Ni kweli serikali imekataza wananchi wa Bagamoyo wasiuze mashamba na viwanja?

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,574
Kuna taarifa zimezagaa mtaani kuwa serekali imekataza wananchi na serekali za vijiji vya Bagamoyo wasiuze mashamba na viwanja!

Kama habari hizi ni kweli vipi kuhusu wale walionunua mwanzo? Na Je serekali ina haki ya kumkataza mwananchi wake kutokuuza ardhi bila ya maelezo ya kutosheleza?
 
Siri kali, kumbuka kuna bandari mpya inajengwa huko wakati bandari kongwe zimeachwa zife,
 
Kuna taarifa zimezagaa mtaani kuwa serekali imekataza wananchi na serekali za vijiji vya Bagamoyo wasiuze mashamba na viwanja!

Kama habari hizi ni kweli vipi kuhusu wale walionunua mwanzo? Na Je serekali ina haki ya kumkataza mwananchi wake kutokuuza ardhi bila ya maelezo ya kutosheleza?
Wasipoiuza hiyo ardhi watakufa njaa!
Wabakinayo ardhi ya nini wakati hawajui kuitumia!
 
Halafu ikiwakataza kuuza inawapa mahitaji yao muhimu? Ni ngumu mtu hana fedha ya matibabu au Ada ya mtoto wake ya shule au chakula halafu umwambie asiuze Mali yake kutatua tatizo linalomkabili!
Serikali haina haja kuwakataza, iwape maisha bora ione kama watauza!
 
Ni hatua nzuri,watu wanatumia uelewa mdogo wa wananchi kununua ardhi Yao kwa bei ndogo na wengine kudhulumiwa na wanunuzi matapeli,hiyo haikubaliki,serikali isimamie Ili wananchi wale wauze ardhi Yao katika bei yenye tija Ili kukwamua maisha Yao...
 
Wanadhulumiwa vip wakati wanakubaliana! Na serekali ya kijiji inahusika?
 
Hakuna kitu kama hicho,nimetoka jana huko kwa malengo hayo hayo.Sema mwamko wa watu wengi kununua maeneo huko ni mkubwa.Vile vile wauzaji wana mwamko mkubwa wa kuongeza mke.
 
Back
Top Bottom