Ni kweli Mhe. Deo Filikunjombe alichoma gari la serikali kwa makusudi?

The Hunter

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
1,049
305
Kwa muda sasa nimekuwa nikizisia kauli za kinafki za viongozi wetu, wengi wakiwa ni hawa wafuja mali maarufu, Kitendo cha Mbunge wa Ludewa bwana Deo Filikunjombe kumponda Mwanakijiji ni unafki wa kutupwa, kama kweli Deo unauchungu na nchi yako nini kilikusababisha kuchoma gari la serikali ulilokuwa unatumia pale kijichi na ndani kukiwa na mafaili kibao, na hata raia walipotaka kuuzima moto uliwakataza? najua unakumbuka vizuri! Je ungekuwa msafi ungechoma moto lile gari la umma najua unajua ulilichoma kwa sababu zipi!
 
GREAT THINKER wa JF umekaa wee ukaona bora uje na thread isiyona kichwa wala miguu bila kuambatanisha ushahidi wowote ule
 
GREAT THINKER wa JF umekaa wee ukaona bora uje na thread isiyona kichwa wala miguu bila kuambatanisha ushahidi wowote ule

Unataka ushahidi gani? nenda pale karibu na Neluka sekondari kuna skeleton la ile gari!
Si kweli watu walio abroad si wazalendo kwa kupinga uhuni wa hawa mchwa wachache.
 
dah! Ka ni kweli basi viongozi wengi ni wanafiki si alisema yeye ni mseminary so ana maadil?
 
Unataka ushahidi gani? nenda pale karibu na Neluka sekondari kuna skeleton la ile gari!
Si kweli watu walio abroad si wazalendo kwa kupinga uhuni wa hawa mchwa wachache.

mimi mwenyewe naishi kijichi na hilo tukio nalifahamu sana nililiona kwa hiyo ni ukweli
 
Tatizo humu JF tumechanganyika na MAJANUARY wengi pia,na kila mwanajamii yeyote anapotoa ukweli,basi wao huugeuza kuwa kejeli.kwa maslahi yao na hao mababa na mama zao walioiharibu nchi..kisa ELIMU za kubebwa na CV Fake."TUNAWAELEWAA!"
 
Eh? Naombeni maGreat Thinkers, tuache kashfa na kejeli. Mwenye hiyo story ailete nzima nzima, non-biased, kwa kuwa nahisi kuna watu wametumwa kuharibu mjadala ili kupoteza lengo. Kumbukeni hawa waheshimiwa(ingawa sioni uheshimiwa wao) ni watembeleaji wazuri wa hii mitandao ya jamii ili kujua nafasi yao kwa raia wa kawaida.
 
upupu mtupu kuanza kuleta mambo ya mbunge wa ludewa hapa, mnaofanya hivi mnatakaka kutuondoa kwenye malengo ya msingi
 
guys, i have always loved and respected jf. I thought jf as for great thinkers... Tuache majungu. Deo has never owned a government car. Na si kweli kwamba amewahi kuchoma gari la serikali. Achome gari la serikali ili iweje? Jf si mahali pa majungu, pls.
 
Tatizo humu JF tumechanganyika na MAJANUARY wengi pia,na kila mwanajamii yeyote anapotoa ukweli,basi wao huugeuza kuwa kejeli.kwa maslahi yao na hao mababa na mama zao walioiharibu nchi..kisa ELIMU za kubebwa na CV Fake."TUNAWAELEWAA!"
Unataka kutwambia deo ana cv fake? Tupeni cv yake.
 
