Ni kweli Rais JK anastahilii kupongezwa??

BALAKI

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
371
100
Wana JF, napenda kuwatakieni furaha na amani ktk sikukuu hizi za mwisho wa mwaka.

Hivi karibuni tumeshuhudia masikitiko makubwa pengine kwa mwaka 2013, baada ya ripoti ya mh Lembeli kufichua unyama unaofanywa na vyombo vya usalama juu ya wananchi. Hii ilipelekea mawaziri 4 kupoteza nyadhifa zao japo kwa shinikizo la bunge. Hata hivyo ni wazi kuwa waheshimiwa hawa walitolewa kafara kumwokoa mtendaji mkuu wa serikali PM pinda.

Baada ya Mh JK kuridhia kufuta uteuzi wa mawaziri hao alipongezwa sana na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini
Mimi bado sikuona ni busara kufanya kazi kwa kushinikizwa kwa sababu zifuatazo

1)Mh rais hana taarifa sahihi juu ya watendaji wake kwa kuwa angekuwa anawafahamu vyema hakukua na haja ya kusubiri shinikizo

2)Hii inatoa taswira kuwa watendaji wa karibu na washauri wake akiwemo PM hawakuwa wanamsaidia kupata taarifa sahihi kutoka wizara husika na hivyo kuweza kufanya maamuzi sahihi mapema

3)Mawaziri hawafanyi kazi peke yao, yupo naibu waziri, yupo katibu mkuu wa wizara, inamanisha utendaji mbovu unawahusu hawa wote ni kuwa hawa ni kama injini moja

4)Kufanya kazi kwa shinikizo kwaeza kuigharimu nchi hasa pale ambapo shinikizo latoka kwa watu wenye nia mbaya kama kikundi cha mafisadi na wenye maslahi binafsi juu ya jambo husika wanapodhamiria kumwondoa mtu yeyote alie kinyume na matakwa yao.

5)Inamanisha kuwa serikali haioni matatizo yaliopo ktk wizara nyingine, hivyo inasubiri shinikizo ndo ijue kuna matatizo makubwa. Hawa walioshinikizwa ndio ambao wanafanya vibaya kuliko wengine? La hasha hawa wameanikwa mno ndo maana aibu ikawa kubwa mno tena kupitia kamati

Tunaitaji Viongozi wa nchi wenye kuwafahamu fika watendaji wao, wanaoifahamu fika nchi yao kuepuka kufanya maamuzi kwa shinikizo na kuepuka kuigharimu zaid serikali kwa kuunda kamati za kuchunguza mambo ambayo yako wazi yanaonekana na hayahitaji kamati ndipo yajulikane.
Mungu Ibariki nchi yangu Tanzania

Nawasilisha
 
Unajikanyaga sana mkuu, mara watendaji wabovu, mara wameondolewa kwa shinikizo, na mbaya zaidi ulichokiandika ni tofauti kabisa na kichwa cha mada yenyewe. Dalili za upigaji majungu hizi.
 
Hivi watanzania....tujiulize kujiuzuru kwa waziri n suluhisho...me nahisi n hatua ya awali baada ya hapo sheria ichukue mkondo wke ila c kwa mahakama za majaji wezi wala rushwa n wasiotenda haki km mahakama za nchi hii ikiwezekana wafikishe the heity uholanzi...
 
huyu jamaa ni mzigo tena mzito,mwalimu aliligundua hilo mapema 1995,kuwa using cheap popularity zinaweza wacost watanzania since smost of us ni wadanganyika aka mazuzu,kafanya taasisi ya urais kuwa rahisi insuch mpaka january anaona kuwa nae anaiweza,tunahitaji rais mtendaji na sio mzururaji
 
Kikwete ni wa kuhukumiwa tu, hafai kupongezwa.....apongezwe kwa lipi jema alifanyalo hapa nchini?
 
kijana , wako wale waliopata FURSA , BILA SHAKA WANATAKA utawala huu uendelee hata kwa miaka mingine 100 !
 
Ni raisi mpitaji. Anakaa zaidi nje ya nchi kuliko muda anaokaa humu nchini! Huyu ndiye haswa alipaswa kujiuzulu! Hata hivyo ndiye amiri jeshi mkuu na jeshi ndilo limedhalilisha raia hivyo ajiuzulu!
 
Back
Top Bottom