Ni kweli mwenge haukufika kileleni?

Tundapori

JF-Expert Member
Aug 12, 2007
554
250
Inasemekana ni kutoelewana kati ya serikali na JWTZ kutokana na serikali kuvunja makubaliano ya awali kuwa jeshi la wananchi ndilo lishughulikie mipango yote ya kupandisha na kuzima mwenge miaka 50 ya uhuru. TBC nao (walisusa?). Tukio la mwenge kufikishwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro lilipaswa kurushwa LIVE lakini hata hilo halikufanyika sababu wanazotoa ilitokana na kamera za kituo hicho kushindwa kufanya kazi vizuri katika miinuko ya juu. Hata hivyo, mmoja wa watangazaji wa TBC Sostehes Amas, alionekana kupitia kituo hicho akiripoti kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Hadi leo hakujatolewa hata picha moja ya mwenge ukiwa kileleni.

::Mwananchi

Walitaka CCM ndiyo ipandishe mwenge na siyo JWTZ.
 

The Emils

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
569
195
Inasikitisha sana kuona hata mambo ya muhim kufanywa ya kisiasa...bora huo mwenge uuzwe pesa zake zijengewe madarsa ili watoto wapate kusoma..
 

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
1,500
Ukweli siku zote humtenga mtu mnafiki na mzandiki dhidi ya muungwana na mstaarabu, ww kwenye wakweli haumo. Sothenes Almas hakufika kileleni bali aliishia kituo cha 3 kutoka chini. Na hii yeye mwenyewe alisema kwenye Taarifa ya habari ya TBC kuwa alishindwa kufanya hivyo kutokana na kukosa pumzi na hali ya hewa kuwa nzito. Sasa nakushangaa ww unaesema Sosthenes , yupi huyo sasa? Kuwa mkweli siku zote.

Usimlaumu mwanzisha thread yeye amekupa source habari alipoitoa.
 

Royals

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
1,450
1,500
Kama ni kushindwa tumeshindwa tu. Angelikuwa ni Tido Mhando kila kitu kingewekwa wazi na kuonwa na kila mtu kwenye tv zaidi ya wiki. But ndo hivo siku ya kufa nyani miti yoote huteleza. Hata kuupandisha mwenge kileleni.
 

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
1,500
nyirendabc.jpg
Yaani tumekosa picha muhimu ya kumbukumu ya miaka 50 ya uhuru ni sawa na kukosa picha ya siku ya harusi haiwezi kurudi milele, but who is to be blamed.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,870
2,000
TBC ilionyesha kipindi maalum wakiwa kilele cha mlima kilimanjaro na mwenge wa uhuru niliona labda tuombe warudie


Kuanzia griman point na uhuru peak juu ya kilele cha mlima kilimanjaro ni barufu na baridi negative nilipofika pale juu kamera yangu haikufanya kazi lakini sijui kama kuna uhusiano na hali ya kule juu au la. Vituo viko 6 cha kwanza Malangu, mandara, Holombo, kibo, Gilman's na uhuru peak
PIPIJOJO, kwanza hongera kupanda mlima Kilimanjaro, angalau tuna mwana jf ni mwakilishi wetu aliyepanda mlima kufika kileleni.

Pili kwa taarifa hiyo, kama kule kileleni ni baridi ya freezing points, hata huyo mpigapicha wa TBC asingepata picha kama kamera yake haikuwa na insullator!.
 

Mabulangati

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
795
250
Ukweli ni kwamba mwenge uliika kileleni ila wanahabari wengi hawakufika kileleni picha zipo (mwananchi toleo la tarehe 24/12/2011 page 2 na mwandishi emmanuel herman) kuhitilafiana kati ya jeshi na serikali kuhusu uratibu ndilo jambo lenye utata na sijajua ukweli uko wapi ila nitafanyia uchunguzi thabiti na kutoa habari kamili maana saa nyingine kama kuna maslahi kila mmoja anajaribu kufukuzia. Alipopandisha nyirenda serikali ndiyo iliratibu shughuli nzima na siyo jeshi maana nchi iko chini ya raia.
 

Mr Marcus

Member
Sep 8, 2011
23
0
As a nation mnajisikiaje mkisoma habari hizi?


inamaana wanajeshi hawana press unit yao?

mindhali hakuna picha then hawakufika huko juu

its that simple

huko TBC naona bora Tido arudishwe
 

Sabung'ori

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
2,119
2,000
Inasikitisha sana kuona hata mambo ya muhim kufanywa ya kisiasa...bora huo mwenge uuzwe pesa zake zijengewe madarsa ili watoto wapate kusoma..

...utamuuzia nani kibatari ktk karne hii ya sayansi na teknolojia?...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom