Ni kweli serikali ya Tanzania imeishiwa vyanzo vya mapato?

Ukisoma kitabu kile cha BEHIND THE PRESIDENTIAL CURTAIN utaona mambo mengi anayoyafanya bwana Paul yameanza kujitokeza kwenye utawala wa Gywe.
 
Mimi ningetamani Rais aendelee na ziara zake kutembelea majirani zetu kama vile Visiwa vya Comoro, DRC, Burundi, n.k. huku akiongozana na kundi kubwa la wafanyabiashara na wawekezaji wazawa ili kusaini mikataba mbalimbali ya kibiashara kama wanavyofanya China, Marekani, nk. na hizo nchi. Yaani akatafute fursa nyingine nje ya mipaka yetu ili pesa ya wawekezaji wetu wazawa watakao wekeza huko, irudi nchini kuliko hii ya kuwanufaisha wageni tu mfano Wachina kupitia miradi mbalimbali ya miundombinu huku wazawa tukikamuliwa kweli kweli kupitia kodi na tozo mbalimbali kuwalipa hao Wachina na mwisho wa siku hela zetu wanaenda kujengea nchi yao.
 
Back
Top Bottom