Ni kweli Rais Samia sio mfuatiliaji? Wasaidizi wake wana msaada gani? Kazi yao ni nini? Au na yeye hashauriki?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,206
42,067
Ukweli ni kwamba kuna matukio Rais wetu amekuwa akiingizwa mkenge ni pengine kwa makusudi au kwa bahati mbaya hasa na wasaidizi wake!

Mh Rais alipoingia madarakani alichagua wasaidizi kutoka kada mbali mbali kuanzia uchumi, siasa, diplomasia na kila kona!

Lakini pamoja na wasaidizi hao bado inaonekana ni watu wasio msaidia kabisa zaidi ya kumhujumu!

Kwanza walianza kwenye uteuzi wa boss wa TPDC wakachomeka mtu asiye na sifa baadae baada ya kelele Madam president akagutuka na kurekebisha. Swali: hawa wasaidizi walikuwa wapi kuzuia hili? Rais alikataa ushauri? Hashauriki na yeye?

Pili, hawa wasaidizi walijua kabisa Madam president anakwenda kufanya mahojiano na BBC chombo kinacho angaliwa dunia nzima. Kweli walishindwa kumuandalia kabisa possible questions na majibu?

Kama swala la Mbowe ilikuwa inajulikana wazi litaulizwa sasa mpaka Rais anatoa majibu kuwa wenzie Mbowe walishakiri makosa wakahukumiwa nani alimwambia? Ina maana wasaidizi wa Rais wote walikuwa hawajui kuwa case haijaanza kusikilizwa? Pengine Rais alifanya kusudi au hakutaka kusikiliza ushauri wao kwenye swala hilo?

Tatu, Madam president alikwenda kushiriki kwenye sherehe ya utiaji saini wa mkataba wa utengenezaji meli ambao baadae alikuja kugundua ni wa kifisadi na kipigaji bado maswali yanakuja hivi hawa wasaidizi wake wana msaada gani? Kwanini wana muingiza Rais kwenye mikenge? Kwanini Rais hakusaidiwa kufatilia hilo hadi anapiga makofi kwenye kusaini na baadae ndio ana stuka?

Nne jana kwenye hotuba ya miaka 60 ya uhuru watu walitarajia Mh Rais kugusia mambo muhimu ya kijamii na kiuchumi hasa mfumuko wa bei ya vitu na bidhaa mbalimbali na kutoa majibu na matumaini kwa watanzania lakini bahati mbaya ni kuwa waandaji hotuba wameona ni bora kumuhujumu tu kwa kuweka mambo ambayo siyo ya msingi kabisa na ambayo yalitakiwa kuzungumzwa siku ya uhuru maana ilikuwa historia. Hivi wasaidizi wa Rais kwenye uchumi, diplomasia, siasa na kijamii hawakuwa na la kuandika zaidi ya yale? Kweli kwanini tusiamini kuna watu wana mhujumu Rais baada ya kujua ni mpole?

Kwenye hotuba ya jana kuna makosa mengi hadi watu wanajiuliza ni nani aliyeandika hotuba ya jana na kumpa Rais?

Kiukweli ni wazi Rais wetu amekuwa mzito kufatilia baadhi ya mambo mengi hasa ya msingi hivyo wengi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kufanya yao na kumchomekea.

Bado najiuliza hawa wasaidizi wa Rais ni wanini? Wana kazi gani za msingi?
 
Ukitoa hotuba ambayo haigusi maisha na masumbufu yanayowakumba watu katika maisha yao ya kila siku basi ujue unatoa hotuba ya kipuuzi tu isiyo na maana yoyote na waliokuandalia hotuba hiyo yawezekana wana ajenda ya SIRI na ww kama Rais usipostuka basi ww ni mgonjwa.
 
Baba wa taifa Mwl.JULIUS NYERERE aliwahi kusema hv;MTU AKIKUSHAURI JAMBO HALI YY AKIJUA ANAKUSHAURI JAMBO LA KIJINGA NA KIPUMBAVU NA WW UKALICHUKUA NA UKALITEKELEZA BASI UJUE WW NI ZUZU NA KICHWA CHAKO NI HAMNAZO.
 
Aiseeeee
 
Ukitoa hotuba ambayo haigusi maisha na masumbufu yanayowakumba watu katika maisha yao ya kila siku basi ujue unatoa hotuba ya kipuuzi tu isiyo na maana yoyote na waliokuandalia hotuba hiyo yawezekana wana ajenda ya SIRI na ww kama Rais usipostuka basi ww ni mgonjwa.

Shida ipo kwa waandaaji
 
Raisianatakiea kutoa ma

Raisi anatakiwa kutoa maudhui kisha yana andaliwa ki ufundi na badae anayasema mwenyewe, sasa kama anaenda kutoa speech asiyoijua hapo nani mwenye makosa zaidi yake mwenyewe?
Inawezekana hata huku mitaani hajui nini kinaendelea na hii hali ya ugumu wa maisha haijui.
Anachosubili ni hao wasaidizi wamwambie ndio aamini na wasiposema ndo imetoka hiyo.
 
Ndio maana mimi nalaumu pande zote mbili ukiacha Rais lakini bado wasaidizi ndio wanatakiwa kuwa wa kwanza kujua makosa na kuyapatia ufumbuzi! Rais wetu ni kweli ana uzito wa kufatilia mambo ndio maana nasema nini kazi ya wasaidizi wa Rais?
 
