 per transaction na ukichukulia ndani ni Tzs 2,500 per transaction wapo juu nbc wazuri sana
 

melech

Member
May 29, 2013
62
125
Loooh! Asante sana mabwepand,yaani hadi imebidi nishangae kwanza. Mkuu hiyo 120,000 wanakukata KILA MWEZI? Yaani 144,000/= kwa mwaka?


Mkuu hao stanbic ni wapuuzi tena sana mm natumia salary acount hiyo unayosema maintannace fee ni kweli kabisa Tzs 12,000 na atm charge Tzs 500 per transaction na ukichukulia ndani ni Tzs 2,500 per transaction wapo juu nbc wazuri sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom