Ni kweli mfalme BOKASA wa jamhuri ya central africa aliwalisha marais nyama za watu?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli mfalme BOKASA wa jamhuri ya central africa aliwalisha marais nyama za watu??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BRUCE LEE, Jan 29, 2011.

 1. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana jamvi nimekua na mjadala na baadhi ya wa2 kuhusu viongozi wadhambi wa africa, tulipofikia habari za bokasa,wanasema alianza kama rais then akaamua kujibadilisha na kua mfalme na baadae akataka kujibadilisha na kuwa emperor wa jamhuri hiyo ndio akaandika barua kuwaalika wageni kuja sherehe ya kuapishwa kua emperor ali wachukua wafungwa weye afya na kusema wapewe chakula ili wawe na afya nzuri kwani watakaguliwa na wageni, kumbe lengo lake lilikua wanenepe then wakachinjwa na kua kitoeo cha wageni waalikwa na kila balozi na rais aliehudhuria alikula nyama za wafungwa hao. Pia alikua na kiwanda cha kutengeneza sare za wanafunzi na ilikua nilazima kila mwanafunzi avae sare hizo na kila mtoto aliekamatwa hana sare alipelekwa kwenye zizi la bokasa ambalo alikua anafuga mamba na kuwatupa humo na kuliwa. Wajameni nimeshangazwa na habari na maelezo zaidi yanapatikana kwenye kitabu the world most evil men. Hivi kweli tutafika wa afrika? Historia inatusuta.
   
 2. T

  The Future. Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh! Hapo panatia uchungu sana, lakini swali kujiuliza wapo wapi sasa? Hili ni fundisho tosha la jinsi gani wafrika tulivyokua na matatizo ya asili kumbe hata huyu mkwere karithi dam chafu ya viongozi wadhambi bila shaka hata yeye anguko lake lipo karibu,tuungane kuupinga udhalim wake.
   
 3. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  pia kuna wengine kama mobutu na iddi amini,mi namashaka na akili zao pamoja na imani zao,inakuaje mpaka mtu anaamua kua mnyama kabisa na kufanya matukio ya ajabu?
   
 4. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walimpakazia tu because he was eccentric so an easy target. yes alikuwa dictator lakini hakulisha watu nyama, incident hiyo alimtania balozi mmoja wa nje kwamba nyama aliyoandaliwa ni ya watu. (kitabu kizuri ni the political oddessy of emperor bokassa)...very interesting insight on the crazy man. watoto waliuwawa na polisi na wanajeshi walioletwa kuzima maandamano kupinga uniform ambazo walilazimishwa kununua kwa kiwanda cha familia yake, siyo mamba.
   
 5. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  mwana habari, kwanini alazimishe watu kuvaa uniform za kiwanda chake? Na kwanini ajibadilishe vyeo kila kukicha? Sina imani na kauli yako kua alizingiziwa nahitaji kufanya utafiti wa kihistoria.
   
 6. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  usidhani iddi amini uliyemuona kwenye movie ndio yule mwenyewe:car:
   
 7. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  najua sio mwenyewe wa kwenye movie ya rise and fall of amin, ila nimeona documentary yake mwenyewe, alihojia kuhusu mpango wake wa kuishambulia israel,na uhasama wake na nyerere alicheka kisha akasema nyerere ni mzuri na ana mvuto na kama angekua mwanamke angemuoa,nikweli amin aliwafukuza wahindi, alikula moyo wa mtoto wake baada ya kuambia na waganga wa kienyeji kua akifanya hivyo hakuna atakae weza kumuua na atakufa kwa amri ya mungu. Hakuna haja ya kumtetea amini alikua mchafu tu.
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Historia iliyopotoshwa!

  Unapoandika habari kuwa ".. Nasikia blah blah blah..." Ufahamu kwa dhati kuwa unaadika uongo!

  Bokassa, Mabutu, Amin .... walitenda makosa ya kiungozi kama watawala wengi tu duniani walivyofanya .. tatizo ni kuwa mismamo yao haikufurahisha watawala wa Ulaya ya Magharibi!!

  Kuvalishwa uniform wanafunzi kwa lazima kuna tofauti gani na sera ya Nyerere ya vijiji vya Ujamaa?
   
 9. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  kwani sera ya vijiji vya ujamaa waliopinga nyerere aliwaua?una linganisha usiku na mchana?we vipi baba enock?kwa hiyo waliopinga kuvaa sare walistahili kuu awa?na huyo mobutu hivi unajua aliyo mfanya patrice lumumba?usikurupuke na kuanza kutetea ujinga.
   
Loading...