Kwa muda sasa nimekuwa nikizisia kauli za kinafki za viongozi wetu, wengi wakiwa ni hawa wafuja mali maarufu, Kitendo cha Mbunge wa Ludewa bwana Deo Filikunjombe kumponda Mwanakijiji ni unafki wa kutupwa, kama kweli Deo unauchungu na nchi yako nini kilikusababisha kuchoma gari la serikali ulilokuwa unatumia pale kijichi na ndani kukiwa na mafaili kibao, na hata raia walipotaka kuuzima moto uliwakataza? najua unakumbuka vizuri! Je ungekuwa msafi ungechoma moto lile gari la umma najua unajua ulilichoma kwa sababu zipi!

huu ni upotoshaji wa makusudi. naijua hii ajali. gari lile ni range rover,lilikuwa mali ya deo. lilipata ajali ya moto mara baada ya kutoka service. nadhani fundi umeme alichemsha. kipindi hicho deo hakuwa mfanyakazi wa serikali. mtoa mada hii ni mwongo wa makusudi. hafai humu ndani. au aombe radhi. tito mganwa
 
upo sahihi huu ni uzushi. mtoa mada, labda, atakuwa na agenda nyingine, binafsi. great thinkers think great, and ont in a majungu way. please
 
Wakuu,

Mimi nilikuwa Mkazi wa huko Kijichi wakati huo, hapo naona Bwana Hunter hajafanya utafiti wa kutosha. Hiyo gari ni kweli iliungua, ilikuwa ni Range Rover old model HSE 4.6. Iliungua hapo karibu na nyumba ya jamaa mmoja anaitwa Dominick alisimama hapo kulikuwa na kioski akawa kasimama akiwa anamsalimju huyo mke wa rafiki yake mwenye nyumba, gari ikaanza kutoa moshi kwa upande wa chini, yeye Deo hakuona, mke wa huyo jamaa akamstua kuwa vipi mbona gari yako inatoka moshi sana, huyu jamaa akamjibu kuwa eti hiyo ilikuwa ni kwa sababu aliwasha AC, wakaendelea kuongea, mara yule mama akamstua kuwa haiwezekani mbona moshi ni mwingi mno, jamaa kustuka anashuka atizame mara moto ukalipuka into flames, akaanza kuhaha kutoa laptop na documents toka kwenye gari, na watu wakaja kujaribu kuuzima. Kumbuka ile gari ni ya petroli, na wenyewe mnajua moto wa petroli si kama wa mafuta ya taa. Jamaa walijaribu kuizima ikashindikana, na hata watu wa Fire Fighting walichelewa kufika, nilifika hapo ikiwa inamalizika kuwaka.

Ile Range Rove ilikuwa ni mali yake Bw Deo si ya serikali, huyu bwana hajawahi kuwa na gari ya serikali kwa hiyo hapo aliyeanzisha mada ametudanganya. Na ili kuthibitisha hili Kampuni ya Bima kupitia broker mmoja aitwaye IMPEX INSURANCE walimlipa kwa sababu alikuwa na comprehensive insurance, ingelikuwa ya Serilaki wangemlipaje?Na pia ninavyofahamu mimi kampuni za bima hawalipi kienyeji ni mpaka wajiridhishe mazingira ya ajali, kukiwa na any sort of negligence or intentional destruction on the side of the claimant huwa hawalipi. Kwa hiyo naunga mkono wanaJF wengine kuwa hayo ni majungu, na kwa mujibu wa umakini wa mtandao wa wanaJF hatuendekezi majungu humu ndani. Hivi mtu mzima,Unasemaje vitu usivyokuwa na uhakika navyo?Si ufanye utafiti kwanza? Ikumbukwe kuwa majungu ni hatari sana katika jamii.

Nawakilisha.
 
Dogo unaakili sana, hiyo ndiyo hoja!!!!!. Deo achome gari la serikali ili iweje???? Katika Wasifu wake hakuna mahali alipowahi kufanya kazi na akakabidhiwa gari la Serikali. Kwani MKURABITA ambako alifanya kazi kulikuwa na madreva ambao waliwaendesha. Hilo gari la Serikali ni la Wizara gani na Idara ipi???? Serikali gani hiyo ambayo imekaa kimya kwa muda wote huu. Aache kutuharibia mood kwa DEO.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom