Ni kweli pesa ilikuwa ngumu kuipata lakini ilikuwa na thamani tofauti na sasa

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
769
2,244
Ukweli lazima usemwe hata kama ni mchungu.

Kwa miezi kadhaa kabla ya machi 2022, pesa ilikuwa na thamani japo ilikuwa si rahisi sana kuipata kutokana na mirija mingi ya rushwa na ufisadi kufungwa. Leo hii pesa haina thamani. Tsh elfu 10 ni kama sh elfu 1.

Bidhaa bei ghali. Tozo kila mahali. Kila mtu analia. Hata wenye nacho (japo hawasemi) ila wanajua wazi hali si shwari. Mbaya zaidi bidhaa pamoja na kuwa bei ghali, mahali kwingine hazipatikani kirahisi.
Mipaka imefunguliwa. Nafaka zinasafitishwa nje ya nchi.

Hakika Tz imekuwa yatima! Nendeni vijijini, mijini kwa wananchi wa kawaida (wenye akili za kawaida) mtafahamu kwa uhalisia jinsi hali ilivyo!

Inahuzunisha sana. Kila kukicha afadhali ya jana!
 

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
769
2,244
Ukweli mtupu, ukichench elfu 10 inaisha hapo hapo.
Kuna mdau mmoja alisema, inafika mahali unafanya hesabu, maanake unaweza kuhisi umedondosha au hujarudishiwa change kamili.

Inasikitisha sana. Bidhaa bei iko juu. Hasa za chakula. Na mtu huwezi kuacha kula. Hali ni mbaya!
 

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,627
14,027
Ukweli lazima usemwe hata kama ni mchungu.

Kwa miezi kadhaa kabla ya machi 2022, pesa ilikuwa na thamani japo ilikuwa si rahisi sana kuipata kutokana na mirija mingi ya rushwa na ufisadi kufungwa. Leo hii pesa haina thamani. Tsh elfu 10 ni kama sh elfu 1...
Sasa wewe kwako kipi Bora upate urahisi wa kupata pesa au ugumu wa kupata pesa?
 

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
769
2,244
Sasa wewe kwako kipi Bora upate urahisi wa kupata pesa au ugumu wa kupata pesa?
Pesa ni kama maji ya kunywa.

Kadri unavyokuwa na kiu, ndivyo unavyohitaji zaidi.

Hivyo basi, kadri unavyopata pesa iwe kwa urahisi au ugumu; ikiwa bidhaa ziko juu, makato ya kodi na tozo kila mahali, gharama kubwa za usafiri na usafirishaji; basi ujue ndivyo itakavyotumika zaidi. Na huwezi ona thamani yake!
 

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
7,281
8,977
FB_IMG_16561807386406851.jpg

waa husika mwenyewe ndoivo tena darasa walikuwa ivo
 

heartbeats

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,477
5,873
elfu kumi ni kama buku mazee kuna mtu anataka kuuza nyumba yake ml50 ina sehemu kubwa nkamwambia unaitupa
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom