Ni kweli siku hizi wajinga wengi ni vijana?

Ni kweli vijana walio wengi ni wajinga, na ujinga huu umeanzia kwenye tafsiri ya neno ujinga.
Ujinga ni nini?
Aina za ujinga?
Tabia za ujinga?
Hasara za ujinga?
Faida za ujinga?
Vijana wapo wangapi?
Vijana wajinga wangapi?
Vijana wasio wajinga wangapi?
NB: Mifano dhihiri inahitajika kuipa uzito hoja
Hitimisho.
 
Hivi polepole n kijana au Mzee?

Nikipata jibu kama kijana basi n kwel vjana Wa sikuhiz n wajinga maana hawasimamii ukweli mfano ishu ya katiba mpya

Kwa wazee nao n wajunga×2 ya vijana


Mfano kabudi na ishu ya katiba Mpya
Prof Lipumba na ishu ya uchaguzi Mkuu 2015
Wazir Wa habari utamadun na michezo Dr mwakyembe kukana andiko lake (thesis)

Lakn vjana kukana majina yao kama huyu boss Wa dar PCM kulikana jina lake DAB nao n ujinga pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni kweli na sababu kubwa ni wavivu wa kusoma au wakiwa wanasoma ni magazeti ya udaku kina shigongo wametajirka kupitia ujinga wa vijana wa sasa kwa story za kina diamond na wema sepetu.Ni rhisi kudanganywa na wanasiasa kwa sababu tu ya kukosa uwezo wa kupambanua mambo kwa kutoshugurisha akili yao.
 
ni kweli na sababu kubwa ni wavivu wa kusoma au wakiwa wanasoma ni magazeti ya udaku kina shigongo wametajirka kupitia ujinga wa vijana wa sasa kwa story za kina diamond na wema sepetu.Ni rhisi kudanganywa na wanasiasa kwa sababu tu ya kukosa uwezo wa kupambanua mambo kwa kutoshugurisha akili yao.
Tunatokaje hapo?
 
kwa mtazamo wa kitaaluma, Ukweli ni Relative.
Ndio maana akiongezea na points, references na facts kusupport hiyo argument yake ndio tutakuwa na uwanja mnene wa kupima.

Mtazamo wangu zamani watu wazima wengi walikuwa wajinga katika kizio cha academic education wakati maeneo mengine kama mahusiano, kutafuta pesa, kulea familia, ufundi walikuwa na akili. Kipindi hiki vijana wengi sio wajinga hasa katika nyanja ya taaluma maana wengi wamesoma na kuelimika katika umri mdogo kuliko hata zamani.

Pia elimu imerahisishwa hata bila kwenda shule unaweza kujifunza kusoma na kuandika kwa kutype kwa smartphone bila kwenda shule, Na hiki kinaweza kufanikiwa kwa Vijana kuliko wazee
Umeiweka vizuri hii mkuu
 
Ipo kauli inazunguka sana kwenye mitandao ya kijamii hivi sasa. Kauli hiyo inadaiwa kutolewa na Profesa Mwesiga Baregu. Isome hapo chini.

"Zamani tulikuwa tunafuta ujinga kwa watu wazima, siku hizi wajinga wengi ni vijana." - Profesa Mwesiga Baregu.

Kauli hiyo ina hoja na inafikirisha. Ni kweli siku hizi vijana wengi ni wajinga?

Kwamba, ujinga ni upi? Tafsiri yangu ya ujinga ni kutokujua kusoma na kuandika. Labda na kuhesabu. Je, ni hivyo?

Au, muktadha wa ujinga ni upi kwa kauli hiyo?

Nadhani ipo haja tujadiliane tujue. Kama ni kweli basi tujiulize kwanini vijana wengi wamekuwa wajinga katika zama hizi

View attachment 1404867
Zamani wazee wengi hawakupata access ya elimu, kutembea maeneo mbalimbali kujua tamaduni na namna mpya ya maisha ya wengine waliishi kwenye yale waliyoyajua kwenye mazingira yanayowazunguka na hii ilipelekea ujinga kwa maana ya kukosa maarifa mapya lakini walikuwa na uwezo mkubwa wa kumsoma mtu mgeni, kupambana na majanga kama magonjwa, muingiliano wa jamii walisisitiza sana kutooana bila kujua history za family na Mambo mengi ambayo kimsingi yapo na faida kubwa sana kimaisha kushinda kijana wa Sasa ambaye hata akikosa Panadol hajui kwamba maji na kupumzika au kunywa chai inaweza kumpunguzia kuumwa kichwa aubinti anapata uja uzito mpaka anajifungua hajui labour aende na vitu gani?

Siku hizi kijana amesoma, ametembea m hi mbalimbali Ila full ujinga hata ukisema akae akuandikie paper huku maofisini ni tabu tupu hapa tunaongelea intellect sio kujua kuandika, kutumia simu, kuwa na laptop, sijui video calls nk. Unaweza kujua hayo lakini kichwani hakina kitu kabisa na hii ndio anayoongelea professor.

Yawezekana hali hii ya vijana inasababishwa na ukuaji wa technology ambayo inarahisisha Mambo kiasi ya kwamba binadamu akisharahisishiwa anakuwa hawezi kutumia Ile rate ya 0-5 % ya intellect (IQ) ya mwanadamu wa kawaida na tusipowasaidia vijana tunabakiza taifa la wajinga wengi wasioweza kutoa mawazo mbadala kwa wenzao ili kuweza kulikwamua taifa maana siku hizi kila Jambo utasikia mbona Kenya au marekani wanafanya hivi, where is our intellectuals? Wako wapi wataalamu walioweza kusaidia nchi zao kwa utaalamu wao wenyewe???

However kumlaumu kijana haisaidii, wazee Wana nafasi ya kuwasaidia vijana waweze kujitambua na kufanya makubwa zaidi yao sababu fursa za sasa no nyingi kushinda wakati wa zamani.
 
Back
Top Bottom