Ni kweli Mrisho Ngasa na Haruna Chanongo wamesaini Yanga?

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984
Kuna tetesi hizo na kwamba tayari wapo Kambini kujiandaa na michuano ya Sportpesa.
Mwenye taarifa zaidi atujuze jamani.
 
Sio kila tetesi zote unaziamini,ni uongo
wp_ss_20170604_0006.png
 
safi sana nampenda chanongo kweli.nilimtamani sana siku moja atue yanga dogo anajua sana huyu.pale simba ni figisu ndo zilomuondoa
 
Labda mashindano ya SportPesa yanaruhusu kusajili wachezaji but sidhani kama hao wachezaji watachezea Yanga baada ya hayo mashindano ya SportPesa.Kumbuka hayo mashindano yanaanza wakati wachezaji wengi wako kwenye timu zao za taifa
 
Kuna tetesi hizo na kwamba tayari wapo Kambini kujiandaa na michuano ya Sportpesa.
Mwenye taarifa zaidi atujuze jamani.
Ikiwa hivyo nitafurahi sana na naamini hata Ngasa atafurahi pia! Yanga mrudisheni huyo mtu! Bado ana uwezo wa kucheza ligi ya bongo. Ondoa Busungu, Matheo na magalasa mengine rudisha Ngasa!
 
Ndala bhana mchezaji jua la magharibi lakini bado wanae
Kwani Boko anaujana gani? Si bora Ngasa mwenye mapenzi na moyo wa kuitumikia klabu kwa dhati kuliko huyo Boko akikosa maslahi anadengua! Zimwi likujualo halikuli likakwisha ndugu! Viongozi wangu wa Yanga mrudisheni Ngasa bado anaweza akaisaidia timu!
 
Sio kila tetesi zote unaziamini,ni uongo
NGASSA KUANZA KUONEKANA UWANJANI NA YANGA KESHO




Mshambuliaji Mrisho Ngassa ataanza kuichezea Yanga katika michuano ya SportsPesa Super Cup kesho.

Yanga itaivaa Tusker FC ya Kenya katika mechi ya pili baada ya Singida United kuwa imeanza mechi ya kwanza dhidi ya AFC Leopards.

Ngassa amefanya mazoezi na Yanga jana na leo asubuhi tayari kwa mechi hiyo ya SportsPesa Super Cup.

Taarifa zimeeleza kwa kuwa michuano hiyo wachezaji huru wanaweza kushiriki, Yanga imeamua kumtumia Ngassa baada ya yeye kuomba kwa kuwa ni mchezaji huru.
 
Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza Jumatatu ya Juni 4, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa michezo miwili kuchezwa, Yanga inatarajiwa kuwa na wachezaji watatu wapya
 
Back
Top Bottom