Ni Kweli Sera za CCM zimekuwa ni janga kuu la taifa? Tunavuna tunachopanda...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Kweli Sera za CCM zimekuwa ni janga kuu la taifa? Tunavuna tunachopanda...?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 14, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Ni kana kwamba watu hawataki kuamini kile ambacho wanakiona na wamekiona kwa macho yao kwa muda mrefu. Kuanzia kwenye kilimo, maji, afya, nishati, utalii, mifugo mpaka kwenye elimu -na kila kitu katikati- tunaona jinsi tulivyo nyuma kulinganisha na uwezo (potential ) yetu. Cha kushangaza kila siku tunawalilja watu walewale waje na mipango mingine au sera nyngine za mambo ambayo yametubitika kuwa yamewashinda. Kwanini tunamini leo kuwa chama kilekile kilichoshindwa kinaweza kuja na suluhisho bora? Kwa nini vigumu kwa viongozi wa upinzani, wasomi na wanaharakati kusema kilicho dhahiri kuwa SERA ZA CCM NI JANGA KUU LA TAIFA? Tunajisikia vibaya kufanya hivyo au hatupendi wao wajisikie vibaya?

  SERA YA AFYA 2003: Malengo ya sera hii ambayo ilichorwa karibu miaka 10 nyuma yako hivi:

  2.4 Policy Objectives
  The objectives of the Policy are to:

  2.4.1 Reduce the burden of disease, maternal and infant mortality and increase life expectancy through the provision of adequate and equitable maternal and child health services, facilitate the promotion of environmental health and sanitation,
  promotion of adequate nutrition, control of communicable diseases and treatment of common conditions.

  2.4.2 Ensure the availability of drugs, reagents and medical supplies and infrastructures.

  2.4.3 Ensure that the health services are available and accessible to all the people in the country (urban and rural areas).

  2.4.4 Train and make available competent and adequate number of health staff to manage health services with gender perspective at all levels. Capacity building of human resource at all levels in management and health services provision will be addressed.

  2.4.5 Sensitize the community on common preventable health problems, and improve the capabilities at all levels of society to assess and analyse problems and design appropriate action through genuine community involvement.

  2.4.6 Promote awareness among Government employees and the community at large that, health problems can only be adequately solved through multisectoral cooperation involving such sectors as Education, Agriculture, Water, Private Sector including Non Governmental Organization, Civil Society and Central Ministries, as Regional Administration and Local Government, and Community Development, Gender and Children.

  2.4.7 Create awareness through family health promotion that the responsibility for ones health rests in the individuals as an integral part of the family, community and nation.

  2.4.8 Promote and sustain public-private partnership in the delivery of health services.

  2.4.9 Promote traditional medicine and alternative healing system and regulate the practice.


  Ni yapi kati ya malengo hayo ambayo miaka kumi baadaye tunaweza kusema yamefikiwa kwa kiasi cha kutosha?

  SEKTA YA ELIMU

  Rakesh na wenzake waliandika mojawapo ya nyaraka muhimu kuelezea hali ya elimu nchini. Sehemu yake inazungumzia suala la mitihani lilivyo na kwanini sera hii haieleweki na haina malengo ya kuboresha elimu:

  3.4 Policy challenge four: measuring success
  In Tanzania, when all is said and done, educational success in primary and secondary education is measured in terms of examination results. Graduates are categorized into two camps ‘wamepasi' and ‘wamefeli'. Seven years of primary or four years of secondary education is judged on the basis of one set of one-time examinations. The past Minister for Education, Hon. Joseph Mungai, used every opportunity to point out that pass rates in the Primary School Leaving Examinations (PSLE) had increased from about 22% to 50% under PEDP, and this was clear proof that the quality of education had improved.


  What do these examinations look like, and what do they measure? My colleagues and I had a careful look at the PSLE last year. The examinations are multiple-choice, and in large part measure regurgitation of facts. Even the English and Swahili language PSLE do not require students to write a single sentence! In large part they do not measure analytical or problem
  solving skills. They do not measure the outcomes or capabilities as described above. The increased pressure to perform has meant that teachers teach to enable students to pass the exams, ‘cramming' to remember things that are not likely to help one much and which will be forgotten shortly after the examinations anyway. The constituent parts of the final examination
  scores have also been changed, such that the Swahili language score (in which Tanzanian students do best) count for more, and the overall performance score improves, when in fact there may no actual improvement. Our calculations suggest that it is possible for primary school leavers to pass Swahili and fail everything else and still score above the overall pass rate for the
  primary examinations.

  The risks here are great: that we distort learning objectives to focus on aspects that are not the skills and capabilities we desperately need, and that we lull ourselves into believing we are doing much better when in fact we are not. No wonder that a common concern of teachers of tertiary education is that their students lack basic competencies, and that the number one complaint of employers in Tanzania is not red tape or corruption or infrastructure but the lack of human resources – despite improved pass rates.

