Ni kweli ninachokiona ni utaifishaji au ni marekebisho ya makosa ya ubinafsishaji wa Mkapa?

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,260
7,195
Kwa jinsi naona jitihada za utawala huu, na juhudi za kujinasibu na sera za mwalimu Nyerere ni wazi ninachokiona ni km utaifishaji wa kila kitu kiwe cha umma tena. mara nyingi nikiwa na mashaka na ninachokiona huwa najaribu fikiria inawezekana ni askari kanzu wa Mkapa kaamua mrekebishia mtangulizi wake makosa ya ubinafsishaji au lah. Ila mengi yanaonyesha kwamba hapana, tunarudi kule kule kwenye mali za umma.Mali ambazo ni risk sana katika utawala mbovu ,pamoja na ule ugonjwa sugu wa serikali nyingi duniani.Kukosa ufanisi kwa kiasi cha kufanya kila project ya serikali kuwa hasara kuliko faida. Serikali nyingi duniani kwao hasara ya thamani ya hela sio kitu, kwao faida za kisiasa ndio muhimu sana.Hii si nzuri sana kuweka usitawi wa nchi ktk hisani ya wanasiasa wanaopita.

Macho na akili za kijamaa hayajawahi kuwa rafiki wa biashara.Mjamaa akiona hela huwa anaona kwa akili za shida zake. hawezi pata best price kwa realistic ways, wanatupa tupa kwa vile hawapo serious sana ktk principals za uchumi.Ndio maana wanaibiwa sana, na wakipewa nafasi ya kujirekebisha huja na mabei ya kubuni. Wajamaa haamini sana sheria ndio maana sio ajabu kumkuta mjamaa ni dr ila anaenda kwa mganga kwanza kucheki malaria, unaweza mkuta ni mchumi ila rais asiye mchumi ndio anamuongoza.Mjaa kila kitu kwake ni fadhila na ,ndio maana hawana ahsante.Mjamaa anachopewa anataka kiwe bure kabisa,kisipokuwa bure kabisa analalamika sana kuwa SIO BURE, ila yeye akitoa hata haki ya mtu huiita fadhila.

Sasa hivi juhudi zote za kushusha madaraka chini zilizofanywa kwa hela ya misaada au kodi za wananchi wengine ili nasi tuanze jikomboa, zimegeuzwa kuwa bure, alichofanya mkapa hata km alifanya vibaya kimerudi zero, maendeleo ya mabenk binafsi sasa yanarudi chini tunarudi ktk serikali ielile yenye watu wanaoweza kuingia kwa makundi ya kikanda,badala ya weledi.

Hali ilivyo kuna kila dalili kwamba, serikali itapata faida za muda mfupi ila mapato sio endelevu tena, muda sio mrefu visima vitakauka.Halamshauri zitakausha hela kwa rais na kuzipeleka hazina(Km kuchimbia hela chini na sio kuweka ktk bank zinazozungusha), watu wanafungiwa hata km kuwa wazi kungesaidia walipe kodi kwa awamu.Ni tabia km zile za watu wanaotaka kula ya leo tuu kesho itajijua yenyewe.

Tusipojiangalia tunaweza jikuta hatuipi nchi km wezi walivyokuwa wakisaidia uchumi. Km wezi walikuwa wakizungusha hela kwa namna serikali ilikuwa ikipata kodi ktk bidhaa,huduma na mishahara kwa iasi kikubwa kuliko sasa.Then serikali ilipaswa kutafuta namna ya kuongeza hiyo kodi toka ktk channels zinzpopita hela za wezi ili mapato yawe makubwa kuliko hela waliyoiba+riba. Technically ingekuwa km walikopeshwa vile.By the time mkakati wa kuwaadhibu unapita,basi kuwafilisi iwe ni faida mara dufu,na wasilete mshtuko ktk uchumi.
 
Kazi anayo jamaa ila anasahau kuwa zama zimebadilika huko duniani na sio nyerere tena

sent from my iPhone 7 nimeinunua SAPNA pale Posta mtaa SAMORA
 
Kazi anayo jamaa ila anasahau kuwa zama zimebadilika huko duniani na sio nyerere tena

sent from my iPhone 7 nimeinunua SAPNA pale Posta mtaa SAMORA
Ujamaa ni ushetani mkubwa sana.Na ujamaa haujengi jamii ya watu walio tayari kukiri makosa na kuruhusu dunia ya watu wengine iende mbele.Noth Korea wanafanya upuuzi wa kumfa mtu,south korea rais anatoka kirahisi tu na kupelekwa mahakamani mapema sana bila hata ubishi km tunaouona hapa wa akina muhongo,chenge, na wengine. CCM km chama haijawahi kiri hadharani makosa yao , ila wanatumia gharama kubwa snaa kuyafunika.
 
Venezuela,Zimbabwe wanajuta Kwa kile kifanyikapo sasa Tanzania.Masikini anadhani tajiri akinyanganywa Basi yeye lofa anapata
 
Chaga Development Manifesto. Kwao kila kitu kibaya kama wanga.
Kwani hukutaka chaga Development?Mtakuwa wachawi tuu,km mpo busy kuzuia wengine kufanikiwa kwa vile mnaona wakifanikiwa watawazidi. Una udogo wa akili sana.Nani kakuambia unaanza kwa kupitisha kila kitu kizuri ndio baadae ugundue kuwani vibaya?Ndio maana kila siku mpo empty. Hatuhitaji kila kitu kuwa kibaya ili tuangamie.Ingekuwa hivyo basi binadamu wanaokufa kwa UKIMWI ,hata mzinzi hakuwa mbaya ktk issue nyingine za maisha ila UKIMWI . Huwezi futa makos amakubwa hivi kwa ushabiki wa kikanda na kikabila eti hujaona mazuri.Makosa mengine unakubali ni makosa ili ujirekebishe kwa vile yanaathiri wengine.
 
Venezuela,Zimbabwe wanajuta Kwa kile kifanyikapo sasa Tanzania.Masikini anadhani tajiri akinyanganywa Basi yeye lofa anapata
Wajamaa wapuuzi kweli kweli,hasara wanazotubebesha bila huruma kwa vile sheria wamezishikilia wao, wanadhani wengine duniani wanaruhusu huo ujinga.Kwanza mijaaa haiwjibiki kwa lolote, hata nyumba zao zina njaa kwa vile inafuja chakula, inaumiza wanachhi na yenyewe ikishachacha ,inakuja tena kuvizia misaada kwa wananchi wao. Haijui dunia imeungana,na issue za dharura duniani,mijaa haina msaada zaidi ya kuhitaki kusaidiwa. Watu makini hawawapi huo muda.Ndio maana inalia sijui ubeberu.
 
Na huyu ngosha tusipokuwa makini atatuingiza huko huko. Watanzania tumatabia ya kufuata upepo bila kuhoje na kuangalia mbele kuna nini? Ila madhara ya ya kujazana upepo tutauona baadaye. Halafu mtaanza kusema alikuwa anaamua pekeyake wakati kuna viongozi wakuongea nae kama hataki umma unalibeba.
 
Back
Top Bottom