Ni kweli Mwenyekiti ameshindwa kudhibiti Uhalifu Kitongoji cha Magadirisho?

Emashilla

Senior Member
May 24, 2012
138
26
Bwana Jela(CCM)alitangazwa mshindi. Huyu ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa Kitongoji cha Magadirisho kwa miaka mitatu iliyopita.
Siri kubwa yafichuka kwa ushindi wa CCM Magadirisho katika nafasi ya mwenyekiti wa mtaa katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni katika mamlaka ya mji mdogo wa Usa-River,Arusha. Miongoni mwa mambo hayo ni:

(1)Biashara ya Mali ghafi ya kutengeneza gongo

Inasadikiwa kuwa Msambazaji mkubwa wa molasesi inayodhaniwa kutumika kama mali ghafi ya
kutengeneza pombe haramu ya gongo na wasaidizi wake walimpenda Jela.Mfanyabiashara
huyu ni jirani yake.Huenda watu hawa walikuwa na mashaka kama chama kingine kikishika madaraka
biashara hii ingechunguzwa na hatua kuchukuliwa endapo inatumika kwa malengo hayo mabaya.

(2)Biashara haramu ya gongo na pombe zingine

Ufuatiliaji unaonesha, "WAMTONI" ni kundi la watu wanaokaa muda mrefu maeneo ya mito kwa lengo
la kuchemcha pombe haramu ya gongo au piwa. Baadhi ya mabalozi wa nyumba kumi wananyooshewa
vidole kuwa ni vigogo wa kuchemsha gongo.Biashara ya gongo inauzwa hata mbele ya ofisi ya
Kitongoji.Soko la gongo ya Magadirisho inaelezwa kuwa ni maeneo ya Mali Asili, Kwa Mangusha,
Ngurdoto na Jijini Arusha pamoja na Magadirisho eneo analoishi Mwenyekiti wa Kitongoji.Wauza
gongo, Pombe za nafaka kama busaa na madadii walihofia biashara zao.

(3)Uharibifu wa Mazingira

Eneo jirani na makazi ya Bwana Jela kuna uharibifu mkubwa wa mazingira hasa ya chanzo cha maji
ya chemchemi ya Magadirisho. Watu wanaofanya shughuli za kuchimba mawe, udongo na kutengeneza
matofali karibu au ndani ya chanzo hiki cha maji walihofia kuzuiwa kuendelea kuhatarisha
chanzo hiki muhimu cha maji kimewafanya kukirudisha CCM madarakani pamoja na mapungufu yake.
Chanzo hiki ndicho kinatoa maji yanayotumika Magadirisho juu na kwa baadhi ya watu na taasisi

eneo la Saiti(Site)
attachment.php


(4)Mgambo kutoza watu fedha za kukamata watu

Baadhi ya askari mgambo kama sio wote, walijitokeza kupigania CCM kuendelea kuwa madarakani.
Baadhi ya mgambo katika eneo la Magadirisho waliwekwa kama mawakala wa kusimamia uandikishaji
wapiga kura na hata wengine walianza kukamata vijana ovyo kwa visingizio kadhaa. Ukifuatilia
utagundua kuwa mgambo hawa wanahusika katika kazi ya kukamata watu kwa malipo ya kati ya
shilingi 5,000/= na 30,0000/= kwa kila mgambo. Malipo haya ni kama biashara kati ya mlalamikaji
na mgambo amabyo imeendelea kwa muda mrefu. Hofu ya mgambo hawa huenda ilitokana na
wanachokifanya sio sawa au ni rushwa ndio maana walijikuta wakipambana kuiweka CCM madarakani
tena.Labda kuna mengine nyuma ya pazia!wameacha kulinda amani na usalama na kugeukia siasa.

(5) Mapato na Matumizi ya Kitongoji

Viongozi walitumia propaganda za kila aina kuhakikisha kuwa jamii inawaamini.Mwenyekiti
hajawahi kusoma mapato na matumizi ingawa Magadirisho ina vianzo vingi vya mapato. Suala hili
la mapato ya kitongoji imekuwa changamoto kubwa kwa viongozi wa CCM Magadirisho kulazimika kutumia kila
namna kurudi Madarakani ili kuendelea kufaidi bila kuwaeleza wananchi mapato yao na matumizi
kwa miaka mitatu iliyopita.

WANA MAGADIRISHO NAWAPA POLE KWA KUPENDA MWANGA WA GEREZANI KULIKO GIZA LA URAIANI
 

Attachments

  • Magadirisho Water Tank.jpg
    Magadirisho Water Tank.jpg
    30.8 KB · Views: 89
Tukio la wizi wa mbuzi jana lilichukua sura tata baada ya mwenyekiti kufanikiwa kuwashawishi waliowakamta wezi wawili kuwaachia huru watuhumiwa hao.

Baadaye wezi hao walimuuza mbuzi mmoja kwa mteja. Ndipo walioibiwa mbuzi walifanikiwa kumkamata mnunuzi wa mbuzi. Vijana wezi walikamatwa tena na kufikishwa kituo cha polisi cha Usa-River.

Mwenyekiti Gerald Kidelio(Jela) alilazimika kugeuza utetezi wake kwa watumiwa kuwa hawakuwa wezi. Kumbe vijana hao walikuwa wamehusika na matukio mengine ya aina hii.

Wananchi tunaunga mkono juhudi za vyombo vya dola katika kukomesha uhalifu katika eneo analoishi kiongozi wa Kitongoji hiki.
 
Back
Top Bottom