Ni kweli serikali ina tabia ya kutoweka wazi idadi ya wanaokufa katika majanga

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,316
50,522
Pale panapotokea majanga ni kawaida kwa serikali kupitia mamlaka na hasa vyombo vyake vya usalama kutangaza idadi ya majeruhi na waliofariki ila kumekuwa na maneno mitaani kuwa huwa kuna kawaida ya kupunguza namba ya waliokufa.

Nikiambatanisha na tukio la ajali Jana Mandela Road idadi rasmi iliotajwa ni marehemu wanne ingawa inasemekana kuwa wamekufa watu wengi.

Iko mifano mingi, nikikumbuka ile ajali ya treni Dodoma 2002 kulikuwa pia na utata kwenye namba ya waliokufa.

Je, hivi ni kweli wanausalama huwa wanapunguza idadi?

Je ,yote hayo ni kwa faida gani maana sote tunajua kuwa inapotokea ajali idadi yoyote ya wanaokufa inaweza kutokea sasa kwanini tufichwe?
 
Sidhani Kama Serikali inahusika katika hili mkuu. Ila nafikiri kuna ukweli kwenye hoja yako ya msingi. Takwimu huwa haziko sahihi haswa kwenye ajali za kutisha Kama hiyo ya jana Tabata matumbi.
 
Huuu uvumi hata upande wangu uku wa kusini kaskazini nausikiaga saana. Sijui hata faida ya ili ni nini?
 
Sidhani Kama Serikali inahusika katika hili mkuu. Ila nafikiri kuna ukweli kwenye hoja yako ya msingi. Takwimu huwa haziko sahihi haswa kwenye ajali za kutisha Kama hiyo ya jana Tabata matumbi.
Kweli mkuu Jana nilivoliona lile gari pale kituo cha bugurun sokon aisee ni kama watu zaidi hata ya 20.. Inawezekana huwa wanaficha ili kutowapa watu pressure ila sidhani kama ni sababu ya kutosha
 
Kweli mkuu Jana nilivoliona lile gari pale kituo cha bugurun sokon aisee ni kama watu zaidi hata ya 20.. Inawezekana huwa wanaficha ili kutowapa watu pressure ila sidhani kama ni sababu ya kutosha
Nafikiri pia inawezekana ni kwa nia njema kabisa. Maana si unajua Watanzania sisi kwa kupaniki. Let's say kwa mfano ingetangazwa ya kuwa " Kuna DCM kutoka Gmboto kuelekea Ubungo imepata ajali maeneo ya Tabata matumbi na watu arobaini wamepoteza maisha" nafikiri purukushani na tafrani ingekuwa kubwa sana...inawezekana wangeongezeka wengine Kama kumi kwa Presha.
 
Kwa ajali ya jana tabata naamini kwa asilimia 100% taarifa zitolewazo kuhusu ajali husika ni uongo...... Kuna mtu najuana nae jana kutwa nzima kashinda hana raha na leo hajatoka ndani kwa sababi ys kushuhudia ajali ile.... Na kwa mujibu wake ambae kwangu ni reliable source anasema kama kuna binaadamu wamepona kwenye ajali ile hawazidi wawili...
 
Kwa hii ya juzi nadhani kinyume chake yaweza kuwa sawa.

Waliopona ndio waliokufa, waliokufa ndio waliopona.
 
Dereva wa lori lililobeba ng'ombe amelazwa hospitali. Umri wake miaka 21. Anamlaumu dereva wa daladala.Huyu jamaa wa miaka 21 anasema ana uzoefu wa kuendesha gari toka 2002. Inanikumbusha IGP Mahita alivyokuwa analalamika kuhusu umri mdogo wa waendesha mabasi na malori.
 
Back
Top Bottom