Ni kweli Serikali ya Magufuli inaua upinzani?

ong'wafaza

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
245
105
Kumekuwa na minong'ono mingi kwamba uongozi wa serikari ya Magufuli unauwa upinzani.

Kwa maoni yangu upinzani wa nchi yetu uko katika makundi mawili makuu:

1.Wabishi (opposers).
-Hawa ni watu wanaokataa kila kitu hata kama ni cha ukweli ili mradi kulinda masilahi yao.

2.Wanaharakati (Protestants)'
-Hawa ni wale wanaokataa mambo wanayoyaona yanawanyima haki zao au za wenzi wao.

Mimi naona upinzani ulioko kwenye kundi la kwanza haupungui kutokana na uongozi wa serikali ya Magufuli.

Ikumbukwe kuwa kundi hili la upinzani haliko tu kwenye vyama vya upinzani bali liko pia kwenye chama tawala.

Kundi la pili la wapinzani ndilo linalopungua .

Hii nadhani ndo maana watu wanasema upinzani unakufa.

kama upinzani ni wa aina hii,inawezekana ukawa unakufa kweli kwani watu wengi wanaopinga kudhulumiwa haki zao watazidi kupungua kadri serikari itakavyokuwa inarejesha haki kwa watanzania.

Ila sidhani kama kundi la kwanza litaathirika maana lenyewe kazi yake ni kubisha tu ili mradi kulinda maslahi yake.

Tujadiliane.
 
Kwanini upinzani wamezuiwa kufanya mikutano?

Kwanini upinzani wanawekwa ndani?

Kwanini hamtaki meya wa jiji atoke upinzani?

Kwanini hamtaki upinzani itawale zenji?

Kwanini mnataka kusifiwa tu? Mnaogopa nini?

Kwanini mnajihesabia haki Na kujiona mmmesimama?

Kwanini mnataka vyombo vya habari vifanye vile mnataka ninyi?
 
Magufuli anaua upinzani {UNDELINE} hilo ndio jibulake.

Ngoja waje wa namba 1.
 
usiposifia mwaka huu utanuniwa na kila mtu. kwa mabaya au mazuri we sifia tu ila wakumbuke kuna mtu hapa alisfiwa mpaka akaitwa kijana uku akiwa na umri usiopungua 50 na mwingne mr clean lakin matokeo tumeyaona.
hili ndio tatizo la watanzania wavivu wa kufikiri kwa mapana
 
Kwanini upinzani wamezuiwa kufanya mikutano?

Kwanini upinzani wanawekwa ndani?

Kwanini hamtaki meya wa jiji atoke upinzani?

Kwanini hamtaki upinzani itawale zenji?

Kwanini mnataka kusifiwa tu? Mnaogopa nini?

Kwanini mnajihesabia haki Na kujiona mmmesimama?

Kwanini mnataka vyombo vya habari vifanye vile mnataka ninyi?
mkuu hizo ni dalili za uoga. Kama ccm wanajua upinzani umekufa kwanini wanawanyanyasa na kuwaweka sero ya nini?

hapa bila shaka ccm wanatambua nguvu ya upinzani bado ni kubwa.
 
Upinzani hauwezi kufa wakati mfumo wetu wa kisiasa ni wa KIDEMOKRASIA. Uelewa wa Watanzania walio wengi mfano mzuri ni wewe mleta mada,ndo unazidi kufa.Elimu,Elimu,Elimu ni tatizo kubwa TZ that's all we need kwanza mengine baadae
 
Back
Top Bottom