Raisianatakiea kutoa ma
Raisi anatakiwa kutoa maudhui kisha yana andaliwa ki ufundi na badae anayasema mwenyewe, sasa kama anaenda kutoa speech asiyoijua hapo nani mwenye makosa zaidi yake mwenyewe?
Inawezekana hata huku mitaani hajui nini kinaendelea na hii hali ya ugumu wa maisha haijui.
Anachosubili ni hao wasaidizi wamwambie ndio aamini na wasiposema ndo imetoka hiyo.
hajui kinachoendelea mtaani SHE IS OUT OF TOUCH watu washa give up naye
 
Hotuba ya juzi ilikua ni mahususi kuelekea sherehe za miaka 60 ya uhuru.

Mimi naona alikua sahihi kujaribu kuelezea ni hatua gani nchi imefikia katika hiyo miaka, hasa akielezea hali ilikuwaje wakati tunapata uhuru na tumefikia wapi hadi sasa.

Sidhani kama kulikua na ulazima sana wa kujikita kwenye "shida za maji, kupanda kwa bei ya mafuta, mfumuko wa bei, na kero nyingine za wananchi".

Sijasema kwamba hayo mambo sio muhimu, la hasha, ni muhimu sana, ila sio kila hotuba ni ya ku address mambo ya namna hiyo.

Rais anao uwanda mpana wa matukio ambayo anaweza kutoa hotuba, atayasemea hayo kwenye "platforms" zingine. Juzi haikua ndio mwisho wa Urais wake.

Nyie.
 
Ukweli ni kwamba kuna matukio Rais wetu amekuwa akiingizwa mkenge ni pengine kwa makusudi au kwa bahati mbaya hasa na wasaidizi wake!

Mh Rais alipoingia madarakani alichagua wasaidizi kutoka kada mbali mbali kuanzia uchumi, siasa, diplomasia na kila kona!

Lakini pamoja na wasaidizi hao bado inaonekana ni watu wasio msaidia kabisa zaidi ya kumhujumu!

Kwanza walianza kwenye uteuzi wa boss wa TPDC wakachomeka mtu asiye na sifa baadae baada ya kelele Madam president akagutuka na kurekebisha. Swali: hawa wasaidizi walikuwa wapi kuzuia hili? Rais alikataa ushauri? Hashauriki na yeye?

Pili, hawa wasaidizi walijua kabisa Madam president anakwenda kufanya mahojiano na BBC chombo kinacho angaliwa dunia nzima. Kweli walishindwa kumuandalia kabisa possible questions na majibu?

Kama swala la Mbowe ilikuwa inajulikana wazi litaulizwa sasa mpaka Rais anatoa majibu kuwa wenzie Mbowe walishakiri makosa wakahukumiwa nani alimwambia? Ina maana wasaidizi wa Rais wote walikuwa hawajui kuwa case haijaanza kusikilizwa? Pengine Rais alifanya kusudi au hakutaka kusikiliza ushauri wao kwenye swala hilo?

Tatu, Madam president alikwenda kushiriki kwenye sherehe ya utiaji saini wa mkataba wa utengenezaji meli ambao baadae alikuja kugundua ni wa kifisadi na kipigaji bado maswali yanakuja hivi hawa wasaidizi wake wana msaada gani? Kwanini wana muingiza Rais kwenye mikenge? Kwanini Rais hakusaidiwa kufatilia hilo hadi anapiga makofi kwenye kusaini na baadae ndio ana stuka?

Nne jana kwenye hotuba ya miaka 60 ya uhuru watu walitarajia Mh Rais kugusia mambo muhimu ya kijamii na kiuchumi hasa mfumuko wa bei ya vitu na bidhaa mbalimbali na kutoa majibu na matumaini kwa watanzania lakini bahati mbaya ni kuwa waandaji hotuba wameona ni bora kumuhujumu tu kwa kuweka mambo ambayo siyo ya msingi kabisa na ambayo yalitakiwa kuzungumzwa siku ya uhuru maana ilikuwa historia. Hivi wasaidizi wa Rais kwenye uchumi, diplomasia, siasa na kijamii hawakuwa na la kuandika zaidi ya yale? Kweli kwanini tusiamini kuna watu wana mhujumu Rais baada ya kujua ni mpole?

Kwenye hotuba ya jana kuna makosa mengi hadi watu wanajiuliza ni nani aliyeandika hotuba ya jana na kumpa Rais?

Kiukweli ni wazi Rais wetu amekuwa mzito kufatilia baadhi ya mambo mengi hasa ya msingi hivyo wengi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kufanya yao na kumchomekea.

Bado najiuliza hawa wasaidizi wa Rais ni wanini? Wana kazi gani za msingi?
Rais mwenyewe kilaza mkuu usilaumu wasaidizi, na ukilaza unaanza na kuteua hao wasaidizi wake...

Anajaza wakwe na Mashostu kwenye ofisi ya umma unatarajia nini?
 
Ni dosari ndogo za kawaida sana, kichwa cha RAIS kinabeba mambo mengi na mazito, kupitiwa ni ubinadamu
Sasa mambo gani mazito zaidi ya hayo anayoyazungumzia? Kwamba kazi zake hazihusu hayo anayosimama kuhutubia?
 
Back
Top Bottom