Ni kweli, regia e. Mtema hatunaye kimwili tena! Sasa tufanye nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli, regia e. Mtema hatunaye kimwili tena! Sasa tufanye nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpui Lyazumbi, Jan 18, 2012.

 1. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wana JF wenzangu na watanzania wote kwa ujumla, Regia amefariki! Mwanga huu umepotea haraka sana. Kwangu mimi tangu nilipopata habari hizi kupitia mtandao huu nimejitahidi kulazimisha kuwa ni uongo. Hapana. Mbunge wetu mahili katangulia mbele za haki. Nasoma mabandiko mengi sana humu jamvini, mengi ya maoni nashindwa kuendelea kuyasoma - inaniuma. Kijana hodari na mwenye uthubutu kaitika mbele ya Muumba. Nimefuatilia habari zake tangu ajali iliporipotiwa, tabata, karimjee na leo ifakara, kwa ujumla ni huzuni, simanzi, masikitiko na sura za ukweli kwamba Regia E. Mtema lilikuwa ni tumaini la watanzania wanyonge walioweka matumaini yao kwake na kwa moyo wa dhati kabisa.
  Sasa leo, na hata kama hatuamini, hatutaki, tunamuombea, tunasikitika... Mapenzi ya Mungu yametimizwa! Ametumia utu wake na maisha yake kwa wapenda haki wote nchini. Na alipokwisha kuyafanya hayo kaitwa rasmi.

  Sasa tufanye nini?????????

  Naikumbuka misiba mbalimbali iliyopata kutukumba: - Edward Moringe, Julius Nyerere, Amina Chifupa, Bibi Titi Mohamed, Mtwa Mkwawa, Chifu Milambo ongeza na wengine wa kariba hiyo. Hivi tunafanya nini kwa mawazo, matendo, maneno, tabia... katika kuwaenzi mashujaa wetu? Kutaja majina yao kwenye mabweni? Viwanja? Mashule? n.k? Hebu wana jamvi nisaidieni...

  Tufanye nini?
   
Loading...