  If examinations is what ‘counts'; examinations should count what matters. We recommend that
  examinations policy and structure should be significantly revised. First, the possibilities of using continual assessment should be explored and introduced. The terminal examinations should count for only part of the final result. Second, the assessment should measure the capabilities and skills we need. These include complex comprehension, analysis, problem-solving, creativity,
  and writing. Third, the constituent part of the final scores should reflect an appropriate balance of what a well-rounded competencies required by all students.

   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Wanasiasa hasa Chadema wanasema hivyo mkuu,waliobaki wote wanaharakati,wasomi wanaogopa kusema!! Sisi ni wanafiki sana! Wepesi kusahau!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Lakini wapo wanaotaka ccm iboreshe sera zake na wanaipa ushauri wa kufanya hivyo.
   
 4. C

  Christiano Ronaldo JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mzee Mwanakijiji, unaheshimika sana humu, lakini wewe unajua kilichoshindwa siyo sera za CCM, na wala sera hizo si janga la Taifa. Na ukiangalia sera za Chadema hata CUF, hazina tofauti kubwa na hizi za CCM. Kilicho janga la Taifa ni utekelezaji wa sera hizo. Kwa bahati mbaya watekelezaji wa sera hizo si wanasiasa tu, zaidi ni watendaji serikalini, ambao wengine ni kama wanaihujumu CCM. Ukweli ni kwamba kuna watendaji ndani ya Serikali ni Chadema na wanahujumu serikali kwa faida ya Chadema kisiasa!
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,006
  Trophy Points: 280
  Kuna namna ambayo wana ccm wanaamini kuwa sera zao hazitekelezwi inavyopaswa, kwahiyo wambakia kuondoana madarakani, wana sera nzuri tu sema muda ukwapi?Hawana huo muda, uchaguzi ukishaisha, wanaanza kujiandaa kwa uchaguzi unaofuatia, ndo sera hiyo, na ni vitu ama mali gani atavuna, na kwa kawaida, namna ya kupata kura haipatikani ama kwa maana nyingine haitegemeani na utekelezaji wa sera za chama wala nini, hapo ndo kwenye mzizi wa fitina.
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Mkuu CCM haiwezi kubadilika! Mimi ni Muumini wa sera za Mwl Nyerere lakini ktk vitu ninavyokiri Mwl alishindwa kutusaidia ni kutuachia nchi kama vile wanaofuata wote watakuwa honest kama yeye! Hakutuachia nchi inayoendeshwa na mfumo(system) bali mifumo inaendeshwa na watu watakavyo! Hilo ni kosa kubwa sana! Viongozi wote wa leo ni matunda ya Mwl Nyerere waliokuwa akimtii Mwl Nyerere na sio System!! Hata Marekani ya leo wanaamini imejengwa na waasisi wa Taifa hilo ambao walibuni mifumo isiyoweza kuvunjwa na yeyote!!! ccm ndio mfumo! Hata wapinzani wanachezaj ngoma ile ile ingawa tunawaunga mkono hasa kwakuwa hatuna jinsi!!
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Jiulize hata Rais anawaogopa wanaccm hata kwenye maamuzi sahihi!! Unajua sababu?
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  ngoja nimpishe Dokta Tia-maji-tia-maji wa REDET atoe maoni yake kwanza ndo na mimi nitasema neno.

  napita.
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna chama ambacho kina sera mbaya? (given kwamba sera zinaandikwa na wataalamu na kuweka lugha tamu tamu)..

  Issue ni utekelezaji mkuu, nyerere na sera ya ujamaa na kujitegemea alishindwa kutekeleza, hatimaye ilibidi yafanyike mapinduzi mengine nayo imeshindakana kutekeleza ipasavyo..

  Nini kifanyika: imarisheni monitoring system kwa viongozi wetu through media, mahakama etc..maana tatizo watekelezaji (viongozi) wote iwe upinzani au ccm wana maradhi ya ulafi...
   
 10. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Sera hazijafeli ila ni watanzania ndio waliofeli. Tofautisha hapo, nafahamu wengi hawatanielewa.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Ninaamini hili ndilo kosa kubwa zaidi katika Tanzania hasa miongoni mwa wanaharakati. Watu wanaona meli inazama kwa sababu inaingiza maji lakini ukweli huu hawataki kuuona. Wanalalamika na kudai tatizo ni nahonda; kwamba angekuwepo nahodha mzuri basi maji yasingeingia kwenye meli. Wanatupilia mbali ukweli kwamba kuna tundu kubwa kwenye meli na bila kuziba tundu hilo haijalishi kama nahodha anatoka mbinguni au ahera meli bado itazama. Tumeaminishwa kwa muda mrefu kuwa "sera za CCM ni nzuri, tatizo ni utekelezaji wake" well kama izngekuwa nzuri kihivyo zisingekosa watekelezaji!
   
 12. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwa jinsi hali ilivyo sidhani hata kuna haja ya upinzani, wasomi, wanaharakati, na wengineo kusema kuwa CCM imeshindwa kuongoza.

