Ni kweli Nyerere Hakujenga Uchumi Imara Lakini Watanzania Wengi Walinufaika Nao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli Nyerere Hakujenga Uchumi Imara Lakini Watanzania Wengi Walinufaika Nao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 7, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  WanaJF,
  Kila mara ninaposoma threads zinazomchambua Mwl. Nyerere nimekuwa nikikumbana na hoja zinazonisikitisha sana. Baadhi ya wachangiaji wanasema sera za Nyerere zilifeli kuwaletea maendeleo wananchi. Watu hao wanafika mbali kiasi cha kusema enzi za Mwl. Nyerere wananchi walikuwa na maisha magumu sana. Kwamba kila bidhaa ilikuwa inapatikana kwa foleni.

  Kimsingi, ninakubaliana na hoja kwamba Mwl. Nyerere hakufanikiwa sana katika eneo la uchumi. Pamoja na kutofanikiwa huko, hali ya maisha kwa wananchi haikuwa mbaya kiasi tunachoshuhudia leo na tofauti kati ya wenye nacho na wasio nacho haikuwa kubwa kiasi tunachoshuhudia leo. Vilevile, wakati wa Mwl. Nyerere elimu ilitolewa almost bure na fursa ya kusoma ilikuwa wazi kwa kila Mtanzania, awe maskini au tajiri. Leo hii, watoto wa maskini wenye bahati wanaishia shule za Kata zisizo na walimu wala vitabu. Elimu bora imekuwa kwa matajiri tu.

  Yapo mambo mazuri mengi ambayo yanamtofautisha Nyerere na viongozi wetu wa leo. Tatizo letu vijana wa sasa tunadhani maghorofa na magari yanayoongezeka kwenye baadhi ya miji ni ishara ya kuboreka kwa maisha. Tunasahau kuwa asilimia kubwa ya wananchi ni maskini wa kutupwa wenye kipato cha chini ya dola moja kwa siku.
   
 2. m

  mzambia JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Nyerere ni nyerere hakuna wa kumfananisha africa hata cia wanalijua na walishindwa.
   
Loading...