NADHARIA Ni kweli Rais Samia ana nasaba na familia ya Mfalme wa Oman?

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Habarini,

Nimeona hii kitu ikanistua, naomba kujuzwa juu ya huu undugu na kama kweli, wanyama wetu watabaki kweli?

Maana enzi za awamu ya mzee ruksa, mkewe alituhumiwa/shutumiwa kusafirisha wanyama hai kwenda arabuni saivi Rais Samia anasema ataimarisha usafiri wa majini ili kusafirisha wanyama hai.

Nijuzeni kuhusu hili swala.

1657961716664.png
 
Tunachokijua
Baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Magufuli, jina la Samia Suluhu Hassan lilikuwa maarufu sana si tu nchini Tanzania na Afrika, bali pia duniani kote. Vyombo vingi vya habari vilichapisha habari zake, huku vingi vikieleza ukweli kwamba ndiye mwanamke wa kwanza kuwa Rais katika taifa ambalo lilikuwa likielekea kutimiza miaka 60 ya uhuru. Hata hivyo, katika kipindi chake tangu aliposhika wadhifa huo, kumekuwa na minong’ono ya hapa na pale, ikiwamo wanaohoji endapo Rais Samia ana uhusiano wa kinasaba na familia ya kifalme ya Oman.

Swali ni: Je, ukweli ni upi?

Chimbuko la swali hilo linaonekana kuwa ni siku ambayo Rais Samia akiwa kwenye Kongamano la Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, alitaka kuwepo kwa vyombo vya usafirishaji vya majini kusafirisha wanyama walio hai na bidhaa mbalimbali kwenda nchini Oman ili kuboresha biashara kati ya pande hizo mbili.

Baada ya habari hiyo kuenea, mtumiaji wa JamiiForums aliposti screenshot inayomuonesha Rais Samia akiwa na mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni mjomba wake wa huko Oman. Kichwa cha habari katika mjadala wake kinasema: "Ni kweli Rais Samia ana nasaba na familia ya Mfalme wa Oman?"

Screenshot hiyo ni ya picha iliyopostiwa katika mtandao wa Instagram na akaunti moja mnamo Juni 14, 2022. Maneno yaliyosindikiza picha hiyo yanasema: "Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amtembelea mjomba wake. Uhusiano kati ya Oman na Zanzibar (sasa Tanzania) una mizizi ya kihistoria na kuunganisha baadhi ya uhusiano wa kifamilia na nasaba endelevu."

Kwa kutumia Google Image Search, tumebaini picha hiyo imetumika katika majukwaa mengi ikiwa na ujumbe unaofanana. Hata hivyo, swali la uhusiano wa Rais Samia na familia ya kifalme ya Oman bado halijibiwi wala kuthibitishwa na picha hiyo inayosemekana yupo na mjomba wake.

Pamoja na hivyo, uchunguzi wetu hauwezi kupuuza ukweli kwamba Rais Samia amekuwa akitajwa kuwa na uhusiano na nchi ya Oman.

Kwa mfano, mnamo Oktoba 18, 2017, wakati Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dk. Mohammed Hamad Al Rumhy alipotembelea Tanzania, Rais Magufuli alimtaja Makamu wa Rais Samia kuwa na wajomba wanaoishi Oman. Katika video hiyo, Rais Magufuli alisema: "Nilimtuma jana Makamu wa Rais kwenda kuniwakilisha kule. Na bahati nzuri Makamu wa Rais wajomba zake wapo Oman. Kwahiyo alikuwa nyumbani…"

Dokezo hilo la Rais Magufuli halikufunga mjadala wa uhusiano wa Samia na Oman. Mnamo tarehe 20 Machi 2021, tovuti ya gazeti la The National la nchini Oman lilichapisha makala iliyohusu uhusiano wa Rais Samia na nchi hiyo. Makala hiyo yenye kichwa cha habari "Historia ya Pamoja: Wananchi wa Oman Wafurahia Samia Suluhu Hassan Kuwa Rais wa Tanzania" ilieleza kuwa kiongozi huyo ana uhusiano na Oman kupitia babu yake wa upande wa baba, ambaye alizaliwa katika mji wa Al Mudhaibi, nchini humo.

Makala hiyo pia ilijumuisha mahojiano na baadhi ya ndugu wa karibu wa Rais Samia wanaoishi nchini Oman, ikiwemo Bw. Mohammed Al Naamani ambaye alielezwa kuwa ni binamu wa Rais Samia. Al Naamani alithibitisha kwamba Samia alitembelea Oman mwaka 2016 akiwa Makamu wa Rais, na alipata fursa ya kuwatembelea ndugu zake katika mji wa Al Mudhaibi. Hata hivyo, kutokana na majukumu yake, hakuweza kurudi tena huko baadaye.

Kwa mujibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, nchi hizi mbili zina uhusiano wa kihistoria na kinasaba ambao unaanzia karne ya 19. Inaelezwa pia uhusiano huu ni wa kipekee kwani Oman ndiyo nchi pekee nje ya Afrika ambapo Kiswahili kinazungumzwa kama lugha ya kwanza na watu wake wana uhusiano wa kinasaba na watu wa Tanzania.

Hivyo basi, kutokana na uhusiano huo, si ajabu kwa Mtanzania yeyote (hasa kutoka Zanzibar) kuwa na ndugu wa karibu nchini Oman. Kwa sababu ya mizizi ya kihistoria na kiutamaduni inayounganisha pande hizo mbili, kumekuwa na uhamiaji na uingiliano wa kijamii kati ya watu wa Zanzibar na Oman kwa muda mrefu.

Uchunguzi wetu katika vyanzo mbalimbali vya mtandaoni haujaweza kuthibitisha ushahidi wa kihistoria unaounga mkono madai kuwa Rais Samia ana uhusiano wa nasaba na familia ya ufalme wa Oman, bali huenda ana uhusiano wa familia na Oman kupitia babu yake wa upande wa baba kama ilivyoelezwa katika vyanzo kadhaa hapo juu.
Niliwahi kuona clip JPM akisema Samia wajomba zake wapo Oman! ?!Nafikiri Kuna kitu hapo aidhakwa baba au Kwa mama.
 
Hamna ni waarabu wanajuaga cheza na akili za hawa weusi wetu .mm nafanya biashara na waarabu yaana huwa hawawapendi hata kuwasikia wanaamini weusi washenzi.muarabu ili akuheshimu
1.ajue unahela kumzidi.sisi tukienda Oman ile kuona tumekuja tafuta hela sio kuomba hela utashangaa wanasema watanzania ni ndugu zao na kutuita wajomba .ila ukienda kuomba kazi hata uwe muislamu na maskini hawa koko hawakutambui
2.wanzanzibati halisi ni makabila ya kigoma na tabora .mambo ya kujiita waarabu kisa kuchangia damu kidogo upuuzi mfano wachaga wengi wamezaliana na wakenya sijasikia wakijiita wakenya
 
Habarini,

Nimeona hii kitu ikanistua, naomba kujuzwa juu ya huu undugu na kama kweli, wanyama wetu watabaki kweli?

Maana enzi za awamu ya mzee ruksa, mkewe alituhumiwa/shutumiwa kusafirisha wanyama hai kwenda arabuni saivi Rais Samia anasema ataimarisha usafiri wa majini ili kusafirisha wanyama hai.

Nijuzeni kuhusu hili swala.

Kiswahili kwani ni lugha ya watanzania! Kiswahili kilianzishwa na washihiri(waarabu) wafanyabiashara waliokuwa wakija kwa majahazi Afrika Mashariki, hawa walitua Malindi, Mombasa Unguja, Dar es Salaam, Mafia na Kilwa na Msumbiji, hivyo hakikutakiwa kuwemo kama ni mfano.
 
Acha kuwapa sifa hakuna mwanadamu amewahi anzisha lugha duniani labda hizi za kina Elon musk .lugha ya kiswahili ilizaliwa yenyewe wakati wafanyabiashara (na hapa usidanganywe ndo walikuwa matajiri zaidi) wahindi waarabu na watanganyika ambao na wazanzibar wakiwemo (walikuwa waha au wanyamwezi) walikuwa wakitafuta namna ya kuelewana wafanye biashar ndo kiswahili kikazaliwa .hata kiarabu hakuna aliekianzisha .lugha ya kiswahili ilikamilika kwa miaka 500 huyo muarabu gan alikuwa na kumbukumbu hiyo ndo maana kiswahili kimekopa maneno kwenye lugha si chini ya 10.na asili yake ni unguja na kenya (mali ya Tanzania na kenya ) ndo maana waarabu asilimia 90 hawajui kiswahili
 
Hamna ni waarabu wanajuaga cheza na akili za hawa weusi wetu .mm nafanya biashara na waarabu yaana huwa hawawapendi hata kuwasikia wanaamini weusi washenzi.muarabu ili akuheshimu
1.ajue unahela kumzidi.sisi tukienda Oman ile kuona tumekuja tafuta hela sio kuomba hela utashangaa wanasema watanzania ni ndugu zao na kutuita wajomba .ila ukienda kuomba kazi hata uwe muislamu na maskini hawa koko hawakutambui
2.wanzanzibati halisi ni makabila ya kigoma na tabora .mambo ya kujiita waarabu kisa kuchangia damu kidogo upuuzi mfano wachaga wengi wamezaliana na wakenya sijasikia wakijiita wakenya
Pole sana

Sent from my ATU-L31 using JamiiForums mobile app
 
Habarini,

Nimeona hii kitu ikanistua, naomba kujuzwa juu ya huu undugu na kama kweli, wanyama wetu watabaki kweli?

Maana enzi za awamu ya mzee ruksa, mkewe alituhumiwa/shutumiwa kusafirisha wanyama hai kwenda arabuni saivi Rais Samia anasema ataimarisha usafiri wa majini ili kusafirisha wanyama hai.

Nijuzeni kuhusu hili swala.

Siyo wanyama tena mkuu ni bandari!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom