Ni kweli Sitta, Ukisoma Ilani ya CHADEMA kwa akili ya KiCCM-CCM Haitekelezeki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli Sitta, Ukisoma Ilani ya CHADEMA kwa akili ya KiCCM-CCM Haitekelezeki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Sep 15, 2012.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Takribani wiki mbili zilizopita, nilisoma kwenye baadhi ya magazeti habari moja inayomhusu Mzee Spidi na Viwango Mzee Sitta. Kwa mujibu wa magazeti hayo, Mzee Sitta akiwa katika ziara ya kutembelea Mkoa wa Kagera alitumia fursa akiwa anaongea na wananchi kumjibu Dr. Slaa kuhusu mambo kadhaa aliyoongea juu yake.

  Katika majibu yake kwa Dr. Slaa, inasemekana Mzee Sitta alibainisha kwamba ni kweli kuna wakati yeye kama Mwanasiasa alikuwa anaangalia uwezekano wa kuhamia CDM lakini alighaili baada ya kusoma Katiba yake na Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2005. Eti mambo yaliyowekwa kwenye Ilani ya CDM ni balaa kwa taifa. Alitoa mfano wa sera ya elimu na huduma za afya kwa wananchi bure kwamba ni sera isiyotekelezeka.

  Binafsi, simlaumu sana huyu Babu Sitta kwa sababu natambua kwamba uwezo wake wa kufikiri kwa umri alionao umegoti hapo. Hawezi kwenda zaidi ya hapo. Na hii inatokana na mazoea. Amekuwa kwenye mfumo dhaifu. Mfumo usio na tija. Mfumo uliokosa ubunifu. Mfumo wa kuendesha nchi kwa mazoea. Ndiyo mfumo wa ccm, chama ambacho kadri siku zinavyokwenda ndivyo kinavyopoteza mvuto kwa wananchi. Kwa mawazo yake Babu Sitta ni kwamba hakuna vyanzo vingine vya mapato katika nchi hii zaidi ya hivyo vinavyotumiwa na ccm miaka nenda miaka rudi. Ndiyo maana akiangalia vyanzo hivyo alivyovizoea haoni wapi CDM itapata hela. Akili yake inafikiri kiccmccm. Kazi kwelikweli! Huyu ndiye Babu anayeutafuta urais kwa udi na uvumba.

  Watanzania, hatuna budi kuwapuuza wazee kama hawa. Wenye mawazo ya kimaskiniskini. Wazee ambao akili yao imegoti kwenye boksi linaloitwa ccm. Hawaoni mbele wala hawawezi kurudi nyuma. Ndiyo maana Mzee wa Kiraracha Lyatonga Mrema wakati wa kampeni mwaka 1995 akiwa anapeperusha bendera ya NCCR alipoulizwa atazipata wapi hela za kuhakikisha kila shule inajitosheleza kwa madarasa na madawati, aliwajibu tena kwa kujiamini kabisa kwamba fedha hiyo angeipata kwa kuhakikisha pale Bandarini na Airport kila mfanyabiashara analipa kodi ipasavyo. Aliongea hivyo kwa kujua na kuwa na uhakika kuwa taifa linapoteza mabilioni ya fedha kwa kuwaachia wafanyabiashara wakubwa wapitishe bidhaa bandarini na airport bila kulipa kodi ipasavyo.
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,944
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  kwa kuruhusu baadhi ya mambo ya Richmond yasijadiliwe bungeni ni dhaifu mno. Yeye alitaka Lowassa achafuke na si nchi ifaidike. Hana jipya. An old dog cant be taught new tricks
   
 3. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Hivi bado mnahangaika na huyu babu mnafiki
   
 4. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MKUU GOSBERT, katika kundi la watu ambao ni wanafiki waliokubuhu katika nchi nchi hii, Sitta ni kiongozi wao. Pamoja na uzee wake, bado yupo kwenye harakati za kuutafuta urais. Anachoongea siyo anacho-practice. Ana tamaa sana ya ukubwa. Amechagua kuwa mnafiki ili aupate urais. Yeye anadhani watanzania tumesahau alichofanya bungeni wakati wa skendo ya Richmond alipouzika mjadala kienyejienyeji kwa kutumia nafasi yake ya uspika.
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ndoto za alinacha...
   
 6. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Sita ni gamba flani la karibu na mkiani, alipoua mashirika ya umma kwa wizi wake ipo siku tutamtaka anyooshe maelezo
   
 7. Mdakuzi

  Mdakuzi JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,748
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Huyu babu mnafiki nilishampuuza kitambo, yaani wala hanisumbui kwa masika wala kiangazi!
   
 8. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Loading, please wait............
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani wazee wa aina ya baba mkwe wetu Edwin mtei aliyesema tume ya kuratibu maoni ya katiba mpya imejaa waislam ndio wa kupuuzwa.kinachowafanya wazee wa aina ya mtei waendelee kutamba ndani ya cdm ni safu nyembamba ya uongozi ndani ya chama hicho
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja...
   
 11. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ipi hiyo.....idiot
   
 12. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Akili imeenda likizo!
   
 13. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Unapoteza muda wako na wetu kwa kuwajadili watu wasio na tija kwa nchi yetu kama Sitta? bora ungemjadili mke wake kidogo ingekuwa na unafuu.
   
Loading...