  Nasema hivyo kwa sababu kila kitu kiko dhahiri kabisa kuwa hao jamaa wameshindwa kuongoza. Sihitaji mtu wa kunishawishi eti kuwa wameshindwa kuongoza.

  Macho yangu tu yanatosha kabisa kufikia hilo hitimisho na kuwa nipo tayari kabisa kujaribu utawala mwingine ili angalau niwape wengine nafasi ya kutunyesha wanachoweza na wasichoweza kukifanya.

  CCM nimeshaona wanachoweza na wasichoweza na nimewachoka.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  zinaweza kuwa sera nzuri kweli vitabuni hata zinasikika vizuri masikioni - lakini zimeshindwa! thats my point.
   
 14. T

  Topical JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  That means sera siyo issue hapa; tatizo ni rasilimali wa kutekeleza sera; watu hakuna mkuu Tanzania; Mtasiwa Deo alipokuwa jiji alikuw mzalendo sana aisee, kumbe viwango vya ulaji tu...

  Mkuu nafikiri tuangalie zaidi monitoring system kuliko sera, sera zote tamu tamu (kwasababu ni marketing tool)
   
 15. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo wanaokuwa wamefeli ni watanzania, swala sio kubadirisha sera, badala yake ni kubadiri walengwa wa sera.

  Mfano:
  Mungu ana sera zake ambazo ametuelekeza tuzifuate sie binadamu lakini leo sie binadamu kwa asilimia 99.9 hatuzifuati sera za Mungu. Je ni nani wakubadirishwa kati ya Mungu, sera zake Mungu na binadamu?
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  @mwanakijiji

  Sera ya chama gani zitafaulu na kivipi?

  Sera gani za ccm zimefeli? (unatakiwa uje mategemeo yalikuwa nini? na nakisi ni kiasi gani kufikia malengo kwa @ sera)

  Unajua waandishi kama nyinyi huwa mna kazi rahisi sana "kuandika emotional and generalized opinions"...kama vile zimefeli??(hii kitu ni very subjective)

  From practical point of view; hawajafeli kujua hilo unatakiwa kufahamu malengo ya kila sera yalikuwa nini?
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Uzuri wa waandishi kama mimi ni kuwa lengo letu ni kuchokoza fikra; sitaki kuandika makala kwa ajili ya wasomi na kuwafanyia kazi zote za kutafuta, kuchambua na kuweka tafsiri. Nilikupa mfano mmoja kuwa mojawapo ya sera ya MMAM (Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi ) ilikuwa ni kuwafikishia afya ya msingi wananchi wote ifikapo 2012. Kwamba hili halijafikiwa siyo maoni ni jambo halisi. Haijalishi sababu za kwanini haijafikiwa! Mfano mwingine ni kuwa tuliambiwa ifikapo Disemba 2011 kutakuwa na ongezeko la "megawatts" nyingi za umeme kiasi cha kuondoa tatizo la upungufu wa nishati hiyo nchini. Je tumefikia hapo? Kwenye elimu tumeweka maelengo mengi tu - yakiwemo yale ya milenia - na tayari imeshaoneshwa na wengine kuwa malengo ya 2015 mengi hayatofikiwa iwe kwenye elimu, maji au nishati! Sasa huku ni kufeli au kushindwa kwa sera hizo! Siyo kwamba hazikuwa nzuri au hazikuwa na malengo mazuri ni kuwa zimeshindwa kutekelezeka.

  Au unaweza kuonesha angalau sera ambayo imefanikiwa malengo yake?
   
 18. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  MM, Kuna tatizo mahali. Si kweli kwamba sera za ccm ni nzuri kwani sera nzuri ni ile iliyotungwa kwa kufikiri vizuri na kwa hakika hutekelezeka. Zao zimeshindwa kabisa.

  Naomba ifahamike kuwa watanzania wengi hawana fursa ya kupata habari na hata wanapopata habari kupitia vyombo vilivyopo huwa zimeandaliwa ili kukandamiza ufahamu wao. Si kitu cha ajabu kumkuta mtu mzima akishabikia ccm na serikali yake, huku akilalamikia ugumu wa maisha. Watu hao hawajapata elimu sahihi ya kuweza kuunganisha hizo dots ili wajue ukweli.

  Watanzania tunaoipenda nchi yetu tufanye kazi kubwa ya kutoa elimu sahihi kwa wenzetu. Vyombo huru vya habari vianzishwe na kushiriki katika ukombozi wa nchi yetu. Walimu na wakufunzi wajitolee kutoa elimu ya mabadiliko kwa wanafunzi wao ili nao wakawasaidie watanzania wengine.
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hujakosea ila tambua tu ya kwamba binadamu huwezi kuwa mkamilifu 100%, na mwl mwenyewe alikuwa akisema igeni mazuri yangu na kuyaacha mabaya. Basi mapungufu yake aloacha ni kazi kwa vijana wa taifa hili kurecover na ikiwezekana tuliangushe hili nduli ccm kwani ni hatari kwa maisha ya mtanzania
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sababu kila mmoja anajua maovu ya mwenzie
   
Loading...