Ni kweli malengo yao tumeyasikia lakini uwezo wetu je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli malengo yao tumeyasikia lakini uwezo wetu je?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Sep 30, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Ni kweli malengo yao tumeyasikia lakini uwezo wetu je?

  a) Deni la nje limekua mara takribani tatu kati ya mwaka 2005 hadi 2010 na hakuna la maana ambalo JK alilolitekeleza. Hili deni litazuia wakopeshaji kuendelea na kasi ya miaka mitano iliyopita katika kutukopeshwa kutokana na credit rating yetu kutelemka vibaya mno na ufisadi unazitafuna sehemu kubwa ya hizo fedha. Hivyo sehemu kubwa ya ahadi za wagombea wote zihusuzo miundo mbinu hazitekelezeki. Huo ndio ukweli hatutakuwa na fedha isipokuwa ahadi za shule bure, afya bure na nyinginezo za huduma za jamii hizo kwa kufuta misamaha ya kodi kwa wakubwa hela ipo ingawaje hiyohiyo lazima imegwe kulipia madeni makubwa ambayo JK atatuacha nayo katika msimu wake wa kwanza.


  b) Mfumuko wa bei unaashiria ya kuwa Benki Kuu kwa miaka mitano ijayo itatumia kazi kubwa kupooza athari hizo kwa kuuza fedha za kigeni na serikali itakabiliwa na migomo mingi sana ya nyongeza mishahara ya wafanyakazi kutokana na mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu. Haya yote yana maanisha ya kuwa yeyote atakayeongoza serikali ijayo muda mwingi atautumia katika kupunguza makali ya kiuchumi na wala siyo kubuni miradi mipya ambayo hata hivyo fedha hatunazo.

  c) Hoja ambazo zina gharama nafuu ni za kuboresha utawala bora ambalo ndilo chimbuko la watanzania kutoshiriki katika kuchangia maendeleo ya nchi yao. Na hii hoja ndiyo kiini cha ahadi za Dr. Slaa na kama akifanikiwa angalau tuna uhakika wa miaka mitano ijayo tutakuwa tuna katiba mpya itakayatoa nafasi ya kupunguza migongano ya watendaji serikalini , bunge, mahakama na vyama vya siasa ambako rushwa kubwa kubwa ndiko zimepatia mwanya wa kutusurubu

  c) Kasi ya kukua uchumi wa kati ya asilimia 5 hadi 6, ni ya kuliwezesha taifa liweze kupata ugali wa siku hiyo lakini taifa hili ili liwe na ubavu wa kutekeleza miradi kemu kemu kama wagombea wanavyosema itabidi uchumi ukue kwa asilimia 10 hadi 20 jambo ambaloni ndoto za alinacha.

  Tuwasikilize lakini tuelewe ya kuwa labda ni uchu wa madaraka au wanatudharau upeo wetu au nao ni bora liende haswa kwa CCM........kuweza kutoa ahadi hizi hewaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
Loading...